Muungano umejaa maswali yasiyo na majibu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muungano umejaa maswali yasiyo na majibu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 9, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 9, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=2][/h]Alhamisi, Septemba 06, 2012 07:36 Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
  [​IMG][​IMG][​IMG]

  Pamoja na kujitokeza kwa baadhi ya wanasiasa wasiokubali kuwepo kwa kasoro za msingi katika Muungano ukweli milelele utabaki mahali pale pale kuwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar una maonevu dhidi ya Zanzibar.
  Kwa kweli si Muungano wa haki, umekosa usawa na zaidi ukiikandamiza na umelikosesha uwakilishi Taifa la Zanzibar katika Umoja wa Mataifa.

  Jambo hili limeifutia hadhi, heshima na historia iliyotuka ya visiwa vya Zanzibar ambavyo viliunda dola miaka mingi iliyopita kabla ya Tanganyika kujulikana.

  Hata kama uwakilishi wa Zanzibar awali kabla ya Mapinduzi uliongozwa na Utawala wa Kisultan, bado jina la Zanzibar ndilo lililokuwa likifahamika kimataifa na si la ufalme na himaya yake uliohamia Zanzibar kuanzia mwaka 1832.

  Wakati huo hakuna aliyekuwa akizifahamu nchi za Tanganyika, Kongo, Kenya au Uganda, bado mawasiliano, maendeleo na ustaarabu wa maeneo hayo karibu kote yalitegemea kila kitu kutoka Zanzibar.

  Inapotajwa nchi ya Misri kama ni ya kwanza kustaarabika duniani, ustaarabu pia katika Afrika kitovu chake kinaanza Zanzibar na matunda yake kuenea maeneo mengine ya Bara hili. Hilo halina ubishi!

  Zanzibar na Misri ni mataifa yaliyopata bahati ya kufikiwa mapema na dini, muziki, maendeleo ya kilimo, viwanda, uvuvi na biashara kuliko shemu nyingine Afrika.

  Hakuna mjinga asiyejua kuwa Taifa la Tanganyika hadi leo hii liko hai ila limejificha nyuma ya kivuli cha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huku Zanzibar ikipoteza asili ya utambulisho na umaarafu uliokuwepo kimataifa.

  Msingi wa Muungano wa April 26, 1964 unafahamika na kila mwerevu, ASP chini ya uongozi wa Rais wake Abeid Amani Karume, Serikali yake iliafiki pendekezo la Muungano kamagube kutokana na hofu ya kupinduliwa.

  Upo ukweli kuwa manifesto ya ASP wakati ule, iliaanisha baadhi ya mambo na kusema wakipata madaraka ya utawala wataungana na waafrika wenzao kujenga Umoja. ASP hakikusema kama kitaungana na Tanganyika ima fa ima, la.

  Akitokea mtu mbishi niko tayari kukutana naye ana kwa ana ili kumuonyesha maandishi yaliyomo kwenye vijitabu vya chama hicho katika ahadi yake hiyo za msingi na kwa mujibu wa Katiba yake.

  Serikali ya Karume haikuwa na kundi kubwa la wasomi kama lile la ZNP au ZPPP, njia yoyote ya wao kujitawala wenyewe bila ya kupata msaada wa wengine lilikuwa ni jambo lisilowezekana na kusema wanayo Serikali.

  Karume ni Rais ambaye elimu yake kwa sehemu kubwa ilikosa maarifa ya utawala, alikuwa akiwachukia wasomi, kwa bahati mbaya alizungukwa na kundi la viongozi wahamiaji waliokuja toka maeneo tofauti na kuishi Zanzibar

  Abdallah Kaujore, John Okello, Seif Bakari Omar, Abdallah Natepe na Mohamed Mfaranyaki ni kati ya viongozi wa ASP ambao hawakuwa raia na hawakuzaliwa Zanzibar. Hawa ni kati ya washauri wake wa kuongoza Serikali yake.

  Naamini ndiko kulikouponza utawala wake uliodumu kwa miaka minane toka mwaka 1964 hadi 1972 na kuufanya usifike mbali. Kama alivyoipindua Serikali ya vyama vya ZNP na ZPPP mwaka 1963 na yeye akapigwa risasi.

  Nia ya Rais Karume na viongozi wa ASP kukubali Muungano ilifahamika, kwanza walihitaji kujihakikishia ulinzi wa ndani, usalama wa Serikali yao pia mara zote wakihofia kupinduliwa na kundi la wazanzibari wasomi ambao hawakuwa ASP.

  Jambo hilo ndilo lililoifanya Serikali ya ASP kukubali haraka haraka kujiunga na Tanganyika. Hapo ndipo Rais Julius Nyerere alipouutumia mwanya huo kuiteketeza Zanzizbar kimaendeleo na kuifutia uwakilishi wake Kimataifa.

  Viongozi wa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi Zanzibar baadhi yao bado wana hofu hiyo baada ya miaka 48 kupita. Wanaamini kuwa nje ya Muungano ati Zanzibar inaweza kupinduliwa. Jambo la kujiuliza ziko wapi Serikali za Mapinduzi zinazotambuliwa hivi sasa?

  Andy Rajoilinar wa Madagascar tokea ampindue Marck Rovalmanana mpaka sasa hajawahi kutoka nje ya nchi yake kuhudhuria kikao cha AU wala hakuna ofisi za balozi zinazoshirkiana na Serikali yake.

  K
  ila mmoja ni shahidi. Hata NEC ya CCM kwenye kabrasha lake limeainisha mambo mengi ya msingi ambayo ni kero tupu, karibu yote ni yale yanayoonekana kuikandamiza Zanzibar kimaendeloa hususan katika milango ya kiuchumi.

  Mambo hayo na mengine ambayo yameonekana zamani sana katika Ripoti ya Tume ya Jaji, Francis Nyalali, Wiliam Shelukindo, Jaji Robert Kisanga na nyinginezo, huo ni ushahidi kuwa Muungano umejaa kasoro za kutisha.

  Matatizo ya Muungano hayaanzii katika jukwa la utoaji na ukusanyaji wa maoni ya wananchi juu ya kuundwa kwa Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwanza kabla ya kifo cha Karume kulikuwa na mivutano ya chini kwa chini.

  Rais Aboud Jumbe aliyaanisha kwa utaalam matatizo mengine mwaka 1984 , kundi la watu wanane waliofukuzwa CCM mwaka 1988 akiwemo Seif Sharif Hamad na wenzake walielezea hofu yao juu ya mwenendo dhaifu wa Muungano pia kundi la wabunge wa CCM lililojiita G55.

  Seif pamoja na wenzake ingawaje walimsalati Rais Jumbe mbele ya Nyerere, bado kulikuwa na utata katika Muungano ambao leo tena baada ya miaka 48, mambo yameibuka upya huku mara hii yakizungumzwa bila ya hofu.

  Ikiwa CCM nia yao kweli ni kuwafukuza wanachama wake wanaosema kweli kinyume na utashi wao wa kisiasa, yatawakuta makubwa kuliko yale yaliyotokeea baada ya mwaka 1988 walipofukuzwa wale wanane.

  Kosa kubwa lililofanyika mwaka ule ni kuwafukuza wanachama hao, pengine bila ya uamuzi ule kupita,S eif asingeweza kupata umaarufu huu alionao sasa .

  Naota ndoto kuwa ikiwa CCM watajaribu kufanya siasa za kihafidhina na kuamua kuwafukuza wengine, kundi hilo litakuwa ni maarufu maradufu kuliko ilivyotokea kwa Seif kitaifa na kimataifa.

  Chama cha siasa cha kisiasa ni lazima kikubali kusikiliza maoni, mawazo na michango hasi na chanya. Mawazo tofauti dhambi kusikiliza ila kosa lake huja pale mtu anaposhindwa kujibu kwa hoja.

  Kujenga hoja na mtu kujibu kwa na uthubutu wa kujibu hoja kwa nguvu ya hoja ni matarajio yatokanayo na ukomavu aidha kwa anayeuliza kwa hoja au kujibu hoja kulingana na upeo wa mhusika kunakoambatana na kujua hoja yakinifu.

  Nafikiri hiyo ndiyo modenaizesheni ya kila chama cha siasa kulingana na muktadha wa matakwa ya wakati. Anayeshindwa kumjibu mwenzake kwa hoja huwa amepungukiwa majibu ya msingi. Mtu wa aina hiyo yatosha kwake aitwe si mwanasiasa wa dunia ya sasa.

  Wanaojitokeza na kutaka kujibu hoja za matatizo ya Muungano kutokana na nguvu ya hoja inayojengwa na wanaodai kuwa kuna utata katika Muungano ni lazima wajibiwe kwa majibu ya hoja.

  Inashanga unapomsikia mtu anajaribu kujibu nguvu ya hoja kwa hoja dhaifu akiufananisha Muungano wa mataifa na viungo katika kiwiliwili cha binadamu, huku kwa kweli ni kupungukiwa na uzito wa hoja ili kuijibu hoja kwa wepesi wa jibu la hoja husika.

  Yapo matatizo makubwa katika Muungano. Mwanzoni walioanza kuhoji masuala haya walitishwa na kuambiwa kuwa kuhoji masuala hayo ni sawa na uhai. Matarajio toka kwa waliokuwa na majibu hayo walifikiri watafanikiwa kuviza mawazo ya binadamu wenzao.

  Nafikiri walifanikiwa kuyakandamiza mawazo hayo kwa wakati fulani, wakashindwa kwa wakati wote, sasa mambo yameibuka upya yakiwa hayana majibu stahili kulingana na wingi wa kosaro katika Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

  Nguvu ya kwanza ya CUF ilitokana na uzembe wa viongozi wa CCM, ikiwa CCM itaamua kukubali kuyarudia makosa yae yale, waamini kuwa watakipa tena chama hicho nguvu ya pili ambayo naamini hawatamudu kuizuia.

  Matokeo ya uamuzi huo utasababisha kundi jipya kutengewa nguvu mpya himaya yao itakayojimega kutoka mbavuni mwa CCM na kuunganisha ile iliyokuwepo, hapo ndiyo utakapokuwa mwisho wa chama hicho Zanzibar.

  Jambo hili kwa mtazamo wangu kisiasa halitakiwi kuamuliwa kwa misingi ya chuki, jazba na hamaki, ni jambo linalozungumzika kama lile la mwelekeo wa kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar lilivyokuwa na mtazamo hasi pale awali. Ila mwenye macho haambiwi tazama

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Sep 9, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Kila siku nikisoma habari kuhusu MUUNGANO napata Sababu MPYA KWANINI au SI KWANINI Mzee KARUME aliukubali

  MUUNGAO au KUUKATAA Historia nzuri kweli.
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Sep 9, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  maswali yangu mimi nihaya

  1.kwa nini nchi ya watu millioni moja
  ilete wabunge zaidi ya 50 wakati daresalaam peke yake ina watu zaidi ya milioni tano
  na wabunge hawafiki nane?

  2. kama kweli hawakuwahi kuuridhia muungano...basi ipigwe kura ya maoni waulizwe

  3.mapinduzi ya Zanzibar yalipindua serikali ya kuchaguliwa kidemokrasia huko Zenji
  sasa haki ya kuulilia na kuulinda huu muungano inatoka wapi?

  4.Kwani lazima uwepo?uukivunjwa tutakosa nini?
   
 4. M

  Murrah Senior Member

  #4
  Sep 9, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwandishi angalia facts zako vizuri nchi za kwanza kustaaribika africa sio zanzibar kilwa, mombasa, lamu, sofara,mali, songai, benin misri na ethipia zimestaaribika karne nyingi hata kabla zanzibari haijakaliwa na watu na wala si kokopi ya waarabu. Before you put your craap here check historical facts first na sio utuletee mambo ya uamsho hapa
   
 5. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #5
  Sep 9, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  kasoro zipo kwa vie watu kama nyie mpo.Ila hakuna kasoro isiyokuwa na jibu.Hapa kuvunja muungano au kufanya taifa moja ndio jibu.

  Hujakosea kuwa hakuna usawa ila si usawa huufikiriao.bara imenyonywa sana na kuliko unavyodhani.Wazanzibar mmelikorga wenyewe kwa kushindwa face ukweli hasa pale shida zetu mlizozitafuta wenyewe kulazimish akuwa zililetwa na muungano.

  Nadhani na wewe uache propaganda ukafanye halali na si kunung`unika tuu unataka serikali ikue kila kitu hadi hela ya mahri?Kila mtu akiwa kama wewe nanai atafanya kazi ya kuipatia serikali kodi?
  zanzibar haijawahi pata heshima inayopata sasa hivi, au unazungumzia umaarufu?well, kiswahili hakina equivalence ya haya maneno "famous" and "infamous".Biahsara ya Utumwa ndio ilishikilia uchumi wa sulatan wa Zanzibar,Kingine ni madanguro na sauna/spice baths, baadaye karafuu ikaongeza ajira nyingine ya utumwa mashambani.Yote hayo yanaifanya zanzibar kuwa infamous.
  Mwaka 1600 USA si tuu haikuwepo pia haikuwa ikijulikana kama UK?

  Hembu tuambie nini kilitegemewa toka zanzibar..?gold? mchele?university?Ndizi? samaki?....nini.Hata karafuu si dili sana ukitoka nje ya pwani.Kilwa bagamoyo,tanga, etc hazikuwa zanzibar sasa mawasiliano gani unataka sema.
  Upo ubishi, kwani Kilwa ndio ilitangulia Zanzibar.Tunaomba usitudanganye kwa propaganda kama za waarabu kuwa ulaya waliiba ustaabu na techologia toka arabuni.Hizo ni habari za kudanganya mateja.

  Zanz ilitisha kwa vile ilikuwa hub ya unyama wote wa bara na soon bara wakizubaa hayo yatarudi....yaani sultan akibwata(baragumu)kutaka watumwa na vipusa maziwa makuu watu wanasulubika kupoteza ndugu zao kwa utumwa na wanyama.hiyo link imekatwa sijui ujiji sijui kalenga, sijui na tabora,hakuta tena mamluki wa kubeba watu.wamebaki aina ya watu kama yule jamaa wa arusha anayepeleka watu arabuni .
  Nani kakuambia?Jamii za Aztec iliyo mexicle ya leo, na wengine kama may katika south america.Walikuwa na pyramids long time, walikuwa na michoro ya mingi na kilimo kwa sana.jamii za kichina nazo zina miaka kibao.

  By the way dini gani unasema sasa?Mistry walikuwa na dini za asili ,baadaye wengine wakachukua uyahudi, halafu wakawa Wakristu, ndio Uislam.Sijui unamaanisha ipi hapa?

  Zanzibar walifanya utumwa na uchangudoa(madanguro na mabafu ya viungo) na karafuu kwa sultan tuu....na jamii zilizokuwepo zilikuwa nyingi tuu za kiasia.Sijui dini yako ilichangia nini katik haya?
  Hujakosea kwani mwerevu haoni kama ni issue.Pengine watashangaa mbona bado Zanzibar bado ipo hai.Ila watu wake hawaoni wala kujitambua.
   
Loading...