Malilambwiga
JF-Expert Member
- Jul 19, 2015
- 485
- 296
Kwa kipindi kirefu sasa mabadiliko ya wizara za serikali na muundo wa taasisi zilizoko chini yake umekuwa na mgongano unaopelekea kukwama kwa utekelezaji wa majukumu ya serikali.
1. Mfano EWURA ambayo kimfumo iko chini ya wizara nyingine lakini kiutendaji inafanya kazi zikiwemo za wizara ya maji, wizara ya nishati na madini na pia wizara ya mawasiliano na uchukuzi.
Kwa hali kama hii hakuna waziri mwenye dhamana ya kuiwajibisha moja kwa moja EWURA pale itakapokosea hadi waziri mwenye dhamana na EWURA.
2. Mfano mwingine ni taasisi ya wakala wa vipimo ambayo ipo chini ya wizara ya viwanda lakini shughuli zake nyingine zinaingiliana na Wizara ya Uchukuzi kama ilivyogundulika ktk ziara ya ghafla ya waziri mkuu bandarini dhidi ya upotevu wa mafuta ambao kimfumo uko chini ya Nishati na madini.
3. Mfano mwingine ni ajira ya walimu serikalini. Wapo wanaomilikiwa na serikali kuu na pia wapo walioko chini ya TAMISEMI kwa maana ya Halmashauri, Manispaa na Majiji.
Katika hali kama hii inapelekea mgongano wa utendaji serikalini usio wa lazima na wakati mwingine wizara au taasisi fulani kuona majukumu yake yanaingiliwa na mamlaka nyingine.
Ni vyema ukaandaliwa mpango na wataalamu chini ya upembuzi yakinifu ili kila idara, kitengo au taasisi fulani ya serikali kuwa chini ya wizara inayohusika na utendaji wake wa kila siku.