Muundo wa Muungano: Tanganyika tunataka 'Serikali moja, nchi moja, taifa moja'!

Tusikubali kwenda serikali tatu. Kwa vile tumekatazwa kutaka kuvunja Muungano - japo waliotukataza hawana uwezo huo - na kwamba tunaweza kujadili "muundo" bora wa Muungano. Ninawasihi watu wa bara kudai "Serikali moja, taifa moja, na nchi moja". Haya mambo ya serikali mbili nchi mbili au serikali tatu nchi mbili hayaingii kichwani na ni jitihada za kujaribu kuibeba Zanzibar. Wakati umefika tudai uwepo wa serikali moja tu ya kitafa kwenye nchi moja.

Ninafahamu kabisa matokeo ya watu wa bara kutaka hili. Jambo pekee ambalo tusikubali kuuziwa (CCM na upiinzani wanataka hili) ni serikali tatu. Serikali tatu ni mzigo ambao hatuwezi kuubeba na wala hatupaswi kuubeba. Nawasihi wenzangu tukate kuongezewa mizigo. Tuwe na serikali moja, taifa moja na nchi moja. Sasa kama hili lina maana Zanzibar iwe "serikali moja, taifa moja na nchi moja" na bara iwe "serikali moja, taifa moja na nchi moja" basi na iwe.

Tuwasaidie Zanzibar watoke kwenye Muungano kama hawataki serikali moja kwani mbili hawataki na tatu tutajipa mzigo zaidi!

SAY NO TO SERIKALI TATU!!

Iambie tume ya Warioba - hatutaki serikali tatu!!

KWanini serikali moja wakati 2015 mnacukua nchi? Mie na uhakika wa kwamba CHADEMA wakichukua nchi muungano hatutadumu hata miaka 2. Wasiotaka serikali mbili waipigie kura chadema.
 
Mtanzania1

Kinachoonekana hapa ni kwamba mwanakijiji anacampaign na kuadvocate for compete colonization of Zanzibar by Tanganyika. Anajifanya kasahau/haelewi kuwa Muungano huu ni makubaliano baina ya nchi mbili kwa hayo mambo ya muungano na mabadiliko ya muundo wa muungano lazima yapate ridhaa ya zanzibar kama mdau wa muungano.

Tanganyika can not forcefully impose muungano wanaoutaka wao kwa zanzibar. Huo ni ukoloni, na wala zanzibar haikumpindua mkoloni na sultani wa kiarabu ili itawaliwe na mkoloni mweusi mtanganyika. kwa hilo sahauni, sio leo tena.
 
Last edited by a moderator:
Mwanakijiji uko sawa maana malalamiko hayatamalizwa na serikali tatu. Tukianza kipata pesa za mafuta na Gas watataka asilimia fulani lakini wakipata mafuta na Gas watasema haiko kwenye muungano wakati gharama za umeme, shule, hospitali, jeshi, polisi na ujenzi zipo kwenye muungano. Wanataka tugawane sawa ubalozi n.k.

Sasa mimi naona imefikia wakati wa serikali moja maana hata viongozi wengi wa Zanzibar hawaishi Zanzibar na ni vigumu kujua mtu katokea wapi siku hizi.

Serikali iwe mmoja na kama wanataka wawe na serikali yao basi sawa lakini Tanzania haitakuwa na usalama kwenye serikali tatu itakuwa kama sasa hivi tu tofauti itakuwa gharama zaidi. Sasa tuna wabunge wa bara, wa zanzibar na wawakilishi. Makamu wa rais watatu, rais wawili, jaji wakuu n.k.

Kama tunafikiria tutawafurahisha Zanzibar kwa serikali tatu tunajidanganya.
 
Endelea kuota mchana Mzee!km unataka hoja ya ipate nguvu ungemuomba Mzee wa Upako akamfufua Baba yako wa Taifa akusaidie kupigia debe serikali moja!
Hamna ujanja mtaimbo umeganda!
 
Serikali moja, na ni sisi watanganyika ndiyo tunavyotaka. Kama wazanzibari hawataki serikali moja, basi waishie hukohuko. Sijui kwa nini hii mizee yetu inawabembeleza hawa wazanzibari, wana nini? Get'em out of our way, wanatujazia miinzi tu na misamaki yao.
 
Hakuna serikali 3, hakuna mkataba, hakuna mahusiano.

BLW, hakuna hata mmoja anayesema vunja muungano, wao wanasema ondoA mafuta katika masuala ya muungano.
Hawasemi ondoa elimu ya juu, ondoa mishahara!

Inajulikana sasa kuwa ZNZ wameJitoa SUMATRA lakini bili ya SUMATRA kule IMO(Intern maritime org) inalipwa na Tanganyika kama walivyo na ZESCO lakini bili ya umeme inalipwa na Mtanganyika

Serikali 3 ni kuendelea kubeba zigo la misumari, sisi tunasema waende wao wamegomea serikali 3 why?

Kwa vile hawawezi kusema Dodoma bungeni au ZNZ ndani ya BLW kwa Woga lakini wepesi wa kubeba viberiti sasa tuwasaidie.

SERIKALI MOJA! AU LET ZNZ GO ASAP!
 
Nchi moja, serikali moja, taifa moja = Tanganyika ili liungane na Unguja na pemba kwenye serikali ya shirikisho la Afrika Mashariki na kati.
 
Mimi sitaki Tanganyika iungane na Zanzibar. Hao watu wameshanichosha nami nimeshawachoka.

Waende zao huko na kanchi kao na sisi tubaki na nchi yetu.

Sitaki muungano wa aina yoyote ile na Zanzibar. Nimesema sitaki.
 
Tusikubali kwenda serikali tatu. Kwa vile tumekatazwa kutaka kuvunja Muungano - japo waliotukataza hawana uwezo huo - na kwamba tunaweza kujadili "muundo" bora wa Muungano. Ninawasihi watu wa bara kudai "Serikali moja, taifa moja, na nchi moja". Haya mambo ya serikali mbili nchi mbili au serikali tatu nchi mbili hayaingii kichwani na ni jitihada za kujaribu kuibeba Zanzibar. Wakati umefika tudai uwepo wa serikali moja tu ya kitaifa kwenye nchi moja.

Ninafahamu kabisa matokeo ya watu wa bara kutaka hili. Jambo pekee ambalo tusikubali kuuziwa (CCM na upiinzani wanataka hili) ni serikali tatu. Serikali tatu ni mzigo ambao hatuwezi kuubeba na wala hatupaswi kuubeba. Nawasihi wenzangu ...... Tuwe na serikali moja, taifa moja na nchi moja. Sasa kama hili lina maana Zanzibar iwe "serikali moja, taifa moja na nchi moja" na bara iwe "serikali moja, taifa moja na nchi moja" basi na iwe.

Tuwasaidie Zanzibar watoke kwenye Muungano kama hawataki serikali moja kwani mbili hawataki na tatu tutajipa mzigo zaidi!

Iambie tume ya Warioba - hatutaki serikali tatu!!

Mwanakijiji,

..mimi nataka serikali moja, serikali ya Tanganyika.
Sisi sio wa bara; ni WATANGANYIKA!

Yeah, hata Lukuvi alitamka hivyo bungeni. I prefer a single country, single govt

Hatutaki serikali Tanganyika ni mzigo kwa Tanganyika.

Serikali moja, na ni sisi watanganyika ndiyo tunavyotaka.

Mzee Mwanakijiji

Unatushauri watanzania(wabara aka watanganyika) sote tujiunge na CCM?

Sera ya CCM kutoka serikali mbili kuelekea moja imebadilika lini?
Lini CCM walibadilisha hii kutoka mbili kuelekea moja? Umesema CCM wanataka serikali tatu?

Hata hivyo wazo lako ni zuri tu, sasa uwashawishi CHADEMA na wanaCHADEMA waunge mkono wazo lako.
CHADEMA wana sera ya serikali tatu.Halafu pia uwashawishi CUF na wanachama wake wabadili sera yao ya muungano, serikali tatu.

Lissu ametonesha kidonda bungeni kwa kusema Tanganyika na serikali ya Tanganyika irudi.

Na mwazilishi wa Muungano, Mwalimu alisema ikifufuliwa EAC basi ni vyema Tanzania iwe na serikali mbili, ya Tanganyika na ya Zanzibar. Bofya hapa lissu

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar(Tanzania) kwa miaka 48 umekosa kuvutia nchi nyengine kujiunga nasi,zimekuwepo kelele na mayowe ya wazanzibari kutaka waachiwe wapumue kwa miongo kadhaa sasa. Kweli mkuu unategemea kupata serikali moja, nchi moja na Taifa moja?

Kwa maneno mengine, unasema kuwa tuimeze Zanzibar? Au ndio kampeni ya "Tuwasaidie Zanzibar watoke kwenye muungano"?

Unasema,
Hatutaki serikali Tanganyika ni mzigo kwa Tanganyika.
Tukishawasaidia Zanzibar kutoka katika Muungano, tutabaki na serikali ipi?

Serikali ya Tanganyika huitaki, je unaitaka Tanganyika? Unataka Tanganyika isiyo na serikali?

Ni imani yangu kuwa wengi tutamuunga mkono Lissu katika kupeleka hoja ya kufufuliwa kwa Tanganyika na serikali yake, ili tukutane na Zanzibar huko EAC na kwenye shirikisho la EAC(muungano wa nchi nyingi).Huu wetu ambao umeshindwa kutatua kero za muungano na kuvutia wanachama wepya uachwe ufe bila kuleta vifo vya ziada na vilema wa ziada, na mihanga mengine katika kuulinda/ kulazimisha uwepo.
 
Hakuna haja ya kubadilisha jina la nchi ni kuongeza gharama na usumbufu wa bure. Kama Zanzibar wanataka kujitoa wajitoe lakini hakuna serikali tatu ni upuuzi
 
Ni wazi bora serikali moja kuliko hizi mbili za sasa, na zaidi hakuna mtu makini anayeona practicality ya serikali tatu. Tatizo la serikali moja ni kuwa waZnz wanaogopa kumezwa moja kwa moja na Bara. Na hofu yao hiyo mi naikubali kihistoria ni kweli nchi yao ilikuwepo na ni ndogo kulinganisha na Bara, hivi sasa kuna watu wengi zaidi wilaya ya Kinondoni kuliko Znz yote! Sasa suala la muungano lipo kwa waznz wenyewe kuamua.

Pamoja na kelele za uamsho za kutaka Jamhuri ya Znz irudi, ukweli ni kuwa bado kuna watu wengi Znz wanataka muungano, na zaidi wapemba hawataki uvunjike kwa kuwa wanaogopa waunguja watawameza na wao (wapemba) wamewekeza na kushahabiana sana na watu wa Bara kuliko waunguja.

Tusubiri tuone walete hio kura ya maoni utaona watu wa visiwani watakataa kuuvunja muungano ila mabadiliko ya hapa na pale yatafanyika kwa muundo huu huu wa sasa, yaani serikali mbili.

Mwisho wa yote ni matokeo mawili tu kwa maoni yangu ama muungano utavunjika au utabaki kwa mfumo wa serikali mbili kama sasa yumkini na mabadiliko ya hapa na pale. Serikali moja au serikali tatu hizo zote mbili haziwezekani maana Bara (Tanganyika) ni kubwa mno kulinganisha na Znz.

Mi binafsi napenda muungano uwepo na ushamiri maana Watgnk na waznz ni ndugu wa damu na historia yetu ni moja, na siku zote muungano ni nguvu na utengano ni udhaifu, uchumi wetu ni mdogo sana kuanza kuvurugana bila mpango. Ni vyema tuangalia mbele kwa kushirikiana zaidi katika EAC kuimarisha uchumi wa eneo letu kuliko hii ya kuanza kuangalia jinsi ya kutengana.
 
sioni mantikia ya hoja hii. Wabara karibu watapigana vita vya wenyewe kwa wenyewe. Washaanza chadema vs ccm.zanzibar hali shwari tusitake kuwaingiza zanzibar matatizo
Nineshangaa kama hata wewe ungaliweza kuona mantiki ya hoja hii...Kuona kunahitaji macho.....
 
MKJJ nnapenda nikupe angalizo juu ya suali lako la kuwa na serikali moja ya Muungano

wazanzibari wa leo wameamka sana tena sana, wao wanachodai muungano wa haki na wanataka ifahamike wazi kuwa zanzibar ni nchi sawa na nchi nyengine. kwa hio wanapoungana nchi mbili zinaungana zikiwa nchi mbili zenye mamlaka sawa.

kwa maana hio tukiunda serikali moja lazima tusimame kwenye usawa huo, idadi ya mawaziri iwe sawa, watendaji wa serikali hio pia tuwe sawa. kitu ambacho naaamini watanganyika watakimbia na hawatakubali. na kwa vile miaka 50 makao makuu ya serikali yalikuwa tanganyika sasa makao makuu ya serikali yawe zanzibar.

kwa kweli wazanzibari kwa njia moja au nyengine safari hii wamejipanga kuhakikisha haki yao haipotei. na nnakuhakikishia wataouvunja muungano safari hii ni watanganyika na si wazanzibari na utanambia
 
Mawazo yangu:
SURA YA NNE YA KATIBA YA MUUNGANO WA TANZANIA
Badala ya sehemu pekee ya serikali ya mapinduzi ya Zanzibar, ziwepo sehemu mbili yaani serikali ya Zanzibar na serikali ya Tanganyika zitakazokuwa chini ya waziri mkuu ambaye ndiye atakuwa mtendaji mkuu wa shughuli zote za serikali yaani waziri mkuu zanzibar na waziri mkuu tanganyika. Nafasi ya rais iwe katika Jamhuri ya muungano wa Tanzania na makamu wake mmoja.
Kwa maana hiyo basi, mawaziri wakuu wote (ambao lazima wawe wa kuchaguliwa) watakuwa "responsible" kwa pande zao tuna mabaraza yao ya mawaziri yataundwa kwa kushauriana na raisi pamoja na makamu wake wa jamhuri ya muungano wa tanzania.
 
MKJJ nnapenda nikupe angalizo juu ya suali lako la kuwa na serikali moja ya Muungano

wazanzibari wa leo wameamka sana tena sana, wao wanachodai muungano wa haki na wanataka ifahamike wazi kuwa zanzibar ni nchi sawa na nchi nyengine. kwa hio wanapoungana nchi mbili zinaungana zikiwa nchi mbili zenye mamlaka sawa.

kwa maana hio tukiunda serikali moja lazima tusimame kwenye usawa huo, idadi ya mawaziri iwe sawa, watendaji wa serikali hio pia tuwe sawa. kitu ambacho naaamini watanganyika watakimbia na hawatakubali. na kwa vile miaka 50 makao makuu ya serikali yalikuwa tanganyika sasa makao makuu ya serikali yawe zanzibar.

kwa kweli wazanzibari kwa njia moja au nyengine safari hii wamejipanga kuhakikisha haki yao haipotei. na nnakuhakikishia wataouvunja muungano safari hii ni watanganyika na si wazanzibari na utanambia


sawa' ma Wazanzibari hao wanaotaka usawa huo wa fifty fifty wako tayari kuchangia kwenye hiyo serikali nyingine fifty fifty katika kuiendesha. Wakiwa tayari hilo linawezekana.
 
Hakuna anaetaka Muungano ufe ndani ya mikono yake ,ni lazima mulielewe hilo ,kwani ni kuandikwa kwenye historia milele.Ni bora uandikwe kwa kuirudisha Tanganyika na sivinginevyo baadae muungano utakufa wenyewe kama uyoga mwitu.
 
Back
Top Bottom