Muuguzi adaiwa kumzaba makofi mwanamke aliyejifungulia sakafuni

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,007
9,873
Muuguzi wa zamu katika Kituo cha Afya Mazwi mjini Sumbwanga anadaiwa kumzaba makofi usoni mwanamke mmoja aliyejifungulia sakafuni kwenye moja ya vyumba vya kituo hicho juzi usiku.

Taarifa zilizopatikana kutoka kwenye kituo hicho, zinasema mama huyo ambaye jina lake halijawekwa hadharani, alifika hapo kujifungua na kitendo cha kujifungulia sakafuni kilimkera muuguzi huyo.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbwanga, Jacob Mtalitinya alikiri kutokea kwa tukio hilo na kuwa tayari wamemsimamisha kazi muuguzi huyo aliyemtaja kwa jina la Valentine Kinyaga ili kupisha uchunguzi wa tukio hilo.

Shuhuda wa tukio hilo, ambaye hakutaka atajwe gazetini alieleza kuwa mjamzito huyo alifika kwenye kituo hicho cha afya cha Mazwi yapata saa 7.00 usiku.

Alipofika kwenye kituo hicho, taarifa zinaeleza alifuata taratibu za kawaida za kuonana na watu wa mapokezi na wauguzi waliokuwa hapo.

Mama huyo inadaiwa alipokewa na muuguzi huyo aliyekuwa zamu na kupelekwa chumba maalumu kwa ajili ya kusubiri kujifungua.

“Baada ya kufika kwenye chumba hicho, inadaiwa muuguzi huyo alimwelekeza asubiri kuhudumiwa.

“Ila sasa baada ya kuwa amewekwa kwenye chumba hicho, muuguzi aliondoka,” anasimulia shuhuda, ambaye alikwenda hapo kwa matibabu na kushuhudia mkasa huo.

Habari zaidi zinadai kwamba, baadaye mjamzito huyo alianza kulalamika amebanwa na uchungu lakini muuguzi huyo alipokwenda tena chumbani humo alimtaka aendelee kusubiri.

“Wakati mama huyo anaendelea kusubiri, ilifika hatua ya kujifungua na akatandika kanga yake sakafuni na kujifungua.

Inaelezwa kuwa baada ya kujifungua, wanawake waliokuwa katika chumba hicho wakisubiri kujifungua walimuita muuguzi huyo wa zamu na kukuta mama huyo amejifungulia sakafuni.

Hata hivyo, baada ya kupewa taarifa ile, muuguzi huyo alianza kuhamaki kwa hasira kutokana na kuchukukizwa na kitendo cha mama huyo kujifungulia kwenye sakafu ya hospitali ile.

Muuguzi huyo inadaiwa alianza kumpiga makofi mama huyo huku akimfokea kwanini amejifungulia sakafuni pasipo kumtaarifu yeye ili ampeleke chumba cha kujifungulia.

“Muuguzi alikuwa mkali hasira zilimpanda zaidia akampiga makofi usoni yule mama,” alieleza shuhuda yule.

Shuhuda huyo anadai baada ya kumpiga makofi, ndipo alianza kumsaidia kwa kumtoa mtoto na kuendelea kumpa huduma.

Kitendo cha mama huyo kupigwa makofi na muuguzi kiliwaudhi sana ndugu zake waliokuwa wakimsubiri ajifungue.

Inadaiwa walitoa taarifa kwa uongozi wa hospitali hiyo, ambapo ulipeleka taarifa katika mamlaka za juu za kiutawala wa hospitali hiyo ili uchukue hatua stahiki.

Kufuatia tukio hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Sumbwanga, Mtalitinya alisema wamemsimamisha kazi muuguzi hiyo ili kupisha uchunguzi wa tukio hilo.

Alipoulizwa kama atachukuliwa hatua za kisheria, Mtalitinya alieleza kuwa hatua yao ya kwanza ni kufanya uchunguzi.

Mtalitinya alisema kwa upande wake madaraka yake yanaishia katika kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya mtumishii huyo, ila sasa aliyefanyiwa kitendo hicho ana uhuru wa kuamua kama atataka kuchukua hatua za kisheria.
 
Wamama wengi wanapitia kadhia hizi za kuburutwa na matusi ya fedheha toka kwa hao wanaoitwa manesi hasa wa hospitali ya umma, wakiitwa wamama watoe shuhuda zao jamii itashangaa! Ole wenu enyi manesi waovu! siku mkijaribu vitendo hivyo haramu kwa ndugu yangu nitahakikisha nazaa na nesi husika!
 
Manesi wakiwa kwenye mavazi yao na majengo yale wanajiona Waungu watu
 
Huyo nesi anatakiwa aandamwe ipasavyo ili haki ya mama huyo ipatikane, na iwe fundisho kwa manesi wenye tabia hizo!
 
Ee Mungu wajalie kina mama wote moyo wa uvumilivu kuanzia kutunza mimba mpka siku ya kuleta kiumbe duniani ule uchungu Mungu aliuweka kwetu kwa sbb tunaweza kuvumilia maumivu makali jamani yale ni maumivu makali ambayo hata ktk sayansi hakuna maumivu yanayozidi maumivu ya uchungu wa kujifungua Inshort hayana mfanowe. Huyo nesi ni either ni mgumba au ana roho mbaya kwa sbb kama ni mzazi amepitia haya anajua kbs ktk stage hyo hta kunyanyua mguu hauwezi sasa angepandaje kitandani au kutembea?. Ikishafika stage ya ku push hakuna mjadala utapush any where kwa sbb ni mwili una force kufanya hivyo. Dah nimeumia kwa kweli.
 
Ukisikia lawama ndio hizi, hivi huyo mama angefikwa umauti huyo muuguzi bado uchunguzi ungefanyika? Huu upuuzi upo hadi kwa wale waapuzi wakuu wa wilaya kupiga watu fimbo!! Natamani saana siku initokee nitoe mfano kwa taifa hili haijalishi nimekosa kiasi gani lakini hakuna mtu wa kuniadhibu kwa namna yoyote bila mamlaka husika. SHEENZZZ
 
Kama Waziri mpya wa Afya Dr. Gwajima akilikalia kimya hili basi nae hamna kitu kama wengine. Wanaojifungua wananyanyaswa sana na hamna hatua zinazochukuliwa uongozi umelala
 
Halafu manesi wote wa wodi ya wazazi au labor huwa na roho mbaya na matusi nimeshuhudia hii government.
 
Back
Top Bottom