Muungano hatuutaki Wznz na mulizeni Samuel Sitta anaujuwa ujumbe wetu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muungano hatuutaki Wznz na mulizeni Samuel Sitta anaujuwa ujumbe wetu.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Nov 22, 2011.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Nov 22, 2011
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [h=1]Mh Abou Jee kuna uhalali gani wa Katiba hii wakati mshirika wa huo Muungano wenyewe kizani(hayupo)?.[/h]Written by Hassan10 // 22/11/2011 // Habari // No comments

  [​IMG][​IMG]Mh Aboubakar acheza na Nyoka wenye sumu kali kwa Zanzibar.

  Mimi naona viongozi wapotolewa na badae kutupumbaza na sisi wananchi, Swala langu ni hili Jee kuna faida gani ya katiba kwa Zanzibar wakati Muungano wenyewe haupo wameshauvunja hao wajanja wasemao tulinde Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
  Kwa nini viongozi wetu wa Zanzibar wanachindwa kusema kwa vitendo kuwa hakuna tena Muungano ulokuwa ukiitwa wa Tanganyika na Zanzibar kwa hio katiba hai resist tena Zanzibar kwa vile Tanganyika haipo.
  Wzanzibar hakuna sababu ya kwenda mbali wakati pafupi pako kujadili pako, nikusema kwa nguvu zote Baraza la Uwakilishi kuwa Rudisheni Tanganyika tujadili upya Muungano sihivyo basi hatuko tayari Wzanzibar kusulubiwa kwa jina la Tanzania.
  Ikiwa Waziri wa sheria na Katiba Mh Aboubakar anasema tujipange vizuri Wzanzibar kujadili katiba mpya ? jee vipi hatma ya Zanzibar ktk Muungano wakati katiba imeshaeleza wazi wazi kuwa Muungano usiguswe ktk mambo 3 alio yataja Kikwete ?.
  Na katiba imempa nguvu Kikwete bada ya mchakato wote wa kujadili katiba basi anao uwezo wakukubali au kuvibataa vipengele yeye binafsi.
  Jee pindipo Wzanzibar wakasema wamechoswa na Muungano huu na kero zake na wanatako maoni yao nikuvunjwa vipi Mh Abou hili wakati Raisi wa Muungano amepewa uwezo wakupinga chochote bila kuingiliwa?.
  Mimi nahisi viongozi wetu washe unafiki na wajifunge kibwebwe kumtafuna Jongoo kwa meno ili waseme tujadili Tanganyika sio Tanzania, ikiwa hili lina uzito kwenu basi turudishieni Wananchi dawa tunaijuwa na tiba itapatikana kwa kipindi kifupi tu.
  Tutumie turufu yetu ya kura ya maoni ili kuskilizwa Wzanzibar na wao wana mamuzi gani hivi sasa kuhusu hatma ya nchi yao ndani ya Muungano?.
  Katiba haina mabungufu mengi tu kama Chadema wasemavyo, mimi nasema kwa Zanzibar haifai kabisa Chadema wao wanadai kubadilishwa vipengele vya katiba lakini nchi yao iko na nguvu zake Tanganyika ijitayo Tanzania?.
  Chadema wasisahau kuwa katiba imeinyima Zanzibar nguvu za kujadili maslahi ya nchi mbili zilizo ungana sawa sawa kwa kunda Muungano wan chi mbili .
  Kama ingefuata usawa katiba basi mchakato wote wa katiba ungekuwa ni nchi mbili zenye mamlaka kukaa kitako na kujadili mambo ya Muungano sio leo kuambiwa Rais wa Muungano ndio mwenye mamlaya yote na atamshauri tu Raisi wa Zanzibar huku mchakato wa katiba ukisimamiwa na Spika Mtanganyika,Waziri wa katiba Mtanganyika hii yote ni zarau na sio haki na Wzanzibar hatuka tayari kukokotwa na Rahisi wetu Dr Shinuna.
   
 2. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #2
  Nov 22, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Muungano wa Zanzibar na wapi?
  Zanzibar is a sovereign state, where is Tanganyika?
   
 3. J

  JokaKuu Platinum Member

  #3
  Nov 22, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,769
  Likes Received: 4,982
  Trophy Points: 280
  Kakke,

  ..unamuona Mwanasheria Mkuu wa ZNZ hapo ktk picha alivyofurahia kupitishwa kwa mswada?

  ..wa-Zenj mkifika huku Tanganyika mnajisahau kabisa.

  ..sikiliza mchango wa Hamad Rashidi ambaye alitumia muda mwingi kudhihaki elimu ya Tundu Lissu, badala ya kutetea maslahi ya Wazanzibari.

  ..hata CUF hawana mpango na haya madai yenu ya kuvunja muungano. mapendekezo ya CUF ni serikali 3, wakati zile za Tanganyika na Zanzibar zikiongozwa na magavana.

  ..sasa sijui mipaka ya kiutawala na kiutendaji ya hao magavana ikoje, lakini nina wasiwasi kwamba watakuwa na madaraka madogo sana kulinganisha na Raisi wa serikali ya Mapinduzi ya ZNZ aliyepo sasa hivi.
   
Loading...