Story Room
Member
- Nov 27, 2020
- 56
- 147
Sultan Uwezo
🇹🇿 +255
Mchungaji Rodney alisimamisha gari lake kando ya mto senegal na kisha akashuka chini taratibu akijikagua suruali yake ya kadeti ya kaki ambayo ilikuwa imechafuka sana.
Iliitazama kwa muda akajaribu kuipukuta lile vumbi lakini hakuweza hivyo aliamua kuachana nayo na kuelekea mtoni ambako kwa mbali kulikuwa na watoto waliokuwa wakiogelea.
"Yaani ningeipata furaha kama ya hawa watoto japo kwa dakika moja tu ningefarijika sana aisee lakini kila siku matatizo tu kwangu kwanini?"
Alijisemesha akiketi kwenye jiwe lililokuwa kando ya maji na kuanza kuyachezea maji kwa mikono yake.
Na kwa kumuangalia ni dhahiri alikuwa na jambo kichwani linalomsumbua.
" Hivi kwanini Bartholomew haupatikani? Na kwanini ulinifanganya kuwa umeshaziweka hela kwenye akaunti? Mbona nashindwa kupata majibu ya moja kwa moja mimi Rodney?" Alivua miwani yake na kuanza kuitazama.
Aliketi pale kwa dakika kadhaa kisha aliona aondoke zake hivyo alianza kuufuata mto ule mpaka walipokuwa wale watoto waliokuwa wakiogelea na baada ya kuwafikia alitoa simu yake mfukoni na kuanza kuwapiga picha, tendo lile kiasi fulani lilimsahulisha na kilichotokea kwani alionekana kukifurahia sana mpaka pale simu ilipoita.
"Mke wangu kipenzi." Aliita baada ya kupokea.
"Uko wapi mume wangu?" Mke wake alimuuliza.
"Niko nje ya mji kidogo najaribu kuutafuta utulivu wa akili mke wangu vipi kuna tatizo huko?" Alimuuliza.
"Hapana si kawaida yako mpaka muda huu hata kunipigia simu?"
"Kichwa hakiko vizuri nisamehe mke wangu dakika chache nitakuwa hapo." Alimjibu akiitazama saa hakika muda ulikuwa umesogea hivyo alipandisha kimlima kutoka kule mtoni mpaka alipolifikia gari lake aliwasha na kuondoka. Kijua kikiwa kinazama Mchungaji Rodney aliwasili nyumbani.
" Piiii pipiii...... " Alipiga honi afunguliwe geti. Mlinzi alichungulia kupitia mlango mdogo na baada ya kujua ni mwajiri wake haraka alifungua geti. Baada ya kupaki gari alimwita mlinzi kwa kumpigia honi.
"Ndani kuna nani?"
"Kwa sasa hakuna mtu, mama katoka muda huu kasema anarudi muda si mrefu."
"Okay kaendelee na kazi."
"Sawa bosi."
Mchungaji Rodney alishuka kwenye gari na kuingia ndani ambako aliongoza moja kwa moja chumbani kwake huko alifungua kabati lenye biblia akaichukua moja na kurudi nayo sehemu ambayo huitumia kusali na hapo alipiga magoti na kuanza kusali.
Lakini wakati hayo yote yakifanyika mke wake alikuwa katulia kwenye gari lake ambalo alikuwa amelipaki kwenye uchochoro wa kuja nyumbani kwake huku macho yake yakiwa kwenye laptop yake akifuatilia kila tukio lililokuwa likifanywa na mume wake.
"Hivi nje ya huyu Bartholomew ni nani mwingine alikiona kichupa?" Mchungaji alikuwa akiongea peke baada ya kuinuka kutoka kwenye eneo la sala.
"Hivi kwanini hiki kichupa kimemchanganya sana huyu mwanaharamu? Ni cha nini?" Mke wake akiwa kakishika alijiuliza maswali ambayo majibu yake hakuwa nayo, aliifunga laptop na kisha aliondoka lile eneo kurudi nyumbani kwake.
"Mke wangu ulikuwa wapi?"
Mchungaji alimuuliza mke wake.
"Nilikuwa dukani kuna vitu vilikuwa vimepungua ndani nikaona nisisubiri kesho wakati muda huu nina nafasi."
"Sawa sawa mke wangu." Alimjibu akifungua friji.
"Hivi mume wangu una nini maana siku kadhaa hizi sikuelewi vizuri ni kama kuna jambo linakusibu lakini hautaki kuliweka wazi."
"Ni uchovu tu mke wangu unafikiri kuna lolote basi hakuna." Mchungaji alimjibu akinywa maji.
"Sawa mume wangu wacha nikaoge."
Alimuaga na kuingia chumbani. Akiwa chumbani Catherine alitoa simu yake na kumpigia mtu ambaye hakujulikana mara moja wana uhusiano gani naye.
"Nisikilize Jumbe, huyu mpuuzi keshaanza kuchanganyikiwa na huu ni mwanzo tu, sasa cha kufanya ninahitaji umuandae huyo mpuuzi alfajiri na mapema tunakwenda kuimaliza kazi yetu."
"Itakuwaje bosi hawezi kukushtukia kweli?" Jumbe alimuuliza.
"Hiyo kazi niachie mimi wewe fanya kama nilivyokueleza sawa?"
"Sawa bosi." Jumbe alimjibu. Na kisha Catherine akakata simu na kuiweka pembeni akaoga na baada ya kumaliza alitoka na kumkuta mume wake akiwa anapitia nyaraka kadhaa.
"Mume wangu..!" Catherine alimwita mume wake.
"Naam mke wangu." Aliitika Mchungaji.
"Nilikuwa naomba ruhusa kesho niende kijijini nikaione mifugo yetu kama ujuavyo majukumu ya hapa na pale yamesababisha kukosa muda wa kutembelea mashamba na mifugo na ukizingatia vifaranga ndiyo vina majuma mawili tu."
" Mungu wangu unajua mke wangu akili haikuwepo kabisa upande huo yaani toka Bartholomew aingilie mambo yangu nimechanganyikiwa sana. Ningependa tuongozane ila wewe nenda kaangalie inaendeleaje mimi ngoja nimalizie majukumu yangu na kama nikimaliza mapema nitakufuata mke wangu, ulikuwa unategemea kuwa huko kwa siku ngapi?" Mchungaji alimuuliza mke wake Catherine.
" Kama nikikuta iko vizuri sitakaa sana labda siku mbili hivi ila ikiwa tofauti hapo nitakupigia simu kuomba siku nyingine zaidi za kuihudumia." Alimjibu huku akimng'ong'a kisogoni.
" Wala usijali mke wangu kumbe itabidi nimtaarifu mzee Daud akupokee na pia uongozi wa kanisa utatakiwa kujulishwa juu ya uwepo wako au unaonaje?" Mchungaji alishauri.
" Hapana Mchungaji mimi nafikiri usiwataarifu kwani kwa kufanya hivyo watanipokea kwa ukubwa wangu kitu ambacho kitanifanya nishindwe kushughulikia shamba langu. Wewe usiwaambie kitu chochote waje washangae niko kijijini." Catherine alimjibu mume wake kile ambacho alikifikiria.
"Hakuna tatizo mke wangu kama umeona iwe hivyo sawa ila tu tahadhari ni muhimu ukifika toa taarifa ili wajue uwepo wako."
"Sawa mume wangu wala usiwe na wasiwasi juu yangu nitakwenda salama na nitarudi salama tu lakini kuna kitu umeongea hapa sijakielewa vizuri."
"Kipi mke wangu?" Mchungaji aliachia ile karatasi na kumgeukia mke wake.
"Umesema Bartholomew sijui kafanyaje?"
"Aaahh huyo achana naye mke wangu kuna pesa nilimkabidhi apeleke benki lakini cha ajabu akaunti bado haijapokea hela yoyote ile mpaka sasa na kinachotuchanganya akili hapatikani hewani wala kwake yaani sijui itakuwaje na ukizingatia tulimuamini tu kwenye nafasi hiyo ya uhasibu hajasomea kokote kule, na hatujui Wahisani wetu wakilijua hili itakuwaje?" Alimjibu akijifuta jasho usoni.
" Mhh yaani jambo kubwa kiasi hicho unakaa nalo tu bila kunishirikisha Mchungaji? Au hatuaminiani?" Catherine alimtupia lawama Mchungaji.
" Hapana siyo hivyo mke wangu kumbuka si suala langu peke yangu linahusu kanisa hivyo baada ya kikao cha kwanza cha Bodi walishauri tulifanye kimya kimya hata wake zetu tusiwape taarifa na ndicho kilichofanywa siyo kwamba sikuamini mke wangu kipenzi." Mchungaji alijitetea mbele ya mke wake ambaye alionekana kukerwa na jambo hili.
" Sawa mume wangu lakini ninachokuomba jaribu kumpelekeza mke wake anaweza kujua chochote kwenye hili au hata kueleza mume wake kaenda wapi."
" Nashukuru mke wangu kwa ushauri nitaufanyia kazi kesho asubuhi kabla ya kuanza pilika zangu." Alimjibu akifunika dokumenti zake na kisha kumfuata mke wake kitandani.
JE NINI KITAENDELEA?
KARIBUNI KATIKA SEHEMU YA PILI YA HADITHI HII.