Muswada wa Sheria ya Mapitio ya Katiba: Download na pitia uone kilichomo na usambaze

huo muswada ukifika bungeni ni lazima wabunge wa upinzani wawe makini na pia wajaribu kurob na baadhi ya wabunge wa ccm ili kuweza kuufanyia marekebisho muhimu ili mwisho wa siku tuweze kupata katiba ambayo ni nzuri
 
WANA JF.
Karibuni wote kwenye hili jambo muhimu sana kwa mustakabili wa amani(Uhai )na mali zetu ili mwisho wa siku tuweze kumwepusha OCAMPO kuwa hapa Bongo pamoja na kwamba haitaturudishia uhai wa wapendwa wetu kama yafikia kama kwa wenzetu Kenya na Kwingineko.

I will be back for my Comment.
 

Attachments

  • Tanzania-Constitutional-Review-Bill-2011.pdf
    1.1 MB · Views: 234
Toka mwanzo mwanasheria mkuu jaji Werema alikwisha sema kwamba hakuna haja ya kuandikwa katiba mpya. Sijashangaa ofisi yake kuleta rasimu hii muswada.

Hawa ni aina ya viongozi wa serikali ambao siku za karibuni wamekua wanalalamikiwa kwamba badala ya kumsaidia Rais wamekua wanafanya maamuzi ambayo mwisho wake wanaihabisha serikali. Watanzania wote bila kujali vyama, itikadi, dini, kabila na rangi kama tutabariki uhuni na kutunga Katiba ya hovyo, ni sisi tutakaokuwa wahanga wa upuuzi wetu.

Kwa ndugu zangu wa CCM ni lazima mtambue kwamba hamtatawala Tanzania milele. Mkifanya hila, mkapitisha Katiba isiyofaa, mtambue baada ya miaka michache mtakua majeruhi wa kwanza wa katiba hiyo! Kwa utendaji wa serikali yetu kwa miaka ya karibuni itakuwa ni kichekesho na kutowajibika kama Bunge litakubali kupitisha hiyo rasimu kama ilivyo.
 
Submit your own bill and let the people choose!!.....you can cry all you want,or you
can draft an alternative bill.Facts are facts,we went to the polls and the oppostion lost!
kobello

Kwa nini wewe umekazania kitu hiki who doesnt know that CCM won by God's hand, but here we are not discussing who is the winner we are discussing the tabled bill and its amendments can you add something from there than repeatedly saying Kikwete won Slaa lost.
 
Kutakuwa na public hearing juu ya mswada huu tarehe 07/04/2011 mjini Dodoma .
hivyo kila mmoja anapaswa kuhakikisha kuwa walau mawazo yake yanawekwa ili wale ambao wataweza kwenda kushiriki na hata wabunge wale ambao wanapita humu waweze kuchukua maoni na kuyawasilisha .

Mswada huu ni copy and paste ya ule wa Kenya uliokuwa umekataliwa na wakina Raila mpaka ukapelekea kuwepo kwa chungwa na ndizi , sasa sijui na hapa wanataka wawepo ndizi na chungwa ama nini wanataka .ukitaka kuupata wa Kenya nenda google na utaupata unaitwa constitution review act .
 
Maoni yangu kuhusu muswada wa kutungwa kwa sheria ya mabadiliko ya katiba ya Nchi ya mwaka 2011.

THE CONSTITUTIONAL REVIEW ACT, 2011.

  1. Kifungu cha 1 (2) kinasema kuwa mswada huu utakuwa sheria na kuanza kutumika rasmi tarehe 01/06/2011 …..hii maana yake ni kuwa serikali tayari imeshaamua kuwa ni lazima mswada huu utapitishwa na Bunge la mwezi April bila kufanyiwa marekebisho na ndio maana wameweka muda wa kuanza kutumika kwa muswada huu .Je? Bunge likikataa kuupitisha mswada huu serikali8 itachukua hatua gani kuhakikisha kuwa unaanza kutumika tarehe tajwa? Mbona miswada mingine huwa inaandikwa tuu kuwa utaanza kutumika mara baada ya kupitishwa na buinge na kusainiwa na rais?
2. Kifungu cha 3 tafsiri ya neno katiba ni pamoja na "for the purposes of this Act it includes amendments to an existing constitution" hapa maana yake ni kuwa sheria hii sio kwamba inaenda kusababisha kuandikwa upya kwa katiba bali ni kwenda kufanyia marekebisho katiba iliyopo…..je ? hili ni lengo letu ?

3. Kifungu cha 5 kinampa madaraka rais katika kuunda tume ya kusimamia mchakato wa katiba …. Ni kwa nini itungwe sheria hii wakati katiba imempa mamlaka rais kuunda tume ya aina hiyo? Yafaa tume hii wajumbe wake wakawa wanapendekezwa kutokana na wadau mbalimbali na hivyo uteuzi ukafanywa miongoni mwa majina yaliyopendekezwa na sio kuyaachia mamlaka hiyo kwa mtu mmoja kuteua wajumbe kwa kushauriana na watu wengine wawili. Ni heri hata bunge likapewa mamlaka ya kuteua wajumbe ili rais asiwe na mamlaka ya kuingilia mchakato husika .

4. Kifungu cha 6 (1) kinasema kuwa wajumbe wa tume watateuliwa kwa uwiano wa nusu kutoka Zanzibar na nusu Bara ……..hii sio sawa hata kidogo kwani kutokana na idadi ya watu ni ukweli usiopingika kuwa wajumbe kutoka bara watakuwa na uwiano wa kuwakilisha watu wengi kuliko wale wa upande wa Zanzibar na hata itakapofikia wajumbe wa tume wanataka kufanya maamuzi kwa njia ya kura kwenye jambo ambalo wao wenyewe wameshindwa kuafikiana na haswa likiwa ni jambo ambalo linahusu upande mmoja wa muungano hakika hapatakuwa na uamuzi.Eneo hili likiachwa kama lilivyo litaifanya tume ishindwe kufanya kazi yake .

5. Kifungu cha 6 (3) (b) kinazungumzia watu ambao wako kwenye vyombo vya usalama lakini hakizungumzii chochote kuhusiana na watu ambao wamekuwa ni wastaafu wa vyombo hivyo , kwani kwa muda mrefu serikali imekuwa na utamaduni wa kuteua wastaafu wa vyombo hivi kwenye tume mbalimbali hapa nchini.

6. Pia kifungu hicho hicho cha 6 (3) hakizungumzii chochote kuhusu uwapo wa wajumbe ambao wamekuwa wakituhumiwa kwa mambo mbalimbali kiama mafisadi n.k kuwa miongoni mwa wajuimbe wa tume husika , kwani wapo wanasheria ambao kwa kipiondi kirefu wamekuwa wakijihusisha na vuitendo vya kukosa uadilifu ila hawajashitakiwa , sasa wakiwepo kwenye tume itakuwa sio sahihi.pawepo na kifungu kinachoonyesha kuwa wajumbe wa tume wasiwe ni watui ambao jamii iliwahi ama imewatilia mashaka katika utendaji kazi wao.

7. Kifungu cha 7 (1) a,b, na c kinatamka kuwepo kwa mwenyekiti na makamu mwenyekiti lakini muswada hauonyeshi ni nani ambaye anahusika na uteuzi wa watu hao na haswa ikizingatiwa kuwa wajumbe wa tume watakuwa nusu kutoka kila upande wa Muungano hivyo zoezi la kupiga kura litakuwa gumu ama lisilowezekana kabisa.Na kama ni kuwa rais ndio atateua mwenyekiti na makamu mwenyekiti itakuwa sio sahihi kwani yafaa wajumbe wa tume wakaachiwa jukumu la kuteua mwenyekiti na makamu mwenyekiti wao.

Pia kifungu hiki hakitamki sifa za Mwenyekiti na Makamu mwenyekiti wa tume hii badala yake zinatajwa tuu sifa za kuwa ama wazaliwa wa pandfe za Muungano , ingefaa sifa za Mwenyekiti na Makamu mwenyekiti zikawa safa na sifa anazopaswa kuwa nazo Jaji wa mahakama ya Rufani .

8. Kifungu cha 8 (1) kinazungumzia juu ya hadidu za rejea ambazo mwenye mamlaka ya kuzitoa ni rais pekee ………tume hii haitaweza kuwa huru na badala yake itaenda kuwa tume ya rais kama tume nyingine zilizopita za Jaji Nyalali na Kisanga .Hadidu rejea yafaa zikatolewa na Bunge kwani ni chombo kinachowakilisha wananchi.

9. Kifungu cha 9 (2) na vifungu vidogo vya (a) –(j) vimeitaka tume bila kujali mawazo ya wananchi kuhakikisha kuwa hakuna jambo litakalobadilishwa kwenye mambo yaliyotajwa kama vile Muungano,Mamlaka ya rais,uwepo wa serikali mbili n.k. swali la kujiuliza hapa ni kuwa je? Tume hii inaenda kukusanya mawazo ya wananchi ama tayari imeshakuwa na msimamo juu ya nini ambacho wananchi wanapaswa kukisema au hata wakisema mawazo yao hayatazingatiwa? Yafaa wananchi wakapewa uhuru na tume ikachukua mawazo ya wananchi kwa uhuru stahiki bila kuingiliwa ama kupewa tahadhari kama ambavyo imetakiwa kufanya.

10. Kifungu cha 10 kinazungumzia mamlaka ya tume na kusema kuwa itakuwa huru…….swali la kujiuliza hapa ni kuwa hii tume itakuwa huru kutoka kwa nani wakati inawajibika kwa Rais ambaye ndio anaiteua na kuipa hadidu za rejea? Na pia wameshapangiwa majukumu yao ?

11. Kifungu cha 13 (1),(2),(3),(4) na (5) kinataja uwepo wa secretariat , ila la kushangaza ni kuwa wajumbe wa tume idadi yao imewekwa na sheria ila wajumbe wa secretariat sheria haikutaja idadi yao na wala hata jinsi wanavyopaswa kupatikana badala yake wajumbe wa secretariat wanaenda kuwa ni maofisa wa serikali. Kuruhusu kifungu kama hiki ni kumpa mamlaka waziri mwenye dhamana kuteuwa wajumbe wa secretariat hata kama ni makada sifa pekee ni kuwa maofisa wa serikali 13(5).

12. Kifungu cha 14 (2) kinazungumzia masilahi ya wajumbe wa tume na wale wa Secretariat kuwa ni kwa kadiri waziri wa sheria na katiba atakavyoamua ……jambo hili sio sawa kwani yafaa malipo ya wajumbe hawa yakawa wazi kwani wanaenda kufanya kazi ya wananchi , ingefaa sheria ikatamka kuwa wajumbe hawa posho yao itakuwa sawa na posho ya mbunge kwa siku ama posho ya Jaji wa mahakama kuu n.k ili wananchi wawezse kufahamu tume hii italigharimu taifa kiasi gani cha fedha.

13. Kifungu cha 15 kinawapa kinga wajumbe wa tume na wale wa Secretariat , ingefaa kinga hii ikawa ni pamoja na Rais kutokuwa na mamlaka ya kuwafukuza kazi bila kufanyika kwa utaratibu maalum wa kuwafukuza kazi (ingefaa wakalindwa na sheria na haswa sheria inayowapa kinga majaji na utaratibu mzima wa kuwafukuza).

14. Kifungu cha 17(f) kinasema kuwa tume itaandaa na kuwasilisha taarifa yake kwenye vyombo vya kikatiba kama ambavyo hadidu rejea zitasema , wakati huo huo kifungu cha 16(1) nkinasema kuwa tume itawasilisha taarifa yake kwa Rais na hapo ndipo ataiwasilisha kwa rais wa Zanzibar na baadae atamwagiza waziri kuiwasilisha kwenye Bunge la katiba . kwa hiyo hapa ni kujichanganya kwa vifungu hivi .
15. Kifungu cha 18 (2) (a) tume itapaswa kuwa na muhutasari wa maoni ya wananchi----- swali la kujiuliza hapa ni kwanini watumie muhutasari na sio maoni yote ya wananchi? Wakati nyaraka nyingine ambazo tume inapaswa kuwa nazo ni pamoja na 2(b) Mapendekezo ya kamati kuu ya CCM YA Mabadiliko ya katiba ya mwaka 1977 ? mbona tume isitumie pia nyaraka za vyama vingine vya Siasa ? kwanini nyaraka za CCM Pekee?zitumiwe na tume ? lengo lake nini?wakati nyaraka hiyo ndiyo ilipelekea kuwepo kwa katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977?

16. Kifungu cha 19 (2) kinasema kuwa "the draft consititution Bill shall form an annex to the report of the commission" je lengo la tume ni kuandaa bill ama nini? Nini wanapaswa kuandaa kama main document?

17. Kifungu cha 27(1) kuhusu tume ya taifa ya uchaguzi kusimamia zoezi la kura za maoni , jambo hilo sio sahihi kwani kutakuwa na mgongano (conflict of interest ) kwani tume ni miongoni mwa walalamikiwa katika kusimamia chaguzi hivyo kuipa madaraka ya kusimamia tena kura za maoni ni kuendeleza malalamiko ambayo yapo miongoni mwa jamii na kulifanya zoezi kutokuwa smooth.

18. Kifungu 28 (2) kinavizuia vyama vya siasa katika kufanya kampeni wakati wa kura za maoni juu ya katiba mpya na ni Tume pekee ambayo imeteuliwa na Rais ndio inapewa mamlaka ya kufanya kampeni hizo za kuhamasisha wananchi kuunga ama kutokuunga mkono katiba mpya .Jambo hili halipaswi kuwepo kwenye mswada huu kwani linaelekea kwenda kusababisha vurugu na pia kuvinyima vyama vya siasa haki zao za kimsingi katika kufanya kampeni kwenye masuala mbalimbali.Iweje tume iliyoundwa na rais iweze kuaminiwa kuwa inafanya kazi vyema kuliko vyama vya siasa?vyama hivi vimesajiliwa na hivyo yafaa vikapewa fursa ya kufanya kampeni kama ambavyo wenzetu wa Nchi nyingine huwa wanafanya mfano Kenya, Zanzibar katika mabadiliko ya 10 ya katiba yao n.k.
Iko wapi haki na uhuru wa kutoa maoni?

19. Kifungu cha 28(4) kinataja mtu anayeitwa "Returning officer" na amepewa madaraka na mamlaka makubwa ya kuijulisha jamii juu ya kura za maoni .huyu anapatikana wapi na mbona hata kwenye interpretation ya sheria hii hajatajwa popote ? huyu ni miongoni mwa wajumbe wa tume ama anapatikana wapi?

20. Kifungu cha 30 , tume ya uchaguzi inapewa mamlaka ya kusimamia zoezi la kura za maoni …wakati tume hiyo haina watendaji kwenye ngazi za mikoa, wilaya ,kata, vijiji,mitaa na vitongoji……..wakati huo huo walioko huko ni wateule wa Rais yaani aliyeteua tume ndio huyo huyo anaenda kusimamia uchaguzi husika . kiundwe chombo huru kwa ajili ya kusimamia zoezi la kura na tume ibaki na majuu7kumu yake ya kusimamia uchaguzi mkuu.

Nimeyaona hayo kwa leo ila nitaendelea kusoma na kupitia nyaraka mbalimbali kwa ajili ya rejea ili kujua jinsi ambavyo mfumo huu umeweza kusaidia ama kutosaidia upatikanaji wa katiba mpya katika nchi mbalimbali na haswa ikizingatiwa kuwa mfumo huu wa tume za Rais umeshafanyika mara nyingi hapa nchini bila mafanikio yeyote.
 
Ukisoma Section 20.1,2 &3 ya huu Mswada kwa kweli utaona uhalisia wa huu Mswada asilimia mia Moja.Kwa hakika uundwaji wa hii Tume hauna tofauti yoyote na Tume zilizokwisha pita.
Ni imani yangu kuwa Chadema na Wanaharakati wengine watapasa sauti kwa sasa ili huu mswada usiende Bungeni Kupigwa Muhuri.Hawa watu hawana AIBU (CCM) kwa uwingi wao Bungeni wataupitisha kwa masilahi yao.Lakini na pata tumaini kuwa iko siku Nguvu ya Umma itafanya Kazi kama si ndani ya Mchato huu!

Mswada huu haufaia kwa Karibu 65%.Maeneo yafuatayo kwa Maoni yangu yana mapungu na yanahitaji marakebisho.
Kichwa cha Mswada na vifungu vifuatavyo. 5, 6;1, 7;1, 8;1, 9;2, 10,13,14;1,16;1,2&3, 20;1,2&3 ,21;1,2,&3,22;2,23;3&,24,26,27,28;2&3 and 31;1&2.
 
Asante Kiranja.

Kuna vitu nimeviona kwenye hiyo bill itabidi nichangie hata kama sintasikika nitajiridhisha nilisema endapo mtoto wangu wa miaka miwili atakaponiuliza hapo baadaye nitajitetea niliwaambia.

Kifungu 12 A person shall cease to be a member of commission upon.....
(a) Death..........hii sawa
(b) resignation...........sawa lakini isiwe kwa kulazimishwa kukubaliana na maelekezo ya rais
(c) inability by reason of health..........kwa nini wameweka sababu moja je kama ataonekana ana mapungufufu mengine kama busara na uwezo wa ku-judge mambo itakuwaje
(d) removal by misconduct............sawa lakini iwe fair maana definition ya misconduct ni pana sana.

Kifungu 28. kinazuia kufanya kampeni..........hii si haki hata kidogo katiba ni yetu sote kwa nini tukatazwe kufanya kampeni, tuliona Kenya kulikuwa na makundi mawili Orange na Banana sisi tuna YES na NO sasa hiyo Tume iliyopewa mamlaka ya kufanya kampeni itakuwa upande gani i think this is horrible mistake kwenye huu muswada.

Mwisho rais amepewa mamlaka makubwa sana kwenye swala hili utadhani hii katiba ataondika nayo atakapomaliza muda wake, yeye ni kila kitu muswada mzima umejaa neno rais why? nilitegemea ujae neno 'wananchi' kama utapitishwa baada ya miaka 10 tutarudi kwenye wimbo ule ule katiba haikushirikisha wananchi. Natoa rai kwa walioandika na rais mwenyewe aone kuwa kuna tatizo la msingi hapo.

Kama itapita kama ilivyo nitaanza kampeni ya kuiita Katiba ya Kikwete si katiba ya Tanzania.
 
Yani nchi hakuna watu wenye uchungu na nchii hii. Walioanda hii bill ni kama hawajasoma au hawajui umuhimu wakatiba. Mwenyekiti wa kijiji,katibu taarafa si wanachama wa vyama hao? Au hapo hapo wanakataza kuwa wanasiasa hawatakiwa kushiriki?????. Kwa ujumla inamapungufu mengi sana ni bill iliyokaa kiubabe zaidi na sio kuwap watanzania haki yao ya kuanda katiba yao.
 
Katika pita pita yangu nimekutana na maoni ya huyu Bwana nimependa baadhi maana yameguzia maeneo yanayonipa wasiwasi mkubwa.
Soma hapa chini.
1. Dear Zitto,
Thanks for sharing this Government Notice about the Tz Prospective Constitution.
The following are my observation as far as this Bill is concerned, which are directed to you member(s) of the Parliament (representatives of Tanzanians) for actions.
1. The heading of the Bill is wrong. Since the needed document is the New Constitution, we don't I personally don't want it read as "The Constitutional Review Act, 2011; rather reads The New Constitutional Act, 2011. Therefore, all phrases in the document with such "constitutional review" appearing must be corrected to reflect the reality;
2.PART II of the Bill, roman (j) has the same problem of …constitutional review…, (l) is not clear when when saying.. legal mechanism for the President to Constitute a Constituent Assembly. What is the legal implication of this, is there any legitimacy for him?;
3. PART III, 5. of the Bill, "The President may….., Where is the legitimacy for Mr. President to own such mandate? An independent body is needed to be en-charge of the new constitution process. This independent body will possess the legitimacy if formulated by the Parliament and not the President (refer to the past experience of such committees turned to be useless);
4. 6 (1) The president has got no any legitimacy to appoint such important committee as conflict of interest is an obvious to affect the composition. The task remains in the mandate of the house of representatives (Parliament) and not otherwise, (2) this also does not apply following change of (1);
5. 6 (2) (e), the President has no mandate to set required criteria on behalf of the public (Tanzanians). It remains the task of the Parliament as well;
6. 7(1) about composition of the commission, it's totally wrong idea. First of all members must be Parliament's appointees. Hence, every process involved in setting criteria is posed to the House of representatives not the President of the United Republic of Tanzania;
7. 8 (1) is not a responsibility of Mr. President to set and issue Terms of Reference (ToRs) for the commission responsible for the new constitution. The Parliament in consultation with different stakeholders possess this mandate, 8 (2) there must be time limit for the commission to pursue this process. Hence, it should not be left an open task without time-frame, 8 (3) applies only and only if the Parliament formulates ToRs;
8. 9 (2) Is not valid unless the Parliament is given such mandate over the New constitution process of not only passing this Bill but also overseeing the whole process until we finalize our constitution;
9. 10 Reflect no any independence of the commission if formulated under the Presidential Office (we already seen the passed commission, Judge Kisanga & his peers);
10. 13 we do not need Presidential Appointed members of the commission because of weak institutional framework in the government, conflict of interest, and the passed experiences;
11. 14 (1) As said earlier, we do not need a constitutional review, hence this phrase must read ..new constitution..;
12. 16 (1) we do not want the passed happen again, for the commission submitting report to the President, let the Parliament handle everything, (2) & (3) No mandate to Mr. President required insofar as the new constitution process is concerned (Conflict of interest, poor passed experience, and weak government institutions centered to the mandate of President's Office).

Once more, Honorable Zitto, at end of a day, this Bill will come to the House for discussion, please mobilize all patriotic members to get to know all observations, which if improved on this Bill will foster for Tanzania having such a new constitution opening up opportunities for the development process of our people. I understand also that, there are other observations, which if combined with my little one will definitely strengthen your discussion ground during the session.
I beg to submit.

Emmanuel D. Chonza
March 30, 2011 at 6:13 PM
 
Asante sana mkuu kiranja kwa kutupa analysis ya mswada huu. Naomba unipm ili tuweze kuweka sawa hzo comments na tuzifikishe mahali stahiki.
 
We realy need it for in depth critical and constructive analysis!!. Mwenye nao atupatie jamani!!. Au nao ni Siri hautakiwi kujulikana!!. Manake hii nchi haichelewi kusema muswada ni siri!!

Journalists where are you?? Huu muswada mpaka sasa ulitakiwa uwe umeshatolewa kwenye magazeti, kila mwananchi auone!! This is all about our destiny!!
 
Mnajua ni kwa nini wanazungumzia wenyeviti wa vijiji?
Mbona sio madiwani?

ntawatumia matokeo ya vijiji 2009 then mtajua ni CCM i8n action.
 
Wakati wa watanzania kuamka ni sasa, kama kuna mahali tulizembea wasomi, wakulima na wafanyakazi wa nchi hii basi hii ni nafasi yetu kuonyesha mshikamano na kuilazimisha kwa hoja au ikibidi nguvu ya umma wawaachie wananchi maamuzi katika mchakato wa uundwaji wa katiba
 
Hiki ndicho maana yake fanya analysis ya hizo data japo sio za kweli ni zile zilizowasilishwa bungeni na waziri wa TAMISEMI Celina Kombani.

POSTIONPolitical PartiesCCMCHADEMACHAUSTACUFNCCR MageuziTLPUMDUPDPUDPPPT MaendeleoSAUTADEADPJAHAZI ASILIANLDNRADEMOKRASIA MAKINITOTAL /GENDER%SAUVILLAGE CHAIRPERSONTotal98000289104073845006800000000M96272851040338450068000000001047698.3F17340400000000000001811.7MEMBERS OF VILLAGE COUNCILTotal113631361610653204211475812690150010020M10553033101014810396419116580010020115229F81013065510251056711320000000010053

naona zipo kwenye excell zimegoma ntaziweka baada ya kuzibadilisha .
 
kwa mfano kusema kuhoji tume ya iliyoundwa na rais ni kosa la jinai amabayo azabu yake ni jela miaka mbili au failni ya mil. 5 au vote pamoja haina tofauti kabisa na ile sharia ya kiarabu ya kuadhibu kwa kupigwa mawe hadi kufa ukienda kinyume na uislamu.

kwa ndoto niliyooteshwa leo ni kwuwa huu mswaada kama wakristo wataukubali upite, basi watakuwa wahanga wa sharia kali za kiislamu na watapata mateso makubwa kutoka kwa hawa waislamu wa pwani.

na huu muswaada ukipita tu, basi tzazania haitakwepa kitanzaia cha kujiunga na OIC na kmakhakama za Kadhi ambazo huwa ni kero kubwa kwa jamii ya wakristo duniania kokote.

nawakilisha.
 
Mnajua ni kwa nini wanazungumzia wenyeviti wa vijiji?
Mbona sio madiwani?

ntawatumia matokeo ya vijiji 2009 then mtajua ni CCM i8n action.

Nanusa harufu ya damu damu vile, tena sio mbali sana toka hapa tulipo, halafu naona kama watu wanajitayarisha kwenda kuishi ng'ambo, wengine Ukonga, wengine wakihojiwa na O'Campo alimradi Tanzania imeshakuwa si salama tena,

Hawa watawala wetu wangekuwa na akili ndogo tu ambayo hata mwanangu anayo basi upenyo huu ndio wangetumia kuweka mambo sawa kwa maisha yao ya baadaye lakini ndio kwanza wanajichimbia...kweli sikio la kufa halisikii dawa
 
kwa mfano kusema kuhoji tume ya iliyoundwa na rais ni kosa la jinai amabayo azabu yake ni jela miaka mbili au failni ya mil. 5 au vote pamoja haina tofauti kabisa na ile sharia ya kiarabu ya kuadhibu kwa kupigwa mawe hadi kufa ukienda kinyume na uislamu.

kwa ndoto niliyooteshwa leo ni kwuwa huu mswaada kama wakristo wataukubali upite, basi watakuwa wahanga wa sharia kali za kiislamu na watapata mateso makubwa kutoka kwa hawa waislamu wa pwani.

na huu muswaada ukipita tu, basi tzazania haitakwepa kitanzaia cha kujiunga na OIC na kmakhakama za Kadhi ambazo huwa ni kero kubwa kwa jamii ya wakristo duniania kokote.

nawakilisha.

kama uvccm pwani walivo laumiwa na uvccm bara. watu wa pwani ni hatari sana kwa mstakabali wa taifa.
 
Back
Top Bottom