MUUNGANO: Ipigwe kura ya maoni Tanzania nzima. Ndoa za walokole zinavunjika sembuse ya mkeka?

Chilisosi

JF-Expert Member
Oct 19, 2008
3,051
747
Ndugu zanguni,

Nimekaa chini nimejiuliza nimekosa jibu
Kwa nini kila kukicha huu muungano hauishi manung'uniko?
Walianza wa zanzibari na sasa wabara wanataka muungano uvunjike ni kwa nini hasa?
Tuliungana tukiamini kuwa sote ni ndugu na sasa tatizo ni nini?

Mimi naona itakuwa vyema kama serikali ikiitisha kura ya maoni nchi nzima ili tuone kama tunautaka au hatuutaki huu muungano halafu kura zikiishahesabiwa kama zinazosema Uvunjike zinazidi asilimia 50 basi uvunjike na zikiwa chini basi usivunjike kamwe na iwe mwisho wa kelele za muungano.

Nyote mnajua hakuna guarantee ya ndoa kudumu milele kwani zinavunjika hata ndoa zilizofungwa Kanisani/misikitini sembuse ndoa za kiserikali?

NDOA YENYE KELELE NI HATARI KWA WANANDOA.
images
image056.jpg

UZALENDO KWANZA!
 
Mkuu wangu Chilisosi naunga mkono hoja by 100%, Maana mpaka hapa tulipofika tushachoka na matusi ya Jussa na Seif mara waseme Tanganyika ni mkoloni mweusi, Sasa huu ndo muda wa kufanya maamuzi magumu ikibidi.
 
Naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja. Briliant idea.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Mkuu wangu Chilisosi naunga mkono hoja by 100%, Maana mpaka hapa tulipofika tushachoka na matusi ya Jussa na Seif mara waseme Tanganyika ni mkoloni mweusi, Sasa huu ndo muda wa kufanya maamuzi magumu ikibidi.
Mkuu huu Muungano utakuja ku cost maisha ya watu bure,
Ni afadhali tuuvunje sote tuishi kibachela tu , mtu unajiamulia cha kufanya bila kujali mwingine atalalamika au kuona kapunjwa
 
Me naona uvunjwe tu tujue tunaanzia wapi manake tumeshachoka na kelele,wakiambiwa kama wanataka au hawataki wanasema muungano uwepo ila muundo ubadidilike.Me naona uvunjike maana tutakua na amani.
 
Siungi mkono, naogopa kwa sababu ni dhahiri baada ya kuvunijika muungano tutaanza kupokea wakimbizi kutoka zanzibar kwa kasi ya ajabu. NIULIZENI KWA NINI KM KWELI HAMJUI SABABU
 
Mkuu huu Muungano utakuja ku cost maisha ya watu bure,
Ni afadhali tuuvunje sote tuishi kibachela tu , mtu unajiamulia cha kufanya bila kujali mwingine atalalamika au kuona kapunjwa

Ha ha haaaa! Na ile ndoa ya CCM n CUF itakuwaje??? Ndo talaka tatu au??
 
Jamani tusiwaudhi waasisi wa muungano wetu.
Mkuu mimi nawanezi na kuwapenda sana waasisi wetu na kamwe sitafurahi kuona wamekwazwa.
Lakini nina uhakika kama wangekuwa hai wenyewe wasingependa kuona watu wanapoteza maisha yao kwa sababu ya muungano.

Leo hii mimi binafsi naogopa kwenda Pemba kutembea kwa sababu ni mbara sasa haya maisha gani?
 
Km huwezi kwenda kwa kuogopa huo ni Ujinga wako!cz Pemba wapo Watanganyika wengi tu tena wakatoliki wala hawaguswi na tunachanganyika nao!
mm binafsi maziwa ya Ng'ombe ya mwanangu nanunua kwa mkiristo wala hakuna tatizo na ananiletea mpaka Nyumbani!
Hizo ni propaganda za Baba yako wa Taifa JKN!
Hapa Mada ni Mamlaka Kamili ta Zanzibar Shengesha Baadae!!!
 
Mkuu mijadala inaendelea imani yangu tutafika pazuri tu mungu yupo upande wetu daima tumevuka sehemu nyingi hata hili tutalishinda.
 
Km huwezi kwenda kwa kuogopa huo ni Ujinga wako!cz Pemba wapo Watanganyika wengi tu tena wakatoliki wala hawaguswi na tunachanganyika nao!
mm binafsi maziwa ya Ng'ombe ya mwanangu nanunua kwa mkiristo wala hakuna tatizo na ananiletea mpaka Nyumbani!
Hizo ni propaganda za Baba yako wa Taifa JKN!
Hapa Mada ni Mamlaka Kamili ta Zanzibar Shengesha Baadae!!!
Ni hivi,
Sisi hatutaki kuwa nanyi tena, tumechoka, tunataka tanganyika iwe peke yake kama zamani
Nyie si mlilianzisha? sasa unaogopa nini tena yakhe!
 
Mm kinachonishangaza ni Watanganyika kukosa Uzalendo wa Taifa lao!!!
Ss waZanzibar ni Wazalendo ndio mana tunadai mamlaka kamili ya Taifa letu ss kwa nini nyinyi waTanganyika hamdsi chenu!!?
Huku Zanzibar hasa kunanini?mpaka ikawa mnatung'ang'ania hivi!!?
 
Hivi wewe mpaka sasa hunielewi tu??
Sisi hatuutaki huu muungano tunadai tanganyika yetu sasa wewe kinachokuuma nini wakati sisi tunadai nchi yetu kama mnavyodai nyie, au mnataka muwe na nchi yenu halafu muwe na pia mna Tanganyika?
 
Ni hivi,
Sisi hatutaki kuwa nanyi tena, tumechoka, tunataka tanganyika iwe peke yake kama zamani
Nyie si mlilianzisha? sasa unaogopa nini tena yakhe!

Na ss pia tushachoka ukoloni wa Tanganyika vunja Muungano wa Dhulma mbalini!hakuna anayeogopa hapa ss tuko wazi hatufichifichi msimamo wetu!
ZANZIBAR KWANZA SHENGESHA BAADAE!!!!
 
Siungi mkono, naogopa kwa sababu ni dhahiri baada ya kuvunijika muungano tutaanza kupokea wakimbizi kutoka zanzibar kwa kasi ya ajabu. NIULIZENI KWA NINI KM KWELI HAMJUI SABABU

Idadi ya wa-Zanzibar walioko Tanganyika inakisiwa kuwa zaidi ya walioko Zanzibar. Pili, Muungano utakapovunjika wasidhani wataendelea kubaki Tanganyika kwa uhuru kama ilivyo sasa; watabanwa moja kwa moja na sheria za uraia na uhamiaji hivyo itabidi warudi kwao labda kwa wale watakaochagua uraia wa Tanganyika.

Nne, sheria muflisi ya "uraia wa nchi mbili" inayopigiwa upatu na Membe marufuku; itatuletea matatizo na hawa jamaa. Tano, endapo watavurugana huko kwao baada ya Muungano kuvunjika, watakaobahatika kuvuka bahari wasidhani wataelekea Kariakoo na Ilala kama ilivyo sasa! Wakionewa sana huruma ni moja kwa moja makambini huko Kongwa, Kiteto, au Nachingwea. Wanapaswa kulijua hilo kwa mapana na marefu yake.
 
Back
Top Bottom