Muundo huu wa Muungano utatuumiza sisi Wazanzibar!

Kasheshe

JF-Expert Member
Jun 29, 2007
4,694
787
Najua Viongozi wetu wanapenda huu muundo kwa sababu ya Madaraka. Lakini kwa mwananchi wa Kawaida wa Zanzibar huu muundo hauna tija kwetu. Tusubiri tuone.

Kasheshe @ Bububu,
 
Mambo bado hapo hii ni Rasimu tu Mkuu
subiri andiko la Katiba Mpya ndiyo utajua
Lazima Pemba nayo iwe Jamhuri .
 
Najua Viongozi wetu wanapenda huu muundo kwa sababu ya Madaraka. Lakini kwa mwananchi wa Kawaida wa Zanzibar huu muundo hauna tija kwetu. Tusubiri tuone.

Kasheshe @ Bububu,

Yakhe,

Vipi ndo nyie nyie mumerudi tuonekane tushaanza kulalama kama wazanzibar ni bora kua nje ya Tanganyika (Tanzania) kuliko kuwa ndani ya huo muungano munaosema sisi tunataka kutoka lakini wadanganyika sijaona mapingamizi yyte kutoka kwao kwetu haiwezi kupita hiyo
 
ah ah ah, kweli hii ni ngumu kumeza, basi sisi waBARA tmeumizwa kwa kipindi chote cha miaka 49.
tulieni tu sindano itaingia labda mkimbilie omani

Mkuu Kashorobana,

Mumeumizwa wapi wakati kama mnajua mnaumizwa mbona hakuna alodai kutoka hadi muda huu vipi halafu sisi hatukimbilii Oman si raisi juzi juzi katoka huko huko na yule membe sijui mamba ama ndo yalee baniani baya kiatu chake dawa eehh
 
Najua Viongozi wetu wanapenda huu muundo kwa sababu ya Madaraka. Lakini kwa mwananchi wa Kawaida wa Zanzibar huu muundo hauna tija kwetu. Tusubiri tuone.

Kasheshe @ Bububu,

Mkiona vp jichomoe kabla hamjatuharibia watoto wetu kwa mambo yenu ya kileberali.
By the way rasim ya katiba haijaweka wazi mfumo wa urais wa shirikisho, ni kwa zamu au inawezekana rais toka upande mmoja kwa awamu zaidi ya moja.
Hapa bara tutapiga bao hatuwezi kuongozwa na rais toka sehem ndogo ya muungano; mala zote hatavuka 50%
 
Najua Viongozi wetu wanapenda huu muundo kwa sababu ya Madaraka. Lakini kwa mwananchi wa Kawaida wa Zanzibar huu muundo hauna tija kwetu. Tusubiri tuone.

Kasheshe @ Bububu,

Mkuu kwa nini? Sisi wengine tunashangilia kurudishiwa bendera yetu, wimbo wetu wa taifa na jina la Nchi yetu. Ninyi mmekuwa navyo hivyo wakati wengine tulikuwa tunapiga miayo kuvisubiri hivyo vitu.
 
Wazanzibari kwa kulalamika hatuwawezi, si muwaambie viongozi wenu waache ubinafsi wadai zanzibar yenu huru mkuu.
 
Mkuu kwa nini? Sisi wengine tunashangilia kurudishiwa bendera yetu, wimbo wetu wa taifa na jina la Nchi yetu. Ninyi mmekuwa navyo hivyo wakati wengine tulikuwa tunapiga miayo kuvisubiri hivyo vitu.

Bendera na mawimbo ya taifa yanawasaidia wakagua magwaride... sisi Wanzibar wananchi twatake fedha mifukoni jama!
 
JAJI WARIOBA hakutuelewa wazanzibar tunataka mamlaka kamili ya zanzibar nani kamwambia mambo saba ya muungano hiyo akileta huku tutaipiga kibuti .sisi tunajua kusimamia ajenda yetu ya ZANZIBAR KWANZA MAMLAKA KAMILI

''JAMUHURI YA WATU WA ZANZIBAR'' kwanza mambo saba ya muungano mwisho chumbeee
 
Wazanzibari kwa kulalamika hatuwawezi, si muwaambie viongozi wenu waache ubinafsi wadai zanzibar yenu huru mkuu.

Waende zao hatuna hajanao tupunguze na matumizi yasiyo ya lazima, kama galama za umeme, vyuo vikuu, matibabu nk.
Watuchie nafasi zetu kariakoo, namanga, buguruni kwa mnyamani, magomeni mapipa na kwingine kulipokaliwa na wapemba kibao.
 
Najua Viongozi wetu wanapenda huu muundo kwa sababu ya Madaraka. Lakini kwa mwananchi wa Kawaida wa Zanzibar huu muundo hauna tija kwetu. Tusubiri tuone.

Kasheshe @ Bububu,
Mlikuwa mna beep muda mrefu sasa bara tunapiga pokeeni yakheee. Itafika mahali pia tuseme moewe visa kuja bara. Ni muda tuu. Ila Maalim atakuwa mefurahi sana. Niliona pale kibanda maiti juzi mlifurahi sana, ila hii itakula, kwenu.
 
Japo rasimu imejitahidi kugusia maeneo korofi lakini sioni dalili za hii katiba kukubariwa na kutumika. Ikumbukwe kuwa ili ikubarike ni lazima 3/4 ya wananchi wa pande zote za muungano inabi waikubari, na hakuxa kificho wala kigugumizi kuwa Wazanzibari hawako tayari kuendelea na aina ya Muungano tulionao. Kinachofanyika ni sawa na kiini macho tu. kama kweli tunataka katiba mpya basi kwanza tuwaache Wazanzibari wapumue maana wao wanayo katiba yao.
 
Nataka kuwe na paspot ya kuingia na kutoka znz kwani huku bara wamekuwa wengi kuanzia ajuza vijukuu vilembwe! wanajazana bara! Huku wakisema hawataki muungano!
Wana
 
Najua Viongozi wetu wanapenda huu muundo kwa sababu ya Madaraka. Lakini kwa mwananchi wa Kawaida wa Zanzibar huu muundo hauna tija kwetu. Tusubiri tuone.

Kasheshe @ Bububu,
Leo serikari 3 kesho utasikia serikari 4 mara 5 au zaidi ! Miaka 50 ya Uhuru tumeshwindwa kuwa wamoja na kuwa na serikari Moja? Na kupunguza gharama za kuiendesha serikari lufufu huku bajeti ikitegemea wafadhili toka nje
 
Kwani wazenji si mtabaki hohehahe?ardhi yenu mnairingia sio?haya!watalii wenyewe mpaka wawe summer kwao ndio waje!
 
Najua Viongozi wetu wanapenda huu muundo kwa sababu ya Madaraka. Lakini kwa mwananchi wa Kawaida wa Zanzibar huu muundo hauna tija kwetu. Tusubiri tuone.

Kasheshe @ Bububu,

Kwani sisi wa Tanganyika inatuhusu nini? We have already had our share of problems. We are now calling it a quit. Hurray!

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom