Muuguzi amchoma sindano ya usingizi binti aliyekuwa akimuuguza mama na kisha kumbaka

huyu muuguzi ni muuaji baridi

~alishindwa hata kupiga punyeto LA mate?
~ama hata angejiongeza kule mortuary... au kulikuwa empty.!?

huko aliko bora ajitundike tu:maana hafai hata kuwamo gerezani.
Nadhani atakuwa na matatizo ya akili mkuu, maana kati ya kesi za ubakaji nilizowahi kusikia . thisi is the sickest one
 
Ni kweli tukio hilo lipo na hiyo si mara ya kwanza kwani siku za nyuma muuguzi huyo (jina tunalo) akiwa Kituo cha Afya Tarafa ya Igurubi alifanya tukio kama hilo, hivyo hii ni mara ya pilli na huo ni ukiukwaji wa taratibu na kanuni za kiutumishi,” alisema Dkt. Deus.
Mara ya kwanza hatua hazikuchukuliwa? au alitumia condom? Huyu jamaa mara ya tatu atabaka maiti "ANA TUCHELEWESHA"
 
Hivi alikubali vipi kuchomwa sindano? tuanzie hapo, kumbuka hakuwa mgonjwa
... huyo ni mtoto (16) kaka; tena katika mazingira kama yale ya hospitali akimuuguza mama yake; msongo wa mawazo; hofu; tena usiku; tena kaambiwa na "daktari" probability ya kuhoji chochote ilikuwa 0% kwake.

Imagine hilo bazazi lingemlaghai kwa maneno kama "watu wote wanaouguza ndugu zao hapa ili kuwaepusha na maambukizi wanatakiwa kupewa dawa. Lete kidole chako cha mkono wa kushoto nikuwekee dawa kwa ajili ya usalama wako". Kwa kauli kama hiyo, tena likiongea kwa sauti tulivu kama baba mzazi kwa bintiye kipenzi, unategemea kabinti kale ka miaka 16 tena "bush" kangehoji chochote zaidi ya kuona kanaepushwa na maambukizi mle hospitalini? Nasimama na binti!
 
Hiyo ni kesi ambayo imejulikana,je ambazo hazijajulikana?Mi ninayo mashaka sana,kwenye maofisi,uhuni mwingi unafanyika.Hapo ujiulize wadada na wamama ambao wanaelewana na watumishi wa afya kufanya ngono vyumbani mahospitalini ni wangapi?Manesi wangapi wakike hufanya hivyo?Ni wengi sana,we mwanaume au mwanamke,ukitaka kuwa na mahusiano na baadhi ya watumishi wa baadhi ya kada,jiandae kisaikolojia.
TANESCO,JESHINI etc,ni hatari.
 
Jina na binti( HIMEHIFADHIWA) hata la mbakaji(Limehifadhiwa)
Hospitali anayofanya na alikofanya zamani ZIMETAJWA
Jina la mama mgonjwa na mzazi wa binti yaliyebakwa LIMETAJWA

Siri hapo ipo wapi?
 
Duh!!. Haya ni matumizi mabaya ya pharmacology!. Kama ni kweli inabidi hatua Kali zichukuliwe dhidi yake ikiwa ni pamoja na watu waliomuamisha kutoka kituo cha afya alikofanya unyama kwa Mara ya kwanza. Hospital deserves to be a safe place where sick people get hope and not a place where people get harm!
 
Kumbe kuna wanaume uvumilivu wao Zero kabisa, yaani bado siku 2 tubebwe na upepo wa kisulisuli kupelekwa Mlima wa Moto, huku lenyewe linabaka?
 
Alitenda kosa hilo sehemu nyingine, kaamishiwa hapo katenda tena napo watamhamishia sehemu nyingine tena
Yaani hili ndio nimeshindwa kulielewa. Hawa viumbe wanafanya maamuzi (ya kuhamisha) utafikiri hawajazaliwa na wanawake!!!!! :mad: :mad: :mad:
 
Duh!!. Haya ni matumizi mabaya ya pharmacology!. Kama ni kweli inabidi hatua Kali zichukuliwe dhidi yake ikiwa ni pamoja na watu waliomuamisha kutoka kituo cha afya alikofanya unyama kwa Mara ya kwanza. Hospital deserves to be a safe place where sick people get hope and not a place where people get harm!
Kwamba walimhamisha vile zilikuwa ni tuhuma tu!! Mungu atawalaani!! :mad::mad::mad:
 
MUUGUZI mmoja wa Hospitali ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, amedaiwa kumbaka binti wa miaka 16 (jina linahifadhiwa), mkazi wa Mtaa wa Buyumba, Kata ya Igunga Mjini, ambaye alikuwa akimuuguza mama yake aliyekuwa amelazwa hospitalini hapo.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Dk. Ruta Deus, alikiri kuwepo kwa tuhuma hizo.

“Ni kweli tukio hilo lipo na hiyo si mara ya kwanza kwani siku za nyuma muuguzi huyo (jina tunalo) akiwa Kituo cha Afya Tarafa ya Igurubi alifanya tukio kama hilo, hivyo hii ni mara ya pilli na huo ni ukiukwaji wa taratibu na kanuni za kiutumishi,” alisema Dk. Deus.

Alisema suala hilo tayari liko polisi na wao wanaendelea kuchukua hatua dhidi ya muuguzi huyo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini hapo, mama wa msichana huyo, Wande Salum (42) aliyekuwa amelazwa wodi no. 3, alisema tukio hilo lilitokea Oktoba 10, mwaka huu, saa 4 usiku.

Wande alidai kuwa muuguzi huyo alifika katika wodi hiyo kuangalia hali yake na baada ya kumuona alimwambia ambadilishe dawa.

Alidai kuwa muuguzi huyo aliomba aondoke na mwanawe aliyekuwa akimuuguza na walipofika ofisini alimchoma sindano ya usingizi kisha kumbaka kuanzia saa 4 usiku hadi saa 8.

Wande alidai baada ya kuona muda umekuwa mrefu pasipo mwanawe kurudi wodini, aliomba msaada kwa baadhi ya wagonjwa wenzake wenye hali nzuri wamsaidie kumtafuta.

Alidai kuwa baadhi ya manesi waliokuwa zamu walipopata taarifa hiyo, waliungana na baadhi ya wagonjwa kumtafuta mwanawe na walimkuta eneo la nyasi wanakofulia nguo kina mama akiwa hajitambui, huku akiwa amemwagiwa maji mwilini.

Wande alidai kuwa baada ya kumwondoa katika nyasi hizo, walikuta akivuja damu sehemu za siri kutokana na kubakwa kwa muda mrefu na muuguzi huyo.

Aidha mama huyo alisema kitendo alichofanyiwa mwanawe ni cha kinyama na hakipaswi kufumbiwa macho, huku akiomba vyombo vya dola kumsaka muuguzi huyo apatikane na kufikishwa mahakamani.

Baadhi ya kina mama wanaokwenda kutibiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga, Rehema Julias na Sada Mwinamila, walisema hivi sasa wameingiwa na hofu kutokana na kitendo hicho na kuiomba Serikali kutofumbia macho suala hilo.

Alipotafutwa muuguzi huyo kwa njia ya simu, ilikuwa imezimwa.

Mkuu wa Wilaya ya Igunga, John Mwaipopo, alipoulizwa kuhusu suala hilo, alisema bado hajapokea taarifa yoyote dhidi ya muuguzi huyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Barnabas Mwakalukwa, alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo dhidi ya muuguzi huyo, alisema bado hajapokea taarifa hiyo.

Chanzo: Mtanzania
Huyu Dr Deus ni mpuuzi. Ikiwa alifahamu muuguzi huyo alishafanya kosa kama hilo aliruhusuje aendelee kutoa huduma hapo? Kisha ni yeye tu mwenye taarifa katika uongozi ws jiu wa Mkoa kwa suala nyeti kama hili. Ni fedheha kubwa kwa sekta ya afya.
 
Back
Top Bottom