Muungano Wa NASA wamtangaza Raila Odinga kugombea Urais na Musyoka Makamu wa Rais

its a 50 50 thing right now...it is ifficult to tell who will win...but it is very hard for a Luo to win a presidency....u will see how Kikuyus will turn out to vote in large numbers

Hapa wakenya ndio mnaniachaga hoi Du!!
mnaingiza habari za Luo au kikuyu ili iweje!!
 
mimi pia...mambo gani haya ya premier CS?
hahahaha
it seems ilikuwa ndio njia pekee wata toka na maelewano

lakini watu wata wahammer kuwa there will be cration of new offices and what or whatever!! sijajua wata answer vipi hapo
 
hahahaha
it seems ilikuwa ndio njia pekee wata toka na maelewano

lakini watu wata wahammer kuwa there will be cration of new offices and what or whatever!! sijajua wata answer vipi hapo
hawa watu wa NASA sijui mambo yao yako aje...mambo ya kuleta sijui premier CS...kiti amabacho hakiko kwenye Constitution ya nchi...yaani tuseme siasa za Kenya sio siasa...sisi huwa tunavumilia tu...
 
jumuiya ya africa mashariki inawekwa rehani kwa huu urafiki wa Magu na Raila, hizi chokochoko za kuzuia gesi ya tz kuingizwa kenya zinachombezwa na huu uchaguzi.

sielewi UKAWA watakuwa upande gani kama magu atasupport upinzani wa NASA na wao wataendea kuunga mkono mabadiliko kama ilivyo agenda ya upinzani kenya
Nimemsikia Waziri mkuu mstaafu wa Tz Mh Lowasa amewaasa wale wabunge kutoka Kenya walipomtembelea Monduli kuwa "Safari hii msifanye makosa tena"
Tafsiri ni kuwa Lowasa anaukubali umoja wa NASA.
Maana yake ni kuwa Raila anakubalika kwa Magu na kwa Lowasa.
 
hawa watu wa NASA sijui mambo yao yako aje...mambo ya kuleta sijui premier CS...kiti amabacho hakiko kwenye Constitution ya nchi...yaani tuseme siasa za Kenya sio siasa...sisi huwa tunavumilia tu...
If you went to school I thought uhuru au raila akisema kitu unatadhimi kaka. katiba inasema 22 ministries. Majina ya hawa makatibu it's your business! No 2 do you know why presidents have executive powers to issue executive orders. Mfano NAMATA was created by president uhuru last month through an executive order. Is it kwa katiba. No but it doesn't require Constitutional pathway. Chief minister is no different from a normal CS in Kenya just added responsibility by an executive order!!!
 
hawa watu wa NASA sijui mambo yao yako aje...mambo ya kuleta sijui premier CS...kiti amabacho hakiko kwenye Constitution ya nchi...yaani tuseme siasa za Kenya sio siasa...sisi huwa tunavumilia tu...
inawezekana ikawa haisumbui katiba
lazima wali consult legal officers kabla ya kutangazana hivo
sema tu inawaonesha kama they are there for vyeo kiaina
 
jumuiya ya africa mashariki inawekwa rehani kwa huu urafiki wa Magu na Raila, hizi chokochoko za kuzuia gesi ya tz kuingizwa kenya zinachombezwa na huu uchaguzi.

sielewi UKAWA watakuwa upande gani kama magu atasupport upinzani wa NASA na wao wataendea kuunga mkono mabadiliko kama ilivyo agenda ya upinzani kenya
Nimeskia Mzee wa safari ya matumaini yeye yuko bega kwa bega na Uhuru sasa naona Maneno yako yatatimia mkuu
 
If you went to school I thought uhuru au raila akisema kitu unatadhimi kaka. katiba inasema 22 ministries. Majina ya hawa makatibu it's your business! No 2 do you know why presidents have executive powers to issue executive orders. Mfano NAMATA was created by president uhuru last month through an executive order. Is it kwa katiba. No but it doesn't require Constitutional pathway. Chief minister is no different from a normal CS in Kenya just added responsibility by an executive order!!!
ni kweli unayoyasema ila hakuna kitu ambacho hawa watu wa opposition wako nayo ya kuletea wananchi...hawana sera...they are just power hungry...mabo ya kuleta sijui premier CS..i even thought itakua speaker for Wetangula...anyway, they have nt even won the thing yet..kwa hiyo tusubiri tuone matokeo...maybe they will lose
 
Siyo kweli
Hujui Serikali ya Uhuru inamashaka na Tanzania kuhusu Raila !!
Tunatoa Maoni tu hapa ni maoni Binafsi na mtazamo,
Uhuru alisha jiwekea mizizi
jambo la kushangaza ni kuwa mnajua sana kuhusu Kenyan politics...I am surprised...personally, I dont know anything abt Tanznia...just the wildlife..ikija kwa siasa..namjua tu Magufuli kwa vile alikuja Nairobi hivi majuzi...apart from that I dont know anything...nadhani ni ujamaa uliopo nchini mwenu...mtu anataka kujua kuhusu mwenzake...hapa kenya hasa nairobi utapitwa na watu ukisubiri salamu....hakuna anayejihusisha na mambo ya jirani....sasa tutayajua ya TZ aje?
 
Mpaka Sasa Raila Odinga anapewa nafasi Kubwa ya Kupeperusha Bendera ya NASA.

Kolonzo Musyoka Ametajwa katika nafasi ya Makamu wa Rais japo wengi wanataka yeye ndiye agombee Urais.

Musalia Mudavidi anatajwa katika Nafasi ya Uwaziri Mkuu kama NASA wakishinda.

KTN wana Stream Live Viongozi wa NASA wanatarajia Kufikia hapa Uhuru Pack majira ya Saa nane Kamili Mchana Huu. Ulinzi Umeimarishwa KFU wanafanya Kazi Vizuri Ikumbukwe Uhuru Pack Ipo 200M kutoka Serena Hoteli. Vijana Ni Wengi sana na Askari wapo wengi Kulinda Interference yeyote wakihakikisha Barbara inayoelekea Serena na Kulinda Usalama Wa Raia.

Watu ni Wengi sana Inanikumbusha Mafuriko ya Chama Fulani cha Siasa Pale Jangwani lakini Kikatoka Mikono Mitupu. Msaga Sumu hayupo hapa Kuna Wasanii Wengine.

Muungano wa vyama vya upinzani nchini Kenya National Super Alliance (NASA) umemteua aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga kuwa mgombea wake katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti mwaka 2017.

Bw Odinga sasa atakabiliana na Rais Uhuru Kenyatta atakayetumia chama cha Jubilee kuwania muhula wa pili.

Makamu wa rais wa zamani Musalia Mudavadi amesema viongozi wote wakuu wa muungano huo wamekubalina kumuunga mkono mgombea huyo mmoja.

"Tumekubali kwamba mpangilio huu wa uongozi ni mpangilio ambao tunataka ulinganishwe na Rasimu ya Bomas ambayo Wakenya walitaka, lakini haikuidhinishwa," amesema.

Amesema mpango wao ni kuwa wadhifa wa kinara wa mawaziri na msaidizi wake, kama ilivyokuwa kwenye rasimu hiyo ya katiba.

Mgombea mwenza wa Bw Odinga atakuwa makamu wa rais wa zamani Bw Kalonzo Musyoka, kiongozi wa Chama cha Wiper Democratic Movement.

Waziri mkuu mratibu wa shughuli za serikali atakuwa kiongozi wa chama cha Amani National Congress Musalia Mudavadi.

Naibu waziri mkuu mratibu wa uchumi atakuwa kiongozi wa Ford Kenya Moses Wetangula.

Kiongozi wa Chama cha Mashinani (CCM) Isaac Ruto atakuwa naibu waziri mkuu atakayesimamia utawala na huduma za jamii.

Mpangilio wa Upinzani

  • Raila Odinga - Mgombea urais
  • Kalonzo Musyoka - Mgombea mwenza
  • Musalia Mudavadi - Waziri Mkuu
  • Moses Wetangula - Naibu Waziri Mkuu
  • Isaac Ruto - Naibu Waziri Mkuu
Bw Odinga ni mwanasiasa anayesifika sana kwa ushawishi wake kisiasa na amekuwa katika msitari wa mbele kuunda vyama vya miungano na wanasiasa ambao ni mahasimu wake.

Odinga ni nani?
Baada ya uchaguzi wa mwaka 1997 ambapo Raila alishikilia nafasi ya tatu, kufuatia kuundwa kwa muungano wa chama chake (NDP) na chama cha rais wa zamani Daniel moi (KANU), aliteuliwa kama waziri wa kawi katika serikali ya muhula wa mwisho wa Moi.

Mwaka 2002, baada ya Moi kumuunga mkono uhuru Kenyatta, kama mrithi wake, Raila na maafisa wengine wa KANU ikiwemo Kalonzo Musyoka na wafuasi wengine, walipinga ungwaji mkono wa Kenyatta kugombea Urais.

Waliungana na kiongozi wa upinzani Mwai Kibaki na na kuunda muungano wa National Rainbow Coalition (Narc) ambao baadaye ulishinda uchaguzi wa mwaka 2002.

Raila aliungana na Rais Mwai Kibaki kuunda serikali ya Muungano ya NARC baada ya kumuondoa mamlakani rais mstaafu Daniel Moi.

Mwaka 2005 aliungana na Uhuru Kenyatta aliyekuwa kama kiongozi rasmi wa upinzani, ili kushinda kura ya maoni kuhusu rasimu ya katiba chini ya serikali ya Rais Kibaki .

Wakati Kibaki alipomfuta kazi na washirika wake, aliunda chama cha ODM ambacho kilipiga kura ya 'La' dhidi ya rasimu ya katiba mpya ambayo ilishindwa mwaka 2005.

Aliongoza kampeni mwaka 2007 na kwa shingo upande kukubali ushindi wa rais Kibaki Katika uchaguzi uliokumbwa na utata, ghasia na mauaji.

Lakini hatimaye alilazimika kujiunga na Kibaki katika serikali ya Muungano.

Disemba mwaka 2012, Raila alilazimika kupiga moyo konde na kurudiana na Kalonzo Musyoka chini ya muungano wa CORD, kwani daima husema katika siasa, hakuna maadui wa kudumu.

Raila anaamini kuwa Wakenya wanastahili kuhudumiwa vyema zaidi kuliko ahadi wanazopewa na kwamba chini ya utawala wake.

Raila anaahidi kuleta mageuzi na kuhakikisha uongozi bora.

Chanzo: BBC Swahili

Hivi Africa tulirogwa na nani, hawa viongozi wote wakuu wa NASA wanabanana wote wapate madaraka ya juu ndani ya serikali...india yenye raia 1.2+ bilioni ina Raisi, Makamu wake, waziri mkuu mmoja, sasa hawa duu hawataki kuachana kila mmoja wao anahitaji nafasi yenye ushawishi,..wakuu Raila akifanikiwa ataitupa hii Memoradum hukooo kama Kibaki baada ya uchaguzi 2002...its pathetic guys sijui wote pia wataishi Ikulu..wagebill ya NASA itafanya maisha ya wakenya wa kawaida kua really hard...
 
sasa nani ange mdefeat?, bas he is undefeated

sema mi mwenyewe sijaelewa elewa mambo ya premier CS
Kete angepewa Mudavadi na mgombea mwenza Kalonzo hao wangeuzika kiasi fulani...Raila bana haaminiki huyu..naona the Armenia ninjas wakirudi Kenya
 
Shida ya Kenya ni makabila. Raila ana nafasi kwa sababu mwaka uliopita mudavadi hakuwepo kwenye muungano wao sasa ameongeza nguvu.
 
Kete angepewa Mudavadi na mgombea mwenza Kalonzo hao wangeuzika kiasi fulani...Raila bana haaminiki huyu..naona the Armenia ninjas wakirudi Kenya
hahaha, kama kina uhuru si wa kutoka wasinge toka tu.
by the way who brings large group of voters!!?
 
Tunafuatilia siasa za Kenya kwa sababu ni siasa zinazovutia na zenye ushindani wa hali juu tofauti na mataifa mengine ya kiafrika.

Siasa za Kenya zimekuwa ni darasa kwa wananchi na wanasiasa wa Tanzania hasa chaguzi za ndani ya vyama "primary elections".

Kwani kumekuwa na ushindani mkubwa kiasi kwamba ingekuwa ni Tanzania tungeshuhudia vyama vikivunjika kwa tamaa ya madaraka lakini kwa Kenya hali imekuwa shwari.

Tuna mengi ya kujifunza kutoka Kenya - aina ya siasa na wanasiasa.

Hasa maana halisi ya maneno "siasa ni maendeleo". Kwetu sisi haya maneno bado ni msamiati lakini kwenu mmefanikiwa kufanya siasa zenye tija na maendeleo kwa taifa la Kenya.
aaaahhhhh!!!mkuu umekoleza sana..ila taifa lenyewe safi tu..kuna mengi yakujifunza kweli
 
Technically Ruto from the rich with voters Rify Valley..
teh teh
technically ndio kivipi
nadhani anaye leta kura nyingi awe flag bearer.
wao wamesema watakuwa wakiamua wote kama group, so naamini kama wakenya hawamtaki Uhuru they will rejwct him ila kama wana mtaka hakuna kusingizia eti oo RAO is this, so ngoja tuone uchaguzi utakuwaje
 
Shida ya Kenya ni makabila. Raila ana nafasi kwa sababu mwaka uliopita mudavadi hakuwepo kwenye muungano wao sasa ameongeza nguvu.
mudavadi hana lolote..ni kawaida yake kuotea hivyo..yani hajatoka siku akafanya kampeni ila hujishirikisha kwa kiongozi anayefikiri ataibuka ili apate kufaidi...
 
Back
Top Bottom