Troll JF
JF-Expert Member
- Feb 6, 2015
- 7,804
- 12,233
Mpaka Sasa Raila Odinga anapewa nafasi Kubwa ya Kupeperusha Bendera ya NASA.
Kolonzo Musyoka Ametajwa katika nafasi ya Makamu wa Rais japo wengi wanataka yeye ndiye agombee Urais.
Musalia Mudavidi anatajwa katika Nafasi ya Uwaziri Mkuu kama NASA wakishinda.
KTN wana Stream Live Viongozi wa NASA wanatarajia Kufikia hapa Uhuru Pack majira ya Saa nane Kamili Mchana Huu. Ulinzi Umeimarishwa KFU wanafanya Kazi Vizuri Ikumbukwe Uhuru Pack Ipo 200M kutoka Serena Hoteli. Vijana Ni Wengi sana na Askari wapo wengi Kulinda Interference yeyote wakihakikisha Barbara inayoelekea Serena na Kulinda Usalama Wa Raia.
Watu ni Wengi sana Inanikumbusha Mafuriko ya Chama Fulani cha Siasa Pale Jangwani lakini Kikatoka Mikono Mitupu. Msaga Sumu hayupo hapa Kuna Wasanii Wengine.
Muungano wa vyama vya upinzani nchini Kenya National Super Alliance (NASA) umemteua aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga kuwa mgombea wake katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti mwaka 2017.
Bw Odinga sasa atakabiliana na Rais Uhuru Kenyatta atakayetumia chama cha Jubilee kuwania muhula wa pili.
Makamu wa rais wa zamani Musalia Mudavadi amesema viongozi wote wakuu wa muungano huo wamekubalina kumuunga mkono mgombea huyo mmoja.
"Tumekubali kwamba mpangilio huu wa uongozi ni mpangilio ambao tunataka ulinganishwe na Rasimu ya Bomas ambayo Wakenya walitaka, lakini haikuidhinishwa," amesema.
Amesema mpango wao ni kuwa wadhifa wa kinara wa mawaziri na msaidizi wake, kama ilivyokuwa kwenye rasimu hiyo ya katiba.
Mgombea mwenza wa Bw Odinga atakuwa makamu wa rais wa zamani Bw Kalonzo Musyoka, kiongozi wa Chama cha Wiper Democratic Movement.
Waziri mkuu mratibu wa shughuli za serikali atakuwa kiongozi wa chama cha Amani National Congress Musalia Mudavadi.
Naibu waziri mkuu mratibu wa uchumi atakuwa kiongozi wa Ford Kenya Moses Wetangula.
Kiongozi wa Chama cha Mashinani (CCM) Isaac Ruto atakuwa naibu waziri mkuu atakayesimamia utawala na huduma za jamii.
Mpangilio wa Upinzani
- Raila Odinga - Mgombea urais
- Kalonzo Musyoka - Mgombea mwenza
- Musalia Mudavadi - Waziri Mkuu
- Moses Wetangula - Naibu Waziri Mkuu
- Isaac Ruto - Naibu Waziri Mkuu
Odinga ni nani?
Baada ya uchaguzi wa mwaka 1997 ambapo Raila alishikilia nafasi ya tatu, kufuatia kuundwa kwa muungano wa chama chake (NDP) na chama cha rais wa zamani Daniel moi (KANU), aliteuliwa kama waziri wa kawi katika serikali ya muhula wa mwisho wa Moi.
Mwaka 2002, baada ya Moi kumuunga mkono uhuru Kenyatta, kama mrithi wake, Raila na maafisa wengine wa KANU ikiwemo Kalonzo Musyoka na wafuasi wengine, walipinga ungwaji mkono wa Kenyatta kugombea Urais.
Waliungana na kiongozi wa upinzani Mwai Kibaki na na kuunda muungano wa National Rainbow Coalition (Narc) ambao baadaye ulishinda uchaguzi wa mwaka 2002.
Raila aliungana na Rais Mwai Kibaki kuunda serikali ya Muungano ya NARC baada ya kumuondoa mamlakani rais mstaafu Daniel Moi.
Mwaka 2005 aliungana na Uhuru Kenyatta aliyekuwa kama kiongozi rasmi wa upinzani, ili kushinda kura ya maoni kuhusu rasimu ya katiba chini ya serikali ya Rais Kibaki .
Wakati Kibaki alipomfuta kazi na washirika wake, aliunda chama cha ODM ambacho kilipiga kura ya 'La' dhidi ya rasimu ya katiba mpya ambayo ilishindwa mwaka 2005.
Aliongoza kampeni mwaka 2007 na kwa shingo upande kukubali ushindi wa rais Kibaki Katika uchaguzi uliokumbwa na utata, ghasia na mauaji.
Lakini hatimaye alilazimika kujiunga na Kibaki katika serikali ya Muungano.
Disemba mwaka 2012, Raila alilazimika kupiga moyo konde na kurudiana na Kalonzo Musyoka chini ya muungano wa CORD, kwani daima husema katika siasa, hakuna maadui wa kudumu.
Raila anaamini kuwa Wakenya wanastahili kuhudumiwa vyema zaidi kuliko ahadi wanazopewa na kwamba chini ya utawala wake.
Raila anaahidi kuleta mageuzi na kuhakikisha uongozi bora.
Chanzo: BBC Swahili