Muuguzi Mkuu Wilaya Korogwe: DC unafanya dhambi na manung'uniko ya wauguzi Korogwe DC hayatokuacha salama

the kind

JF-Expert Member
Nov 6, 2019
728
502
Muwe na weekend ya amani na amani iwe nanyi

Kumekua na malalamiko mengi sana dhidi ya muuguzi mkuu korogwe DC kutoka kwa Watumishi wa Afya wilaya hiyo hasa wauguzi

Husikilizi shida zao

Hufuatilii/husimamii stahiki zao.

Unahusika kuwahamisha wauguzi pasipo kuwapa stahiki zao za uhamisho ikiwemo kesho za usumbufu na posho za kujikimu


Kibaya zaidi Raisi Magufuli alipoingia madarakani alisisitiza Mtumishi yeyote wa Serikali pindi atakapohamishwa apewe stahiki zake kabla ya kwenda kituo kipya alikohamishiwa lakini wewe na wakuu wenzio wa idara mmekua hamufanyi hivo na umekua si msimamizi mzuri katika hili wewe kama kiongozi lakini pia umekua ukiwakingia kifua wauguzi ambao wanafanya vibaya kwenye katika vituo vyao na hawakubaliki kabisa katika jamii kutokana na mienendo yao

Kingine kwanini imekua rahisi kwako kupokea malalamiko kutoka kwa wanasiasa hasa madiwani na kuyafanyia kazi hata kama mara nyingi malalamiko yao yanakua si ya kweli na yenye maslahi kwao.

Mfano: yupo diwani ( ) yeye akitongoza mtumishi akikataliwa basi atahakikisha mtumishi huyo anahama kwenye kata yake au mtumishi atakaeonekana yuko na msimamo tofauti na yeye lazima mtumishi huyo ataondoka kwenye kata hiyo,lakini wewe na wakuu wengine wa idara mmekua hamuwaiti watumishi wenu kuwahoji na kusikiliza pande zote mbili

Huna msaada wowote kwa wauguzi wako,kazi yako ni kuhusika na kuwahamisha wauguzi bila kuwapa stahiki zao wala kufuatilia stahiki zao wewe upo kimaslahi tu na kwa hayo maslahi yako familia za wauguzi hao zinaishi maisha ya ajabu,woga na stress nyingi za maisha maana kila siku wanaanza maisha mapya

Hii dhambi uliyoipandikiza miaka yote itakuja kukuadhibu siku yeyote
 
Ni wivu tu kwangu sasa nawaakikishieni sitabadilika na huo wizi wa madawa na Rushwa ambazo mnapenda kuchukua kwa wananchi hamtachukua mimi nikiwepo nitawabana tu sana na kuazia leo nakaza kamba sana
 
Ni wivu tuu kwangu sasa nawaakikishieni sitabadilika na huo wizi wa madawa na Rushwa ambazo mnapenda kuchukua kwa wananchi hamtachukua mimi nikiwepo nitawabana tuu sana na kuazia leo nakaza kamba sana
Kumbe ndo wewe ??
 
Mkuu the kind, pole sana. Kwemye hili andiko lako hasira inasikika zaidi kuliko taarifa uliyokusudia.

Ili tufikie malengo, ukipata nafasi ya kuandika uzi wa aina hii mahala pengine Jitahidi kubalance, hasira na taarifa either viwe sawa au taarifa izidi.

Kwa mfano, umefanikiwa kulitaja Jina la Muuguzi na kumuita shetani lakini ukashindwa kumtaja Diwani asiye tenda haki kwa wauguzi wa kike.

Kila la kheri.
 
Nimeshamwambia mimi nidhamu katika utumishi wa umma muhimu sana nikikundi ambacho nimebana mashlahi yao nanitawabana sana
 
Mtaje na huyo Diwani ili nianze kumchunguza mapema iwezekanavyo. Mimi ni Mbunge wenu ajaye wa Korogwe Mjini. Sitakua tayari kamwe kufanya kazi na Madiwani wa aina hiyo.

Na huyo Muuguzi Mkuu mwambie kabisa siku zake zinahesabika. Sijui ni kwa nini Wanawake huwa hampendani sehemu za kazi!
 
Nimeshamwambia mimi nidhamu katika utumishi wa umma muhimu sana nikikundi ambacho nimebana mashlahi yao nanitawabana sana
Unapo bana maslahi ya watu hakikisha unabana maslahi haramu, sasa isijekuwa unabana maslahi ya watu ambayo ni halali. kama hayo ya uhamisho.
 
Ni wivu tu kwangu sasa nawaakikishieni sitabadilika na huo wizi wa madawa na Rushwa ambazo mnapenda kuchukua kwa wananchi hamtachukua mimi nikiwepo nitawabana tu sana na kuazia leo nakaza kamba sana
Idiot kabisa, kwahiyo adhabu ya mtu anayeiba dawa ni kumuhamisha pasipo stahiki zake?
 
Acha hasira tulia kama maji ya mtungini kisha andika taratibu ili tukuelewe kero yako kwani unalalamika wewe kisha unajijibu wewe! Sisi tutakusaidiaje? DC kafanya nini tena asiachwe salama?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom