Muungano: Siku za maisha yake zinaelekea ukingoni? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muungano: Siku za maisha yake zinaelekea ukingoni?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Filipo, Jun 28, 2011.

 1. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Nimefuatilia magazeti ya leo nimeona wabunge wawili wa bunge letu wakisema muungano uvunjwe! Ingawa spika amewaambia mawazo yao wayapeleke kwenye kamati ya katiba, ukweli unabaki kuwa wabunge na wananchi wengi wa upande mmoja wameonesha wazi kutokuubali muungano na kwa nafasi hii ya kuandika katiba mpya, nadhani siku za muungano sasa zinahesabika!
  Naomba kuwasilisha.
   
 2. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2011
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,097
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  uvunjwe hiyo ndio infinite solution kwa sasa though kuna imapact nyingi lakini naona ni headache tu .tuvunje tuangalie wapi makosa tutarudi kama EAC ..
   
 3. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Jamaniiiiii..........uvunjweeeeeeeee
  anaeogopa si jasiri na muoga wa KUFANYA MAAMUZI MAGUMU
   
 4. M

  Marytina JF-Expert Member

  #4
  Jun 28, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  uvunjwe tena leo hii
   
 5. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #5
  Jun 28, 2011
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Ishakua nivunje kikombe nisivunje? ila wadau wataathirika hawa....
   
 6. Andrew Kellei

  Andrew Kellei JF Gold Member

  #6
  Jun 28, 2011
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Uvunjwe tujipange upya.Tumechoka kuwabeba hao madogo.Utakuta mtu ana F ya English halafu yupo higher learning institution.Ukiuliza wanakwuambia wanatafuta usawa na mgawanyo wa rasilimali nchi.
   
 7. A

  ALI KIBERENGO Member

  #7
  Jun 28, 2011
  Joined: Jun 20, 2009
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kivunjwe kikombe wazanzibari katu daima dawamu hawatoathirikaaaaaa
   
 8. Averos

  Averos JF-Expert Member

  #8
  Jun 28, 2011
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 648
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  Suala la muungano lina interest ya wamagharibi, kwa hivyo linakuwa gumu sana kuamuliwa na watanzania wenyewe, that's why watawala wetu wako tayari kuulinda muungano kwa gharama yeyote. wataishia tu kurekebisha hiki na kile ila kufikia maamuzo ya kuuvunja ni ndoto.
   
 9. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #9
  Jun 28, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mkuu kuathirika wazanzibar sizani kama ni kweli, ila kunafaida nyingi kwao kuliko hasala wazanzibar wamedumaa kimawazo na rigavament la kifisadi la muungano, liserikali lililojaa wizi na ubabaishaji mwingi, miaka ya 90 zanzibar ilikuwa ni mji wa biashara kwa afrika mashariki watu walikwenda kufunga mizigo zanzibar, na kwaujumla wale watu ni innocent sana tuu, sisi ndo tunawachafua i think ningekuwa mzanzibar ningeandamana muungano uvunjike tuu.
  Selikari yenyewe ya muungano utani mwingi sana hakuna mtu ambaye yupo makini kama pinda mwenyewe kapinda tuu!
   
 10. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #10
  Jun 28, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  impact kwa wa zenji, uvuuunjweee..
   
 11. Makoye Matale

  Makoye Matale JF-Expert Member

  #11
  Jun 28, 2011
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 6,480
  Likes Received: 450
  Trophy Points: 180
  Hapa hatuhitaji kuuma maneno, Wazanzibari kimsingi hawahitaji Muungano, baadhi ya Watanganyika bado wanaukumbatia haijulikani kwa maslahi ya nani. Tanganyika ni nchi kubwa kuliko nchi yoyote hapa Afrika Mashariki na ina fursa za kutosha kabisa, kuungana na visiwa vidogo kama Unguja na Pemba ni kama kuwameza watu wa hako kataifa kadogo na ndivyo wanavyojisikia.

  Tuwaache waende zao kama alivyosema Mwalimu, kulingana na hali ya kisiasa visiwani humo sina shaka tutasikia Jamhuri ya watu wa Pemba na Jamhuri ya Zanzibar hata miaka miwili haifiki baada ya kuvunja huu Muungano. Naamini wengi watajuta kwa uamuzi wa kuvunja Muungano watatamani kurudi lakini watakuwa wamechelewa sana.

  Wazanzibari jifunzeni kutoka kwa mataifa jirani Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi wanatamani sana kuungana nasi kuwa shirikisho ili watumie fursa zilizopo Tanganyika, ninyi kwa sababu mmezaliwa na kukulia ndani ya Muungano hamuyaoni haya. Wabunge wa Zanzibar kama hawahitaji Muungano wawasilishe hoja binafsi bungeni, bunge litajadili na kuwasilisha serikalini na baadaye itapitishwa kura ya maoni ili kufikia uamuzi wa mwisho kama ilivyofanyika huko Sudan.
   
 12. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #12
  Jun 28, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kweli uvunjwe kwa kuwa tutafaidika na haya yafuatayo:
  1. Ufisadi utaisha,
  2. Barabara zitajengwa,
  3. Zahanati zitajengwa kwa wingi,
  4. Shule za Sekondari za Kata zitafaulisha na kushika namba moja,
  5. Wezi kwa jina la uwekezaji hawataiba tena madini yetu,
  6. Mgawo wa umeme utakuwa historia,
  7. Wanyama hawataibiwa tena toka kwenye mbuga zetu,
  8. Uchumi hautakua tu kwenye karatasi bali maisha ya wananchi mmoja moja wataboreka,
  9. Rais wetu ataangalia matatizo ya nchi yetu badala ya kuzurura nje ya nchi,
  10. Bajeti yetu haitakuwa tegemezi tena,
  11. ....nk
  Hongereni sana wapinzani wa Muungano na mjiandae na consequences za uhaini!
   
 13. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #13
  Jun 28, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Wazazimbari wana akili wameona kuzidi kuwa na muungano usio na maendeleo hakuna haja yoyote. Yes ufisadi umekuwa kama dini na sisi wa bara ndiyo waasisi na waumini wakuu wa dini hii.

  Bora wajiondoe tu ili wasonge mbele watuache sisi na sera zetu za kulindana lindana. Tuvune tulichopanda.
   
 14. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #14
  Jun 28, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  Ungevunjwa hata dakika hii,hivi kwanza unafaida gani,sanasana wenzetu wazenj wataumia sana,nawaonea huruma
   
 15. V

  Vonix JF-Expert Member

  #15
  Jun 28, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 1,988
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Ulivunjika muungano wa urusi utakuwa huu?????kwanza ulianzishwa kwa ridhaa ya nani????unaanzisha kitu kwa nguvu ukidhani kitadumu wapi!!!it is just a matter of time.Nakumbuka hotuba ya Marehemu Mwalimu JK alipokuwa akiagwa kichama pale Dodoma akiwa na hofu ya watu kutaka kuuvunja muungano alisema ''aaaaah salimini acheni wengine tufe kwanza ndipo muuvunje muungano''sababu kubwa ya kuanzishwa kwake tunaambiwa ni kuilinda zanzibar isivamiwe kitisho hicho bado kipo???????ni muda mwafaka kuuvunja,ni ndoa iliyojaa malalamiko kila kukicha mnasuluhisha hili linazuka jingine kerooooooooooooooooooooooooooooooooooooo!!!!!!!!!!!!!!
   
 16. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #16
  Jun 28, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Haaa haaa! Wazenj wanaandika posts na kujifanya Wabara, kaaaazi kweli kweli!
   
 17. bemg

  bemg JF-Expert Member

  #17
  Jun 28, 2011
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,706
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Muungano wa sasa wakuwa na serikali ya Muungano na ya mapinduzi zanzibar hauna tija.kama tunapenda kuwa na muungano tuwe na serikali moja
   
 18. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #18
  Jun 28, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,892
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  tatizo ni ufisadi uliokithiri!!! ....japo wengine wanafananisha muungano wetu kama "chatu aliyemmeza mbwa kabla ya kumuua", na hataki kufa humo tumboni na wanadhani kumtema ndio suluhisho! UFISADI, UFISADI, UFISADI!!!!
   
 19. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #19
  Jun 28, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Weka hotuba ya Nyerere hapa ili tuone hayo maneno, othwerwise wewe utakuwa ni mzushi wa kutupwa!
   
 20. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #20
  Jun 28, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Wanaumia kwa sababu ya "dhambi ya ubaguzi" inawatafuna, hakuna kingine!
   
Loading...