Chilisosi
JF-Expert Member
- Oct 19, 2008
- 3,051
- 747
Ndugu zanguni,
Nimekaa chini nimejiuliza nimekosa jibu
Kwa nini kila kukicha huu muungano hauishi manung'uniko?
Walianza wa zanzibari na sasa wabara wanataka muungano uvunjike ni kwa nini hasa?
Tuliungana tukiamini kuwa sote ni ndugu na sasa tatizo ni nini?
Mimi naona itakuwa vyema kama serikali ikiitisha kura ya maoni nchi nzima ili tuone kama tunautaka au hatuutaki huu muungano halafu kura zikiishahesabiwa kama zinazosema Uvunjike zinazidi asilimia 50 basi uvunjike na zikiwa chini basi usivunjike kamwe na iwe mwisho wa kelele za muungano.
Nyote mnajua hakuna guarantee ya ndoa kudumu milele kwani zinavunjika hata ndoa zilizofungwa Kanisani/misikitini sembuse ndoa za kiserikali?
NDOA YENYE KELELE NI HATARI KWA WANANDOA.
UZALENDO KWANZA!