MUUNDO wa Tume ya Kuratibu Kuandikwa kwa Katiba Mpya Uweje?

Tatizo ni kwamba tunatumia mwongozo wa katiba hii ambayo hatuitaki ili kuweza kupata katiba mpya.Katiba iliyopo haina maslahi kwa wananchi na kuitegemea kuwa itatuwezesha kufanya mchakato huru ni kosa.Na ndio maana kuna malalamiko kuwa Rais ndiyo mwenye uamuzi wa mwanzo na mwisho.
Chombo kitakachosiamamia mchakato kiwe huru kabisa,na mchakato wa maoni uwashirikishe wadau wote wa jamii kama alivyoainisha mwana JF mmoja hapo juu,na ndio maana wengine hatukuwalaumu wale viongozi wa dini walipotoa maoni yao.
 
Zipo njia nyingine, ni kwamba hujazifikiria tu.



mzee wengine tulishiriki huo mchakato uliosema 80 percent... haukuwa as transparent and participatory kama watu wengine wanavyodhania. Na ndio mchakato ambao unataka kurudiwa tena kwenye hili.
Unaweza kutaja njia nyingine?
Nilikuwapo pia,thats just a flimsy excuse because people were encouraged to vote for multiparty system and they didn't,nilkuwa jeshini na nilihudhuria sana makongamano buhemba!....I remember everything!
 
Mimi nashangaa sana kuona katiba inakuwa kama mali ya Rais na CCM, miongoni mwa mambo wanayotaka wananchi ni kumpunguzia rais madaraka sasa jambo la kushanga muswada uanasema uraisi usijadiliwe hii si haki, nadhani tutapata katiba mpya baada ya JK kutoka madarakani Soon, wananchi walianza kuwa na imani kidogo an rais baada kukubali kuandika katiba mpya laikini sasa anarudi kule ambako alikotoka.

Itafika mahali raisi akifutubia hadharani watu watapiga makofi hadi anyamaze sasa sijui itakuwaje.
 
Tume ya kuandika katiba mpya ni lazima itokane na wananchi. Ila ili kuipa nguvu za kisheria inapaswa muswada wa kuunda tume upitishwe na bunge na kusainiwa na raisi. Muswada huu usiandaliwe na serikali kama ilivyozoeleka bali serikali iwe ni mediator tu kuandaa muswada kwa kutumia maoni yote yaliyokwisha tolewa na wadau mbalimbali na mimi kwa kuongezea ni kwamba muswada huo uwe na structure ifuatayo

1. Uweke wazi kuwa kila chama cha siasa chenye mbunge katika bunge la jamhuri ya muungano basi kinakuwa na nafasi mbili za ujumbe katika tume hiyo bila kujali ina idadi ya wabunge kilicho nao.
2. Dini zote zinazojulikana kuandikishwa Tanzania yaani waislam, wakristo, wahindu, etc kila moja itakuwa na nafasi mbili katika tume hii.
3. Umoja wa asasi za kiraia (e.g TANGO) unakuwa na nafasi mbili
4. Jumuiya ya wakufunzi wa taasisi za elimu ya juu za serikali zinakuwa na nafasi mbili
5. Jumuiya ya wakufunzi wa taasisi za elimu ya juu za binafsi zitoe nafasi mbili
6. Jumuiya ya wakufunzi wa Elimu ya sekondari na msingi wanakuwa na nafasi mbili
7. Jumuiya ya watu wenye ulemavu inakuwa na nafasi mbili
8. Jumuiya ya wazee inakuwa na nafasi mbili
9. Jumuiya ya vijana wa vyuo vikuu Tanzania inakuwa na nafasi mbili
10. Serikali ya Jamhuri ya muungano inakuwa na nafasi mbili
11. Serikali ya mapinduzi Zanzibar inakuwa na nafasi mbili
12. Jumuiya ya wakulima inakuwa na nafasi mbili
13. Jumuiya ya wafanyakazi inakuwa na nafasi mbili
14. Jumuiya ya wafanyabiashara wanakuwa na nafasi mbili
15. Jumuiya ya waganga wa jadi wanakuwa na nafasi mbili(Kina Ambilike nao wana wafuasi wao)

Kazi za hii tume na nguvu za kila mjumbe katika tume hii iwekwe wazi kabisa, na pia itengewe fungu la kukamilisha kazi hiyo na muda wa kuifanya , baadhi yake iwe ni

1. Kumchagua mwenyekiti, makamu mwenyekiti na katibu wa tume miongoni mwao ambao kazi zao hazitakuwa beyond organising public hearings na kukusanya maoni ambapo baada ya kila mkutano kila mjumbe anapewa kopi yake na kazi ya katibu ni kuwa na maoni yote kwa muda wowote na wakati wowote electronic and hard copies, I mean kwenye video, typed in texts na muhtasari kwenye hard copy.

2. Tume hii itatakiwa kuajiri wataalam wote muhimu wa kufanya kazi za kitaalam kama kurekodi kuburn na kuzipa serial numbers public hearing zote, pia wataalam upande wa sheria, fedha etc na kila kitu muhimu kama taasisi inayojitegemea kisayansi.

3. Kuyaunganisha mawazo ya wananchi wote(raw data) na kuyafanyia tathmini ili kuondoa yanayopingana na mikataba ya kimaifa kama Human rights etc kwa unanimous consent among members kisha kuchapisha rasimu yake kama katiba na kuirudisha tena kwa wananchi kuijadili kwa totality na kuongeza ama kufanyia marekebisho baadhi. Na baada ya hapo inapigiwa kura na wajumbe wa tume hiyo kwa kigezo kuwa kilichomo ndani ya rasimu ni maoni solely ya wananchi na hakuna kipengele chochote kilichopachikwa either na wanatume au nje. Ili Rasimu ipite ni lazima wajumbe wote waikubali si kwa kuwa yaliyomo yamewafurahisha la bali kwa kuonesha kuwa kumbukumbu zao za maoni ya wananchi na kilichomo havitofautiani.
4. Wajumbe wa tume hii watakuwa ni observers na mashuhuda wa yale yaliyotokana na wananchi kwa wao kuwa na record ya copy zote zenye alama maalum ya kuonesha kuwa ni genuine kama vile electronic and non electronic securities. Hawataruhusiwa kuchangia wala kuongeza chochote bali wanaweza fanya hivyo kwa kutumia makundi yaliyo katika jumuiya wanazotoka.
5. Wajumbe wote watakuwa na haki ya KU-VETO kitu chochote wanachoona kimewekwa na hakipo katika record zao za public hearing, Unanimous agreement inakuwa ni central focus na inabase kutokana na mawazo yaliyokusanywa tu si kimtazamo wao.
6. Baada ya hapo rasimu hiyo inaanza kunadiwa kwa wananchi kwa ajili ya kuipitishwa kwa referendum na tume ya kusimamia referendum hiyo inachaguliwa na kuundwa na Tume hiyo kwa wajumbe wote kuwakubali watendaji wa tume kwa sauti moja.
7. Mjumbe yeyote akiona mtu aliye ajiriwa anafanya kazi kinyume na maelekezo unanimous ya tume basi anapeleka ushahidi huo mbele ya tume na ikithibitika hivyo mwajiriwa huyo anakuwa amepoteza sifa ya kuwa mwajiriwa na kazi alizokuwa amefanya zinakuwa ni Void na kulazimishwa kurudisha 50% ya mshahara
8 Tume hii haitawajibika tena kwa rais au bunge. Itakuwa ni tume huru kabisa.

9. Tume hii itaanda referendum kwa kuchagua wafanyakazi wake wa kuandikisha wapiga kura na kusimamia uchaguzi baada ya unanimous agreement kwa mwajiliwa yeyote yule na tume itakuwa na nguvu za kuamua kumfuta mtu yeyote kama ilivyotajwa hapo juu. Tume ambayo members wake hawatakuwa na haki ya kushiriki referendum hiyo itakuwa imekamilisha kazi yake baada ya 60% yawananchi wapiga kura wote walioandikishwa na tume hii, tarehe ya referendum iwe June 2013 ili kutoa nafasi kwa vyama na serikali kujiandaa na uchaguzi wa 2015 kwa kutumia katiba mpya.
Note: Mchakato wa kupata wawakilishi wa makundi haya ndani ya jumuiya hizi utasimamiwa na jumuiya zenyewe na kupeleka majina ya wawakilishi wao kwenye ofisi ya bunge na kupewa Air time na TBC na vyombo vya habari kueleza kwa muda wa dakika 15 jinsi walipata wawakilishi hao, na ikipita masaa 24 hakuna mtu wa kupinga kutoka kwenye jumuiyao anakuwa amethibitishwa. Na ikitokea mtu akampinga na baadae ikadhirika kuwa hana uhusiano wala uhalali wa kuwa mwanajumuiya hiyo anakuwa amejitangazia kifungo ya miaka mitatu na fine ya Tzs 5 million, au fine ya Tshs 30million. Mchakato wote wa kuwapata wawakilishi hawa ukiacha wale wa serikali ya jamhuri na zanzibar ni lazima uwe filmed na kuwasilishwa kwenye ofisi ya bunge na mtu yeyote atakayetaka kuuona basi awe na haki kisheria kuupa kwa kununua video yake toka kwenye jumuiya husika kwa pesa isiyozidi TZS 5,000 tu.
 
Ninakubaliana na aliyesema kuwa wananchi wote kwa wakati mmoja hatuwezi kuunda tume na kuratibu shughuli zote. Ni lazima kiwepo chombo kitakachoweza kutoa muongozo kwa vyombo vingine vya kiutendaji. kwa mfano mkutano wa kitaifa ndio utakaokuwa na uwakilishi wa makundi jamii ya taifa. Kwa kupitia mkutano huu kunaweza kupatikana tume ya kuratibu utaratibu kwanza, kuandaa hadidu za rejea na kuunda tume ya kukusanya maoni n.k.

Nilimsikiliza Profesa Shivji akiwa Zanzibar katika mjadala wa ni vipi katiba mpya inaandikwa, nadhani kuna mengi sana ya kujifunza kwa aliyosema ambayo yanaweza kujibu baadhi ya hoja akiwa mtaalam aliyebobea.
Clip hiyo iliwekwa hapa JF na Ghibuu nadhani, kutoka Mzalendo.net. Kama kuna anayeweza kuirudisha tafadhali.
 
Nimependa mawazo ya watu wengi sana na nitajaribu kuyaweka yote pamoja inshallah muda si mrefu: Lakini kuna uwezekano wa kuwa na vitu kama hivi:

Chombo Kikuu:
Baraza La Taifa la Kutunga Katiba - National Constitutional Assembly (wajumbe wake nitafafanua)

Chini yake:

KUSIMAMIA MCHAKATO WA MJADALA NA MAONI
Kamati ya Rais ya Katiba Mpya
- (ni Kamati ya Rais kwa sababu anamteua Mwenyekiti wake tu; wajumbe wengine nitaelezea)
Secretariati ya Baraza la Katiba (ya Kudumu)

KUELEKEA KUANDIKA KATIBA MPYA
Jopo la Watalaam (Wataalamu wakaokataa chini kuandika Katiba (draft) na Final Draft.
Tume ya Muda ya Uchaguzi (Itasimamia chaguzi zote ndogo, Kura za Maoni kuanzia 2012-2015)


Kwa wakati huu nafikiria kitu kama hicho.. (vyombo) nadhani nikitulia weekend hii nitajaribu kuweka mfumo wa utendaji wa vyombo hivi kisheria na mahusiano yake na madaraka ya wananchi kuandika katiba yao. So.. bado nakaribisha maoni..
 
Iundwe tume huru ambayo jukumu lake ni kusimamia mchakato wa kuandika katiba mpya,iteuliwe na bunge kwa kupigiwa kura kuzingatia na sifa na vigezo vitakavyoonekana vinafaa...tume hii isimamiwe na Bunge!...Wakamilishe jukumu hili kwa kupitia kwa wananchi katika kada zote na kuchukua maoni na kero zao mbali mbali kabla hawajakaa na wanasheria na wanazuoni mbali mbali na kuweka sawa hili na lile kabla hawajaipeleka Bungeni na Bunge kuisoma wazi na baada ya kujiridhisha idurufiwe na kuanza kutumika!

Umhimu wa kushilikishwa Bunge sina matatizo nao. Tatizo langu na Bunge kuteuwa wajumbe wa Tume. Kiutekelezaji ni vigumu sana. Wataanzia wapi katika kuteuwa? Je wananchi waombe nafasi za ujumbe alafu wapigiwe kura? Mimi kwa maoni yangu Raisi angependekeza majina na hatimaye kuyapeleka Bungeni kwaajili ya kupitishwa.
 
kwa kuwa wabunge hawawakilishi wapiga kura wao kama inavyotamkwa, bali wanawakilisha vyama vyao vya siasa na bunge, naamini tukiangalia namna ya kuwashirikisha waalimu kwa njia bora kabisa itatupa tija tunayoitarajia, walazimike kujadiliana na wananchi kwenye maeneo yao ili kuwakilisha maoni na msimamo wa wananchi tofauti na wabunge wafanyavyo, wanachaguliwa na wananchi wanatumikia vyama vya siasa. bunge la katiba litokane asilimia 50 na wasomi wa kada ya sheria, 15% wastaafu ambao hawakuwa na vyeo vya juu serikalini, 2% watoke jela, 8% watokee kwa wataalamu, 10% vyama vya siasa, 10% dini 5% makundi maalum kwenye jamii i.e. wenye ulemavu, wanawake, wanaharakati, n.k. jinsi ya kuwapata tujadili kwa pamoja. naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom