Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,462
- 39,928
Wengi tumetatizika na mapendekezo ya Muungo wa Tume ya Rais ya Kupitia Katiba kama inavyopendekezwa na Muswada wa Sheria ya Mapitio ya Katiba. Tuna tatizo jinsi Tume hiyo inavyoundwa, nguvu zake, majukumu yake n.k Baada ya kusoma zile kanuni za msingi za Kuelekea Katiba Mpya yawezekana kila mmoja wetu ana mawazo kuwa tunataka Katiba ambayo kweli itatokana na wananchi na siyo ya kuburuzwa na chama tawala au na serikali.
Binafsi ninayo mapendekezo yangu ya mchakato na muundo na nimefikia mbali kidogo lakini nami ninapata tatizo ambalo wengi tutakutana nalo. Tukizingatia kanuni zile tano za kuelekea Katiba Mpya:
a. Nani asimamie mchakato wa kuandika Katiba Mpya
b. Ateuliwa na nani
c. Asimamiwe na nani
d. Akamilishe vipi jukumu hilo
Kwa hiyo naomba mawazo yatanisaidia na mimi kurefine mawazo yangu kuhusu muundo ili niweze kuwashirikisha nanyi. Je Katiba Mpya tunayotaka mchakato wake uweje kulinganisha na ule uliopendekezwa na serikali? Mchakato ambao utaonesha kuwa wananchi ndio wanaoandika Katiba yao hasa na siyo kikundi cha watu wachache wateuliwa?