Muuguzi aliyetuma picha ya Tsvangirai akutwa amekufa

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
pic+zimbabwe.jpg


Mwanadada huyo alizua gumzo baada ya kusambaa picha kwenye mitandao ya jamii iliyomwonyesha akiwa kando ya Tsvangirai aliyekuwa amedhoofu kwa maradhi kitandani hospitalini. Ncube alishambuliwa na watu wengi kutoka kila kona ya nchi kwa kitendo hicho.

Muuguzi wa Zimbabwe anayefanya kazi katika hospitali ya Afrika Kusini na ambaye alizua gumzo baada ya kuonekana amepiga picha na kiongozi wa zamani wa MDC-T Morgan Tsvangirai akiwa anaumwa ambaye baadaye alifariki dunia, naye amekutwa amekufa.

Gazeti la The Herald limeripoti kuwa tayari polisi wa Afrika Kusini wameanzisha uchunguzi kuhusu kifo cha muuguzi huyo ambaye alikuwa akimhudumia Tsvangirai alipokuwa amelazwa katika hospitali ya Johannesburg, Afrika Kusini akitibiwa maradhi ya kansa ya utumbo mpana.

Tsvangirai alifariki dunia kwa maradhi hayo na alizikwa nyumbani kwake katika kijiji cha Buhera wiki iliyopita.

Inahisiwa kwamba muuguzi huyo Nomsa Ncube (44) aliuawa Februari 18 na washambuliaji wasiojulikana katika nyumba yake katikati ya Johannesburg. Ncube, anayetoka Esigodini eneo la Matabeleland Kusini aliajiriwa ma Kituo cha Tiba cha Wits Donald Gordon Medical Centre (WDGMC).

Mwanadada huyo alizua gumzo baada ya kusambaa picha kwenye mitandao ya jamii iliyomwonyesha akiwa kando ya Tsvangirai aliyekuwa amedhoofu kwa maradhi kitandani hospitalini. Ncube alishambuliwa na watu wengi kutoka kila kona ya nchi kwa kitendo hicho.

Vyanzo vya habari vilivyokaribu na watu wanaoshughulikia uchunguzi wanasema kwamba mwili wake ulikutwa na binti wa kazi ukiwa kwenye dimbwi la damu siku ambayo alipaswa kujieleza mbele ya Kamati ya Nidhamu ya WDGNC kuhusiana na picha iliyosambazwa mitandaoni.

Balozi mdogo wa Zimbabwe nchini Afrika Kusini, Batiraishe Mukonoweshuro alisema bado hawajapata mrejesho kutoka polisi. "SAPS wameanzisha uchunguzi kuhusu mkasa huo ili kubaini mazingira ya kifo chake," alisema.

Chanzo: Mwananchi
 
mshana jr nadhani ujumbe wa post hii unaakisi kilr kilicho kwenye uzi wako wa maana ya picha katika ulimwengu wa roho.
 
Wazim wakatili sana na pia wana ubaguzi hawa washona wa Harare na Wandebele wa Bulawayo ni paka na panya huyo dada atakua kauawa na hao manyamela...
 
Back
Top Bottom