Muuguzi Na Mkunga,Naomba nafasi ya kazi.

Deva

JF-Expert Member
May 29, 2018
1,240
2,000
Habarini wakuu.

Mimi ni kijana wa Kitanzania, umri wangu miaka 24, ninayetegemewa na wazazi wangu kwa hali na mali, Nimekuwa nikijishughulisha pia na vibiashara vya hapa na pale baada ya kumaliza chuo mwaka huu course ya Nursing and Midwifery.

Kwahiyo nikaona nije huku nikutane na watu naweza pata msaada wa connection. Hivyo ndugu zangu kama unaijua zahanati, kituo cha afya,hospital,shirika au taasisi ziwe za serikali au binafsi zinahitaji mtu kama mimi naomba unisaidie kunijulisha ili nijikomboe katika jambo hili.

Na Hata kama kuna mtu humu anahitaji kufanya kazi na mtu kama mimi basi nipo hapa, na wala hatojutia, Natanguliza shukurani.

NB:Ninaweza kufanya kazi yoyote ile halali nikipata maelekezo namna ya kuifanya, sichagui, kikubwa nipate uwezo wa kujihudu mk ia na kuhudumia familia.

Nipo Mwanza.
 
Mwifwa

JF-Expert Member
Apr 3, 2017
38,831
2,000
Mimi ni Muuguzi na Mkunga wa ngazi ya Stashahada
Fanya mchakato usajiliwe kwanza(upate leseni) ndio itakuwa bora zaidi.

Angalia taratibu za kusajiliwa kwenye Nursing and Midwifery Council.
 
EMMYGUY

JF-Expert Member
Aug 6, 2015
8,740
2,000
Kuna Zahanati flani iko huku Magu nitajaribu kukuunganisha kama bado watakuwa na uhitaji wa wafanyakazi.
 
Deva

JF-Expert Member
May 29, 2018
1,240
2,000
Fanya mchakato usajiliwe kwanza(upate leseni) ndio itakuwa bora zaidi.

Angalia taratibu za kusajiliwa kwenye Nursing and Midwifery Council.
Shukrani kwa ushauri, japo ni changamoto kukaa tu kusubiri hivyo vitu, kuna baadhi ya sehemu wanapokea bila shida.
 
Mwifwa

JF-Expert Member
Apr 3, 2017
38,831
2,000
Shukrani kwa ushauri, japo ni changamoto kukaa tu kusubiri hivyo vitu, kuna baadhi ya sehemu wanapokea bila shida.
Kama kufanya practice bila malipo hapo sawa.

Ila ukiwa na leseni ni bora zaidi maana kazi zinatangazwa mara kwa mara na wanaohitajika huwa ni wale wenye leseni.

Kwa hiyo ukiwa unatafuta sehemu ya kujiegesha, fuatilia pia suala la leseni
 
Nzory Mussa

JF-Expert Member
Jan 20, 2017
480
1,000
Kama kufanya practice bila malipo hapo sawa.

Ila ukiwa na leseni ni bora zaidi maana kazi zinatangazwa mara kwa mara na wanaohitajika huwa ni wale wenye leseni.

Kwa hiyo ukiwa unatafuta sehemu ya kujiegesha, fuatilia pia suala la leseni
Ni kweli kabisa mkuu, ukiwa na leseni ni bora zaidi.
 
Deva

JF-Expert Member
May 29, 2018
1,240
2,000
Kama kufanya practice bila malipo hapo sawa.

Ila ukiwa na leseni ni bora zaidi maana kazi zinatangazwa mara kwa mara na wanaohitajika huwa ni wale wenye leseni.

Kwa hiyo ukiwa unatafuta sehemu ya kujiegesha, fuatilia pia suala la leseni
Shukrani, leseni ni mwezi wa kumi na moja kwa utaratibu wa Baraza la wauguzi.

Nasubiri.
 
tony92

JF-Expert Member
Jul 17, 2013
1,151
2,000
Habari mkuu
Wacheki ifakara health institute wametoa nafasi nyingi.
Pia tafuta tangazo la kazi la hawa jamaa wanaitwa African cheetahz archives ltd nao wametoa nafasi nyingi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom