Muungano wa Malawi na Tanzania: Pendekezo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muungano wa Malawi na Tanzania: Pendekezo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by George Kahangwa, Aug 9, 2012.

 1. George Kahangwa

  George Kahangwa Verified User

  #1
  Aug 9, 2012
  Joined: Oct 18, 2007
  Messages: 539
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Wakuu,

  Naamini sote tunaendelea kufuatilia kwa makini mgogoro wa Mpaka kati ya nchi yetu na majirani zetu Malawi. Tumesikia mengi hadi sasa. Yapo yaliyo dhahiri, matharani, Malawi hawako tayari kwa namna yoyote ile kubadili mtazamo wao, nasi kwa upande wetu hatuko tayari kwa lolote lililo kinyume na msimamo tulionao kwamba mpaka wa ziwa Nyasa uko katikati ya ziwa tajwa.

  Japo kwa sasa, pande zote mbili zinadai mazungumzo ya maelewano ndio dawa (sijasikia yanafanyika wapi), yawezekana kabisa mazungumzo hayo yasizae matunda. Wawakilishi wa Malawi watapata wapi ujasiri wa kurejea kwao na kutoa taarifa kwamba wameafiki, mpaka uko katikati ya ziwa? kadhalika wawakilishi wetu wataanzia wapi kutueleza kuwa wamekubali ziwa lote (isipokuwa ile sehemu ya Msumbiji) ni eneo la Malawi?
  Matokeo ya kushindwa kuelewana yanaweza yakawa ni pamoja na kupelekana katika mahakama za kimataifa. Hata katika hilo bado kuna maswali, ni serikali gani itakuwa tayari kutoa taarifa kwa wananchi wake kwamba imeshindwa kesi mahakamani?

  Kadhalika kushindwa kuelewana kutatupeleka katika lile ambalo wengi wamekwisha kulishabikia, ikiwa ni pamoja na viongozi wetu, yaani option ya vita. Hii ni option nzito na mbaya kabisa kwa mataifa mawili yenye uchumi duni. Yamkini Malawi au hata sisi, twaweza kusema tutashinda vita, lakini hilo haliondoi uwezekano kwamba matokeo yanaweza kuwa kinyume na matarajio. Aidha, japo upande wowote waweza shinda pambano la sasa, lakini ikawa ndio mwanzo wa vita itakayodumu vizazi na vizazi, hata ikawa kwamba mataifa haya mawili yatakuwa yametumbukia katika vilindi vya ufukara ambavyo kamwe hayatajinasua.
  Katika mazingira haya, tunapaswa kufikiria option nyingine. Tutakapotafakari zaidi na kukumbuka kuwa si mmalawi wala si mtanzania aliyechora mstari huu unaotaka kutupeleka kubaya, tunaweza kusema; 'wait a minute', sisi ni ndugu, tena hilo halina ubishi, sisi sote tunaamini Afrika ni moja (rejea dhana ya panafricanism), kwa nini tusifute hiki kimstari cha mkoloni?

  Tukikubaliana hilo, jambo baya la kugombea mpaka litatuzalia jambo zuri la kuingia sasa katika mazungumzo (no matter how long maungumzo hayo yatachukua) ya kuziunganisha jamhuri zetu mbili. Hatimaye tukawa na taifa moja; MUUNGANO WA MALAWI na TANZANIA.

  Wawakilishi wetu kama mnanisoma tafadhali ...
   
 2. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Nyerer alishamwambia Banda, unataka kuchukua ziwa na Kyela? Kwa nini usichukue Tanzania yote?

  Banda akaona huyu bwana fyatu.
   
 3. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,552
  Likes Received: 1,896
  Trophy Points: 280
  Kuungana kwa wananchi always si shida,tatizo ni walioko ikulu...Ni kundi la wahuni ama magenge ambayo yakichukua madaraka kuyaachia ni kazi.Madhali kuna wenye kutaka uraisi na kuwa top kwenye maeneo hayo,basi wananchi ndo wenye kupay all the costs...yani vijinchi ambavyo ni kama mikoa tu vina shida.Mkoloni alikuwa na longer terms plans,sasa sisi hadi tushtukie ni too late.Ni kama kupigwa tobo ama kanzu,ambapo reaction yako since ni too late,inakuwa embarassing...
   
 4. George Kahangwa

  George Kahangwa Verified User

  #4
  Aug 9, 2012
  Joined: Oct 18, 2007
  Messages: 539
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Mkuu JMushi,
  Hata suala la madaraka wawakilishi wanaweza kulifanya moja ya items zitakazowekwa mezani, viongozi wa maeneo ya pande zote mbili, ambayo sasa yanaweza kuwa kama yalivyo majimbo ya Marekani au kwa Uingereza; Scotland, England na Wales, wanaweza kubaki, kisha tukawa na uongozi wa muungano, kama hatua ya awali ya kuelekea muungano usio na mstari wowote katikati.
   
 5. George Kahangwa

  George Kahangwa Verified User

  #5
  Aug 9, 2012
  Joined: Oct 18, 2007
  Messages: 539
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Mkuu Kiranga,
  Was Nyerere serious, alimaanisha muungano?
   
 6. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #6
  Aug 9, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  hata tukiunga swala la mpaka litaibuka singida na meatu kunaziwa wana gombea na ni nchi moja..dawa ni kutatua kakipande ni chetu kweli acha kiwe chetu tu..
   
 7. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #7
  Aug 9, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Tukifanikiwa kuungana itakuwa ni blow kubwa sana kwa wakoloni. Itakuwa ni mfano wa African problem being solved by africans. Hata hivyo numbers na language barrier zitawafanya wamalawi wasiwe na political significance, na hapo ndipo mang'wazi watakapoikataa idea ya kuungana!
   
 8. N

  Nonda JF-Expert Member

  #8
  Aug 9, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,222
  Likes Received: 1,957
  Trophy Points: 280
  Unafikiri Wamalawi wataamini kuungana na sisi baada ya kutathmini Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar na jinsi UAMSHO wanavyodai waachiwe wapumue?

  Kuna wapenzi wa Muungano ambao leo wanataka serikali moja tu Tz na kuita nchi ndogo mkoa.Hili ndio kosa la kuona mbali.

  Rai ya Muungano ni rai nzuri lakini turekebishe nyumba yetu ivutie ili hawa wengine wavutike kuomba kuungana nasi.
   
 9. N

  Nonda JF-Expert Member

  #9
  Aug 9, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,222
  Likes Received: 1,957
  Trophy Points: 280
  Kiswahili kinasambaa sana na pia kiengereza kinatumika. Tatizo au changamoto ni aina ya muungano/ muundo wa muungano ambao utapendeza kwa wote/ utaonekana kuwa una manufaa kwa wote.

  Kuna wanadau wanaotoa mifano kuwa US kuna states ndogo sana lakini zimeridhika kuwa katika Muungano wa US.
  Umoja ni nguvu.
   
 10. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #10
  Aug 9, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Umegonga wazo langu. Baada ya miaka 48 bado tuna mzozo wa Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar, lakini kukiwa na dhamira ya kisiasa inawezekana kwani linalouyumbisha Muungano katika TZ ni ukosefu wa dhamira hiyo kulitatua. Wazo mbadala ni kukubaliana kutofanyika shughuli zozote za utafutaji na uchimbaji wa mafuta, gesi na madini kwa faida ya vizazi vijavyo vya nchi mbili hizi.
   
 11. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #11
  Aug 9, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,059
  Likes Received: 7,275
  Trophy Points: 280
  Banda mwenyewe Fyatu,
  Kaja Na Ramani yake anamuonyesha Nyerere na kumshawishi wagawane Msumbiji.

  Nadhani walikutana!!
   
 12. ITEGAMATWI

  ITEGAMATWI JF-Expert Member

  #12
  Aug 9, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 4,222
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280
  Tuungane na wafuasi wa ushoga?Hebu kuweni serious kidogo jamani.
   
 13. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #13
  Aug 9, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,838
  Likes Received: 469
  Trophy Points: 180
  Ndiyo tujifunze kwa huyu mama, wanawake hawafai kuwa ma-rais, Getruda mongella alisikika kule AU kaajiri ndugu zake wengi.Kule Liberia yule kibibi aliyekuja juzi naye inasemekana akajaza ukoo wake ikulu na mabmo hayaendi kabisa kiuchumi.Huyu mama Banda ndiyo usisema hata mwaka hajamaliza anataka kupiganisha nchi eti anataka kuona vita vinapiganwaje.HOVYO KABISA .Leo mnataka kutuaminisha eti hakuna kama ROSE MIGIRO aluuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
   
 14. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #14
  Aug 9, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,087
  Trophy Points: 280
  mbona kuna gazeti la malawi la tar 8 imeandika mazungumzo yanafanyika tar 20 august na yanafanyika Lilongwe
   
 15. a

  anney Senior Member

  #15
  Aug 9, 2012
  Joined: Jul 9, 2010
  Messages: 156
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Good Idea George but all evidences currently support Malawi Claim of the whole lake!Ukitaka nitakutmia.
   
 16. George Kahangwa

  George Kahangwa Verified User

  #16
  Aug 9, 2012
  Joined: Oct 18, 2007
  Messages: 539
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  I have read most of them brother, to me what these 'evidences' support is ultimately a colonial blunder. Like what Mwalimu said, the insanity of it is that, the eastern shore of the lake has usually shifted towards our land. Besides, in the 1960s the Tanzanian side was flooded.
   
 17. George Kahangwa

  George Kahangwa Verified User

  #17
  Aug 9, 2012
  Joined: Oct 18, 2007
  Messages: 539
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Pengine uzoefu tulioupata, ni somo tosha kutuwezesha kuandika muungano ulio bora kabisa, tukiepuka yale yote yaliyoleta shida, huku tukiboresha yale ambayo yametusaidia.
   
 18. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #18
  Aug 9, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Nyerere alikuwa anamwambia maneno ya mzaha Banda wakati mwenzake alimjia seriously.
   
 19. Dickson Ng'hily

  Dickson Ng'hily Verified User

  #19
  Aug 9, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  Mazungumzo yapo na hata kuna hiki kikao kitakachofanyika trh 20/08/2012 huko Malawi Kaskazini katika mji wa Mzuzu....Tuombe Mungu haya yaishe kwa mazungumzo na inawezekana kabisa kuisha bila hata kwenda mahakamani...
   
 20. Nsabhi

  Nsabhi JF-Expert Member

  #20
  Aug 9, 2012
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 1,096
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kwame Nkrumah aliliona hili mapema na kusema kuwa tunagombania vijimipaka vilivyochorwa na wakoloni kwa nini tusiwe na United States of Africa?Nkrumah alidhamiria lakini wenzake wakamgomea! Na kwa sasa ni ngumu kwa Afrika au baadhi ya nchi za Afrika kuungana kwa sababu ya ukoloni mambo leo ambao unatumia dhana ya divide and rule.Wazo la Kahangwa ni zuri ila halitekelezeki kwa sasa hadi pale tutakapojinasua kutoka kwenye makucha ya nchi za kibeberu ambazo zinafurahia kutengena kwetu.Wao kila kitu kinachotokea Afrika ni dili na tukianza vita watatuuzia silaha na kama watependa vitavisiwe na ukomo nao wataendelea kutuuzia silaha bila kikomo.
   
Loading...