Mjuni Lwambo
JF-Expert Member
- Apr 25, 2012
- 9,415
- 8,873
Mwa j nitumie picha yakoNO TO SERIKALI TATU!!
Hatutaki serikali tatu! wala mbili! = moja
Mwa j nitumie picha yakoNO TO SERIKALI TATU!!
Hatutaki serikali tatu! wala mbili! = moja
huo ndo maana ya muungano..tatizo la wenzetu tumeshawapatia/wamejipa vielelezo vingi vya kujitambua kama taifa huru..ni kiasi cha wao kujitangaza kama nchi tu basi.. Hapo ndio ugumu wa kuwaambia tuunde serikali moja unapokuja kwani wameshaonja tamu ya madaraka mjj
Jumaane,
Mimi naona kwa sasa hivi Zanzibar ndiyo inayo colonize Tanganyika kwa sababu yenyewe inajitawala na bado inashare kwenye Muungano. Unasema Tanganyika can't force Muungano wanaoutaka wao na Zanzibar, Je huoni kwa kusema hivyo unataka Zanzibar ndiyo i force Muungano wanaoutaka wao na Tanganyika? Marekani ni muunganiko wa nchi zaidi 40 ambazo zilikuwa na mchanganyiko wa nchi ndogo na kubwa. Maskini na Tajiri lakini wameunda serikali moja. Kwa nini Serikali moja iwe nongwa kwa Tanganyika na Zanzibar? Je nini mantiki ya Muungano kama bado kila muungana ana serikali yake?
Hoja ya Serikali tatu ni hoja ya wanasiasa kujitengenezea nafasi za ulaji.
Nakala: Mzee Mwanakijiji.
TUMBIRI (PhD, University of HULL, United Kingdom),
tumbiri@jamiiforums.com
Mumo wowote tunaoutaka lazima ukubalike kwa watu wa pande zote mbili kwa ridhaa zao - Wanzibari kwa upande wao na Watanganyika kwa umoja wao - Ndipo muungano utakuwa muungano. Sasa tulipofika: Muungano wa serikali mbili haukubaliki - haufai una kero luluki. Watanganyika hawataki serikali tatu - ni gharama kuziendesha. Wazanzibar hawataki serikali moja- hawataki kutawaliwa na kuwa mkoa wa tanganyika. Tufanyeje sasa? Ng'ombe avute gari au gari ivute ng'ombe?
Tusikubali kwenda serikali tatu. Kwa vile tumekatazwa kutaka kuvunja Muungano - japo waliotukataza hawana uwezo huo - na kwamba tunaweza kujadili "muundo" bora wa Muungano. Ninawasihi watu wa bara kudai "Serikali moja, taifa moja, na nchi moja". Haya mambo ya serikali mbili nchi mbili au serikali tatu nchi mbili hayaingii kichwani na ni jitihada za kujaribu kuibeba Zanzibar. Wakati umefika tudai uwepo wa serikali moja tu ya kitafa kwenye nchi moja.
Ninafahamu kabisa matokeo ya watu wa bara kutaka hili. Jambo pekee ambalo tusikubali kuuziwa (CCM na upiinzani wanataka hili) ni serikali tatu. Serikali tatu ni mzigo ambao hatuwezi kuubeba na wala hatupaswi kuubeba. Nawasihi wenzangu tukate kuongezewa mizigo. Tuwe na serikali moja, taifa moja na nchi moja. Sasa kama hili lina maana Zanzibar iwe "serikali moja, taifa moja na nchi moja" na bara iwe "serikali moja, taifa moja na nchi moja" basi na iwe.
Tuwasaidie Zanzibar watoke kwenye Muungano kama hawataki serikali moja kwani mbili hawataki na tatu tutajipa mzigo zaidi!
SAY NO TO SERIKALI TATU!!
Iambie tume ya Warioba - hatutaki serikali tatu!!
Nonda,
kuna kitu kimoja Wzn wameshindwa kukielewa. Wanadai mamlaka kamili 100%. Wakati huo huo wanadai kuwe na serikali 3 au mkataba. Kuwepo kwa vitu hivyo tayari kutaondoa asilimia 100 na kuirudisha chini. Zanzibar watakubali hilo? Kama hawakubali, mamlaka kamili wanayodai ni yapi yatakayowaacha na uhuru wa mamlaka kamili 100%
Ukishasema mamlaka kamili hapo tayari umeshaondoa uwezekano wa mkataba au serikali 3. Labda unieleweshe utakuwaje na mamlaka kamili halafu ukawa na mkataba au serikali 3?
Pili, kuna kitu kinaitwa serikali 3, nauliza kila siku na huwa ndio mwisho wa mjadala hasa kwa WZNZ. Serikali ya tatu ya muungano itashughulikia nini ili ihakikishe kuwa ZNZ inabaki na mamlaka kamili 100%. Na hiyo ya tatu inaendeshwaje kwa gharama ikiwa ZNZ yenye mamlaka kamili 100% ni mbia sawa na Tanganyika itakayokuwa na mamlaka kamili?
Tatu, katika mkataba unaongelewa kuna siri gani ya mkataba ambayo WZNZ hawataki kuiweka wazi? Nina maana mkataba ushughulikie mambo gani yenye faida kwa pande zote zikiwa wabia sawa?
Nne, kitu gani kinachowazuia kusema mnataka kuvunja muungano? Kwanini mnakimbilia serikali 3 au mkataba na si kuvunja bughudha hii ya muungano inayowanasabisha na wabantu ili hali ninyi ni waarabu? Kwanini msitamke LET Tanganyika GO! kama sisi tulivyo na uthubutu wa kusema LET ZNZ GO!
Nomba safari hii usikimbie, uwe na uthubutu wa kujibu. Ukikimbia utakuwa umepoteza uhalali wa kulizungumzia hili jambo kwasababu utakuwa sawa na yule kijana wa mtaani anayeimba mayenu na bolingo ambaye ukimuuliza maana yake hajui, lakini anaimba vema sana.
Nonda,
kuna kitu kimoja Wzn wameshindwa kukielewa. .
Tusikubali kwenda serikali tatu. Kwa vile tumekatazwa kutaka kuvunja Muungano - japo waliotukataza hawana uwezo huo - na kwamba tunaweza kujadili "muundo" bora wa Muungano. Ninawasihi watu wa bara kudai "Serikali moja, taifa moja, na nchi moja". Haya mambo ya serikali mbili nchi mbili au serikali tatu nchi mbili hayaingii kichwani na ni jitihada za kujaribu kuibeba Zanzibar. Wakati umefika tudai uwepo wa serikali moja tu ya kitafa kwenye nchi moja.
Ninafahamu kabisa matokeo ya watu wa bara kutaka hili. Jambo pekee ambalo tusikubali kuuziwa (CCM na upiinzani wanataka hili) ni serikali tatu. Serikali tatu ni mzigo ambao hatuwezi kuubeba na wala hatupaswi kuubeba. Nawasihi wenzangu tukate kuongezewa mizigo. Tuwe na serikali moja, taifa moja na nchi moja. Sasa kama hili lina maana Zanzibar iwe "serikali moja, taifa moja na nchi moja" na bara iwe "serikali moja, taifa moja na nchi moja" basi na iwe.
Tuwasaidie Zanzibar watoke kwenye Muungano kama hawataki serikali moja kwani mbili hawataki na tatu tutajipa mzigo zaidi!
SAY NO TO SERIKALI TATU!!
Iambie tume ya Warioba - hatutaki serikali tatu!!
Nonda, ninachosema ni kuhusu mawazo ya Wazanzibar.Nini mawazo yako juu ya #post 88?
Nonda, ninachosema ni kuhusu mawazo ya Wazanzibar.
Joseph Mihangwa anaandika kama mwandishi tu na wala hawakilishi mawazo ya WZN.
Kwa mfano wewe uwe ndio Rais wetu..
Kama hamna cha kuzungumza Siasa bora munyamaze kimya tu itakuwa ni jambo bora kunyamaza kuliko kuropoka ovyo tu pasipo kuwa na point Nguruvi3