Muuguzi amchoma sindano ya usingizi binti aliyekuwa akimuuguza mama na kisha kumbaka

SAA 4 hadi SAA 8. Wakaanza kumtafuta SAA ngapi? Au hayo ni makadirio?
 
MUUGUZI mmoja wa Hospitali ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, amedaiwa kumbaka binti wa miaka 16 (jina linahifadhiwa), mkazi wa Mtaa wa Buyumba, Kata ya Igunga Mjini, ambaye alikuwa akimuuguza mama yake aliyekuwa amelazwa hospitalini hapo.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Dk. Ruta Deus, alikiri kuwepo kwa tuhuma hizo.

“Ni kweli tukio hilo lipo na hiyo si mara ya kwanza kwani siku za nyuma muuguzi huyo (jina tunalo) akiwa Kituo cha Afya Tarafa ya Igurubi alifanya tukio kama hilo, hivyo hii ni mara ya pilli na huo ni ukiukwaji wa taratibu na kanuni za kiutumishi,” alisema Dk. Deus.

Alisema suala hilo tayari liko polisi na wao wanaendelea kuchukua hatua dhidi ya muuguzi huyo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini hapo, mama wa msichana huyo, Wande Salum (42) aliyekuwa amelazwa wodi no. 3, alisema tukio hilo lilitokea Oktoba 10, mwaka huu, saa 4 usiku.

Wande alidai kuwa muuguzi huyo alifika katika wodi hiyo kuangalia hali yake na baada ya kumuona alimwambia ambadilishe dawa.

Alidai kuwa muuguzi huyo aliomba aondoke na mwanawe aliyekuwa akimuuguza na walipofika ofisini alimchoma sindano ya usingizi kisha kumbaka kuanzia saa 4 usiku hadi saa 8.

Wande alidai baada ya kuona muda umekuwa mrefu pasipo mwanawe kurudi wodini, aliomba msaada kwa baadhi ya wagonjwa wenzake wenye hali nzuri wamsaidie kumtafuta.

Alidai kuwa baadhi ya manesi waliokuwa zamu walipopata taarifa hiyo, waliungana na baadhi ya wagonjwa kumtafuta mwanawe na walimkuta eneo la nyasi wanakofulia nguo kina mama akiwa hajitambui, huku akiwa amemwagiwa maji mwilini.

Wande alidai kuwa baada ya kumwondoa katika nyasi hizo, walikuta akivuja damu sehemu za siri kutokana na kubakwa kwa muda mrefu na muuguzi huyo.

Aidha mama huyo alisema kitendo alichofanyiwa mwanawe ni cha kinyama na hakipaswi kufumbiwa macho, huku akiomba vyombo vya dola kumsaka muuguzi huyo apatikane na kufikishwa mahakamani.

Baadhi ya kina mama wanaokwenda kutibiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga, Rehema Julias na Sada Mwinamila, walisema hivi sasa wameingiwa na hofu kutokana na kitendo hicho na kuiomba Serikali kutofumbia macho suala hilo.

Alipotafutwa muuguzi huyo kwa njia ya simu, ilikuwa imezimwa.

Mkuu wa Wilaya ya Igunga, John Mwaipopo, alipoulizwa kuhusu suala hilo, alisema bado hajapokea taarifa yoyote dhidi ya muuguzi huyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Barnabas Mwakalukwa, alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo dhidi ya muuguzi huyo, alisema bado hajapokea taarifa hiyo.

Chanzo: Mtanzania

Inasikitisha sana kupita kiasi, it's more than danger!
Kama ana HIV Je KWA utaratibu huu amekuwa kawaambukiza watu wangapi??

Ndio maana Mimi siungi mkono kabisa harakati za kufutwa KWA hukumu ya kifo.
Hukumu ya kifo KWA kweli isifutwe, iendelee kuwepo NA itolewe KWA wale watu wanaohitaji kama huyu muuguzi.
 
Ni kweli tukio hilo lipo na hiyo si mara ya kwanza kwani siku za nyuma muuguzi huyo (jina tunalo) akiwa Kituo cha Afya Tarafa ya Igurubi alifanya tukio kama hilo, hivyo hii ni mara ya pilli na huo ni ukiukwaji wa taratibu na kanuni za kiutumishi,” alisema Dkt. Deus.

Halafu mnamwangalia tu? Asipofanya hiyo kazi ya uuguzi dunia itasimama au? Jinga kama hilo muda huu lilitakiwa liwe limenyongwa hadi kufa; hatuhitaji majitu mapuuzi kama hayo katika jamii.
Huyo daktari anatakiwa awajibishwe kwa kumlinda huyo, au kisheria hana kosa?
Yaani mtu afanye ubakaji kwa staili hiyo kisha umlinde?
 
Mtu kafanya kosa anahamishiwa sehem nyngne,tena kosa lenyewe la kufungwa sio chini ya miaka 30.Tunavuna tulichokipanda
 
huyu muuguzi ni muuaji baridi

~alishindwa hata kupiga punyeto LA mate?
~ama hata angejiongeza kule mortuary... au kulikuwa empty.!?

huko aliko bora ajitundike tu:maana hafai hata kuwamo gerezani.
 
Sijaona connection ya moja kwa moja kwa aliyembaka ni huyo muuguzi. Nilijua amefumaniwa akiwa na huyo mtoto. Kumbe mtoto kakutwa kazimia kwenye nyasi!!
 
Aisee!. Sina hakika kama huyu binti aliyebakwa atakuja kuwapenda wanaume. Maana Bikra yake imebanjuliwa kikatili sana. Na huyo Muuguzi wa kuime hastahili kuendelea kuwepo kazini, wala hastahili kuhamishwa kituo cha kazi. Jela ndio kunakomfaa akakutane na mabandidu wenzake wenye tabia kama zake.
 
Alitaka apate cha kupost hapa..

..

Alafu huyu jamaa si niyuleyule ambaye kile kipindi napo kesi yake ilikua hihii ya kumchoma sindano nakubaka??

Inamaana hakuchukuliwa Hatua badala yake akaamishwa au????
 
Alitaka apate cha kupost hapa..

..

Alafu huyu jamaa si niyuleyule ambaye kile kipindi napo kesi yake ilikua hihii ya kumchoma sindano nakubaka??

Inamaana hakuchukuliwa Hatua badala yake akaamishwa au????
 
Alitaka apate cha kupost hapa..

..

Alafu huyu jamaa si niyuleyule ambaye kile kipindi napo kesi yake ilikua hihii ya kumchoma sindano nakubaka??

Inamaana hakuchukuliwa Hatua badala yake akaamishwa au????
 
Nimeshindwa kabisa kuelewa.
Huyo Dr. Deusi naye, mpumbavu wakupigwa chini, hasa mtu anafanya tabia ovyo za kiuaji, si mara ya kwanza. Kama ana UKIMWI??

kama ameweza fanya ujinga huu bila mahesabu kujua kama anaweza kushtukiwa si kichwani amna kitu, mna mkabidhi vipi afya za watu??
 
Back
Top Bottom