Muuguzi aliyempiga Mjamzito vibao akutwa na hatia na kuondolewa kwenye baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania

Kweli mnathubutu kumtetea nesi aliyemwacha mama mjamzito mwenyewe (angeweza kupoteza maisha yake na ya mtoto!); na kana kwamba hiyo haitoshi, anathubutu kumchapa vibao??? Huyo angefukuzwwa na kifungo juu! Sijui mnatetea nini hapa! Kama mapapa wanafanya makosa, nao wachukuliwe hatua stahiki! Kazi ya unesi/udaktari inahitaji moyo wa huruma kwa mgonjwa, hata kama hali ya kazi ni ngumu!
 
Aisee pole Sana Dada Muuguzi;

Wakati mwingine shetani huwa anazunguka zunguka kumtafuta wa kwenda naye huwa ni busara Sana kuepuka ugomvi na mtu yeyote.

Wengine tumejifunza hapa, life goes on.
 
BARAZA la Uuguzi na Ukunga Tanzania, limemwondoa kwenye orodha ya wauguzi na wakunga Tanzania, Valentine Kinyanga wa kituo cha afya Mazwi, Sumbawanga Mkoa wa Rukwa, baada ya kumkuta na hatia ya kumpiga vibao Zulfa Said aliyefika kujifungua kituoni.

Tukio hilo, lilitokea tarehe 5 Januari 2021, saa nne usiku, ilidaiwa Muuguzi, Valentine Kinyanga alimpiga vibao Zulfa Said ambaye alifika kituoni hapo kujifungua.

Akisoma hukumu hiyo jana Ijumaa tarehe 22 Januari 2021, mbele ya wakili wa Serikali, Fortunatus Mwandu, Mwenyekiti wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Abner Mathube alisema, baraza limemtia hatiani mlalalamikiwa (Valentine) chini ya kifungu 26(a)(c) ya sheria ya uuguzi na ukunga kwa kosa la kwanza na la pili.

Mathube alisema, baraza lilichambua maelezo ya mlalamikiwa, mlalamikaji pamoja na mashahidi kuhusu kosa la kwanza la kumpiga mgonjwa kinyume na kifungu 25(3)(c)cha sheria ya uuguzi na ukunga Tanzania.

Katika kosa la kwanza, lililotolewa ushahidi, ulithibitisha ni kweli mlalamikiwa alimpiga mlalamikaji na mtuhumiwa alikiri kumpiga mlalamikaji

Mathube alisema, kosa la pili, lilikuwa ni kushindwa kusimamia maadili na weledi wa kitaaluma kinyume na kifungu 25(3)(k), lilithibitika kwa mtuhumiwa kushindwa kufuata utaratibu wa utoaji wa huduma za uuguzi na ukunga kwa mlalamikaji.

Kushindwa kuchukua na kuhifadhi taarifa za vipimo vya mgonjwa, kushindwa kufuatilia mwenendo wa uchungu wa mgonjwa wakati wa kumpokea katika kituo cha kutolea huduma na kuruhusu mtu ambaye sio mtaaluma kumpima mlalamikaji (mgonjwa)

“Kwa kuzingatia utetezi wa mlalamikiwa na ushahidi uliotolewa na mlalamikaji na mashahidi, umethibitisha mashitaka yote kama alivyo shtakiwa na mlalamikaji na kwa kuangalia uzito wa makosa yaliyobainishwa dhidi ya mlalamikaji.

“Ya kwamba, angeweza kusababisha madhara makubwa kwa kumchapa vibao mama ambaye alikua tayari amejifungua pasipo msaada wake, muuguzi huyo alipaswa kumuhudumia kwa weledi na upendo mkubwa,” alisema Mathube

Alisema, kutokana na hayo, baraza limempa adhabu ya kumuondoa kwenye orodha (Rolls) ya wauguzi na wakunga Tanzania chini ya kifungu 28(3)(a) cha sheria ya uuguzi na ukunga Tanzania ya mwaka 2010 na kutakiwa kurejesha vyeti na leseni kwa muuguzi mkuu wa mkoa wa Rukwa ambaye atawasilisha kwa Baraza.

Hata hivyo, Mwenyekiti huyo alisema, haki ya rufaa imeelezwa chini ya kifungu 31(1) cha sheria ya uuguzi na ukunga Tanzania ambapo anaweza kukata rufaa kwa waziri mwenye dhamana ndani ya miezi mitatu tangu tarehe ya hukumu.

Mara baada ya hukumu hiyo kutolewa, Rais wa Chama Cha Wauguzi Tanzania (TANNA), Alexander Baluya, aliwataka wauguzi kufanya kazi kwa weledi licha ya changamoto ya watumishi hasa katika kada ya uuguzi.

Baluya aliwataka wauguzi wote nchini, kuishi kwa kufuata miongozo ya taaluma yao kwani kukiuka maadili ya taaluma yao inawaondolea sifa na kuonekana muuguzi sio rafiki wa mteja.

Kuhusu changamoto ya upungufu wa watumishi, Baluya alisema suala hili lipo mamlaka nyingine hivyo wauguzi wanapaswa kulinda hadhi ya taaluma yao kwenye vituo vya kutolea huduma za afya mahali walipo.


Picha yake tafadhali ili tukikutana naye tumpishe mbali kama Masudi
 
Kumbe baraza la wauguzi lina mamlaka ya kufuta kazi mwajiriwa?
Kunyang'anywa leseni ya kazi ni sawasawa na kufukuzwa kazi. Moja kwa moja hapo muajiri hawezi kuendelea na mkataba na mtu ambae amethibitika kwenda kinyume cha maadili ya kiapo chake
 
The best way was kuhamisha badala ya kumfutia usajili na hatimaye kukosa sifa ya kufanya huduma nchini
Ili aendelee na ukatili? Watanzania mbona hatujipendi,!!! hatujihurumii?!!! Huyu Anaonekana anachojali ni mshahara na sio huduma takatifu anayotakiwa kuitoa kwa umma. Kwa tabia hiyo unadhani vifo vya kizembe na madhara yatokanayo na utendaji mbaya wa watu wa kaliba yake vitakwisha? Tujihurumie,kuna field hazihitilaji ujanja ujanja. Akafanye shughuli nyingine hata kilimo.
 
Vp
Hivi aliyechapwa vibao angelikuwa mkeo au mama yako Au mwanao ungeliandika ujinga huu?
km aliyefukuzwa angekuwa mama yako au mkeo?
Ni kweli alifanya kitendo kibaya na hakikubaliki lakini adhabu aliyopewa ni kali mno.
Wangeweza hata kumkata mshara kwa miezi kadhaa wampe fidia aliyepigwa
 
kama hana akiba ya kueleweka na vitega uchumi atateseka sana na atajuta siku zote..... Hata kama una hasira ni vizuri kukishusha muda mwingine na kuacha baadhi ya votu vipite tu....tusiache hasira zituongoze
Hasira ukaa moyoni mwa mtu mjinga na mpumbavu
 
Back
Top Bottom