Kwakweli umenigusa sana na wazo lako kwamba muungano uvunjwe na Zanzibar iwe nchi kama Kenya au Uganda halafu tuangalie namna tunaweza kushirikiana kama tunavyoshirikiana na nchi zinazotuzunguka hii ni dawa tosha kabisa ya hili donda ndugu

Nenda ukavunje kwanza ndoa yako!!kama huna nenda kavunje ya wazaZi wako kwanza afu ndo uje kuvunja muungano!!
 
Muungano wetu tunapaswa kuuimarisha na kuudumisha,swala la msingi ni kupiga kura ya ndio wakati ukifika wa kuipigia kura katiba inayopendekezwa kwa kuwa ndio suluhisho la malalamiko ya muda mrefu kuhusu muungano wetu ambao kimsingi ni wa kupigiwa mfano kote duniani,tujiandikishe wakati ukifika ili tufanye uamuzi sahihi
 
sasa mbona mnajichanganya nyie si ndio mliokuwa mkikataa wasijiunge na OIC na wao wanaona kuwa hiyo ni haki yao vile vile walipotaka kurekebisha katiba yao wakakataliwa sasa inamaana kuwa hakuna way out...


Tupige kura ya ndio kwa katiba inayopendekezwa,kero zote zitaisha
 
Baada ya kufuatilia masuala haya na kutafakari hasa kinacho tusibu watanzania ndani ya upinzani, nimekuja kubaini kuwa, Lipumba anatumiwa kuuweka hai muungano huu.

Takriban tangu mchakato wa katiba ulipoanza na alipokuja Samwel Sitta na karatasi zake zikachanwa hadharani katika mkutano zenji, Rais Kikwete alijuwa kuwa wazanzibari hawautaki muungano wa viraka viraka. "Think tank" ya CCM ikaingia kazini na kusuka njama ambayo ikatuletea kutoa maoni ya "Muungano tuutakao". Jaji Warioba kapewa jukumu na kamati yake kutafuta mapendekezo ya katiba kusudi tupate randama itakayo tuwezesha kupata katiba.

Sisi wazanzibari tulijuwa kuwa katiba ile ilikuwa ni "Death Sentence" kwa taifa letu na ndio maana wengi wetu tukajikita kwenye serikali tatu. Tulijuwa wazi ile "social aspect" katika yale maoni hayakuwa na maana yoyote ile isipokuwa hili suala la muungano ndio "centre Point " ya mchakato wa katiba.

Kwa asili mia 62% ambayo ndio asili mia iliokubali serikali ya umoja wa kitaifa zenji , ikataka serikali tatu. Serikali ya Tanganyika ya Zanzibar na ya shirikisho. Baada ya Jaji Warioba na Jopo lake kushindwa kufanikisha matakwa ya chama, hapa ndipo tunapoona chimbuko la Lipumba akishirikiana na Kikwete kuanza kuihujumu CUF. Katika mchakato Lipumba aliweza kuwatoa wana CUF na baadhi ya wapinzani kusudi CCM wapate 2/3 ya kura za bunge la katiba. Mungu mkubwa wakati ule hatukufahamu kilichokuwa junguni.

Kwa bahati tu, tukanusurika licha ya vyombo vya utawala kujaribu kuiba. Kwa hiyo, kama anavosema Lipumba, UKAWA ilikuwa ni kuiuwa CUF, ni kweli kabisa, ila alivopanga yeye na CCM sio ilivokwenda ila ilituunganisha wapinzani tukawa kitu kimoja. Matokeo yake ni fedheha iliokuja wakati wa kura za kitaifa ambapo baada ya jitihada kubwa za kumleta Lowassa kwenye upinzani na kuona kuwa ile njama yake itajulikana, akajitowa kwa kisingizio kuwa nafsi inamsuta. Nafsi itakusuta vipi kama upo kwenye ukweli. Lakini kwa kuwa Lipumba alikuwa sio mkweli tangu awali lazima nafsi itamsuta.

CCM walidhani Lipumba akitoka, chama cha CUF kitayumba kwa vile alipendwa sana zanzibari. Hawakujuwa kuwa Lipumba pia ni "proxy na ni Liability" kwa chama.

Hatima yake wakaona CUF imeshinda zenji kwa kiasi kikubwa sana licha ya wizi mkubwa na vitisho na chadema pia walishinda KURA za bara kwa kishindo.

Tumuulize Nape Nnauye kuhusu ushindi wa chadema na wizi wa kura uliofuatilia. Lowassa na chadema walikubali kushindwa sababu venginevo nchi ingeliwaka moto.

Ushindi wa CUF zenji, ilikuwa pigo sana na kubwa kwa chama kiasi kwamba bila ya kumtumia Jecha kufanya vituko aina ile, leo CCM isingekuwa na jina Zanzibar wala bara.
Kitu kinacho tutatiza nikuwa baada ya kura hapo Lipumba akawa ameshindwa malengo yake akaanza kutaka kujirudisha kinyemela.

Kwa bahati mambo yote haya yakifanyika ilikuwa bado ni kwa siri siri mpaka pale msajili alivotamka anamtambua Lipumba, yoote tuliokuwa tukifikiria yamedhihirika. Kesi ziliopo kortini hazina mjadala. Kama haki itafuatwa hazina uzito wa maamuzi sababu, vyombo vyote vya serikali vimejitokeza waziwazi kuwasaliti wapinzani. IKULU, BUNGE, NEC, RITA, FRANCIS MUTUNGI, JESHI LA POLISI na USALAMA wa taifa, vyote vipo upande wa LIPUMBA.

Kwa kuwa habari hizi sio siri tena, tunasubiri mahakama tuwaone majaji na wao wapo upande gani?. Korti itasimamia HAKI au itafuata CCM?.

Mawakili wa Lipumba na mawakili wa serikali wanajuwa wazi kama kesi imewalemea na wakicheza watashindwa vibaya ndio maana zinaghairishwa na huku akina Lipumba wakiendeleza hujuma.
 
Back
Top Bottom