Muuguzi ang’oa drip za wagonjwa kwa hasira!!!na kuhatarisha kuuwa!!

pageup

Senior Member
Oct 12, 2012
156
0
1827 7463 625.jpg
28/11/012
WATOTO saba wamenusurika kuuawa kwenye hospitali ya wilaya ya Chato mkoani Geita baada ya mhudumu wa afya Maliagoreth Kyaruzi kuwanyofolea maji yenye dawa (drip) wagonjwa waliolazwa kwenye wodi ya watoto kwa madai kuwa ndugu zao walikataa kufanya usafi wa vyoo vya hospitali hiyo.
Watoto walionusurika na vifo hivyo ni Edward Robert (4), mkazi wa kijiji cha Nyamirembe; Kashinje Lukanya (12), mkazi wa Busaka; Irene Nasib (3), mkazi wa Bwanga; Naomi Tumain (5), mkazi wa Kachwamba; Eunice William (3), mkazi wa Kasala; Astelia Siajali (2), mkazi wa Kahumo; na Alphonce Makolobelo.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea jana majira ya saa 2:30 asubuhi baada ya mhudumu huyo wa afya kuwataka ndugu wa wagonjwa wote walilazwa kwenye wodi ya wanawake na watoto, kwenda kufanya usafi wa vyoo kutokana na kuwepo kwa uchafu unaodaiwa kusababishwa na wagonjwa wenyewe.
Wakizungumza na Tanzania Daima Jumatano, baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo William Masai na Ester Misungwi kwa nyakati tofauti, walisema kuwa hatua hiyo ilikuja baada ya ndugu wa wagonjwa kukaidi amri kwenda kufanya usafi kwenye vyoo vya hospitali hiyo.
Baada ya wananchi hao kukaidi amri hiyo, mhudumu huyo kwa hasira aliamua kunyofoa maji yenye dawa waliyokuwa wamening’iniziwa wagonjwa kwa ajili ya matibabu kisha kuondoka kwa majigambo, huku akiwataka watu walioumizwa na kitendo hicho, wakashtaki mahala popote ambapo wangeliona panafaa.
Hatua hiyo iliwalazimu baadhi ya ndugu wa wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo, kuutafuta uongozi wa hospitali kabla ya kuwasiliana na Katibu wa Mbunge wa jimbo la Chato, Gelvas Stephano, ambaye naye alizungumza na Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, ambaye alifika eneo la tukio akiwa ameongozana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya.
Waziri Magufuli alilazimika kuzungumza na wagonjwa na watumishi wa afya kwa lengo la kusikiliza kero zao muda mfupi baada ya kumaliza kujionea hali halisi ya watoto walionyofolewa drip za dawa kisha kurejeshewa.
Kutokana na malalamiko mengi yaliyotolewa na wagonjwa kuhusu vitendo vinavyofanywa na mhudumu huyo, Waziri Magufuli amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Chato, Rodrick Mpogolo, kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kuhakikisha wanamtafuta na kumkamata na kumfikisha mahakamani.
“Bahati nzuri mkuu wa wilaya yupo hapa na OCD na wewe upo hapa, ninaagiza huyo Maliagoreth akamatwe mara moja na kesho afikishwe mahakamani kujibu tuhuma za kutaka kuua wagonjwa saba kwa makusudi,” alisema Waziri Magufuli.
“Nasema huyo siyo mhudumu anayetakiwa kufanya kazi ya afya…maana kuwanyofolea drip wagonjwa kwa kosa la ndugu zao kukataa kufanya usafi wa vyoo haliwezi kufumbiwa macho, huyo Maliagoreth hafai na ninaomba kuanzia leo asikanyage hapa kwenye hospitali kuja kuhudumia wagonjwa…maana ipo siku hata mimi ataninyofolea drip,” alisema Magufuli na kushangiliwa na wagonjwa.
Kadhalika Magufuli aliwataka waganga na wauguzi wengine kutoa huduma nzuri kadri inavyopaswa na kuwatahadharisha iwapo watawahudumia wagonjwa vibaya kwa lengo la kulipiza kisasi kwa madai wagonjwa wamewashtaki itakuwa ni kutowatendea haki wagonjwa.
Vilevile alimwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Shaban Ntarambe, kuhakikisha anamsimamisha kazi mara moja nesi huyo kwa madai kuwa hana sifa za kuendelea kuwa mtumishi kwenye wilaya ya Chato.
Mkuu wa wilaya ya Chato, Rodrick Mpogolo, mbali na kudai kusikitishwa na tukio hilo ameahidi kuunda tume kuchunguza utolewaji wa huduma za afya kwa wananchi kutokana na kuwapo kwa malalamiko mengi.
Aidha alisema nia ya serikali ni kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma bora na kwamba dosari zinazojitokeza atahakikisha zinapatiwa ufumbuzi wa kudumu ili kusijitokeza vitendo kama vilivyojitokeza.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa hospitali ya wilaya hiyo, Dk. Pius Buchukundi, amekiri kutokea tukio hilo na kudai kuwa kitendo kilichofanywa na mhudumu wake siyo msimamo wa hospitali bali ni matakwa yake mwenyewe na kwamba atahukumiwa kwa matendo aliyoyatenda.
Dk. Buchukundi amewataka wagonjwa kutoa ushirikiano kwa uongozi wa hospitali hiyo kwenye matukio ya aina hiyo na mengine yanayoweza kuathiri sifa za hospitali na serikali.
Source: Tanzania Daima
 

Bitabo

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
1,901
2,000
huyo muuguzi asije akawa alitumwa na CCM ili Magufuli akiingilia ionekane CCM inawajali wananchi. Siasa ni mchezo mchafu sana
 

Chibolo

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
4,347
2,000
Tukio hilo linabeba ujumbe mahsusi kwa serikali! We nee to think beyond jamani.
 

Chibolo

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
4,347
2,000
Tukio hilo linabeba ujumbe mahsusi kwa serikali! We need to think beyond jamani.
 

tutaweza

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
634
500
Tanzania yetu bana! Yaani ndugu wa wagonjwa ndio wana wajibu wa kusafisha vyoo! Kumbukumbu zangu zinaonyesha ujamaa ulishakufa zamani na ndio maana wanatukata kodi za kutosha ambazo moja ya matumizi yake ni huduma za afya.
Tatizo kuu sio mhudumu, ni mfumo mzima wa watumishi wa serikali wanaotoa huduma kwa wananchi. Huwa wanataka waonekane kama wao ndio wa kunyenyekewa na wakati wanatakiwa wamchukulie yule wanayemhudumia kama mteja/mfalme. Kisa hamlipi yeye moja kwa moja anamdharau akisahau kwamba kodi zake ndio zinamtengenezea mshahara.
Hilo tukio la huyo nesi ni moja kati ya mengi sana ambayo hayajaripotiwa

Serikali inatakiwa kufumua na kuusuka upya mfumo mzima wa utoaji huduma kwa wananchi.
 

LiverpoolFC

JF-Expert Member
Apr 12, 2011
11,037
2,000
Kwa kweli inaweza ikawa hivyo!

Mafisadi hawana huruma hata kwa wapiga kura jamani??
Haya yote yanatokea kwa ajili ya uongozi legelege iliyoko madarakani ila hakika MWISHO WAO UU WAJA!


huyo muuguzi asije akawa alitumwa na CCM ili Magufuli akiingilia ionekane CCM inawajali wananchi. Siasa ni mchezo mchafu sana
 

Mwanaweja

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
3,576
1,195
siku hizi wanawake wamekuwa wakatili sana zamani walikuwa wanaume tu leo hii haki sawa wanawake ndio wanaongoza kwa ukatili
 

Ta Kamugisha

JF-Expert Member
May 17, 2011
3,431
2,000
Jamani mm Nipo maeneo aya, ni kweli uyu Dada alifanya hii kitu ila yeye so Nesi Bali ni muhudumu wa afya, na isitoshe chato kumejaa wasukuma, na unajua mila na desturi za wasukuma hawanyi chooni yaani hawatumii choo na wala hawachangii choo kimoja na wakwe

Kisa sasa, hawa wasukuma badala ya kujisaidia chooni hapa hosp wamekuwa mekuwa wanajisaidia juu ya choo na kwenye korido ya choo.

Baada ya muudumu kukuta hali inyo ndo akawataka wale wanaowaudumia wagonjwa wakatoe vinyesi vyao, baada ya Kuona wamegoma ndo akazima zile drip na si kuzinyofoa.

Ila kiukweli hawa wasukuma ni Shida hawataki kukata gogo kwenye choo tena cha kufrashi, wamezoea choo ya shimo au kukata gogo porini

Na uyu muhudumu atawashinda maana wamemshitaki kama Nesi wakati yeye ni muhudumu na mfanya usafi tu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions
Thread starter Title Forum Replies Date
Dogo G MUUGUZI,TABIBU,MGANGA au DAKTARI JF Doctor 1

Similar Discussions

Top Bottom