Muswada wa sheria ya madaktari waondolewa bungeni

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
20,388
24,947
Dodoma.


Serikali imeuondoa bungeni Muswada wa Sheria ya Madaktari, Madaktari wa Meno na Wataalamu wa Afya Shirikishi wa mwaka 2016 huku Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Khamis Kigwangallah akisema duniani kote madaktari wasaidizi haitwi hivyo.


Uamuzi wa kuondoa muswada huo ambao tayari ulikuwa umepangwa katika shughuli za Bunge ulitangazwa jana na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson baada ya kipindi cha maswali namajibu.“Mheshimiwa Spika amepokea maombi ya Serikali kuhusu kuondoa muswada huo kwa sasa,” alisema Dk Tulia bila kutaja sababu ya kuondolewa na kuwafanya baadhi ya wabunge kupiga makofi.


Katika vikao vya kupokea maoni ya wadau wa sekta ya afya cha Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Chama chaMadaktari Wasaidizi, Madaktari Wasaidizi wa Meno, Tabibu na Tabibu Wasaidizi, (AMEPT) kiliwasilisha mapendekezo wakitaka kutambuliwa katika sheria hiyo kama madaktari wasaidizi.


Chama hicho kilitaka waondolewe katika kundi la wataalamu wa afya shirikishi nakutambulika kama madaktari kwa sababu wote wana ujuzi na wanawahudumia wagonjwa kama madaktari wenye shahada.

Akizungumza katika Viwanja vya Bunge, Waziri wa wizara hiyo, Ummy Mwalimu alisema sababu kubwa ya kuuondoa muswada huo bungeni ni kupata muda zaidi wa kushauriana na wadau kuhusu sheria inayopendekezwa. “Umetokea upotoshaji kwamba muswada huu unakusudia kuwafuta madaktari wasaidizi. Hicho si kitu ambacho kipo,” alisema.“


Serikali tumetaka kusisitiza kwamba tunatambua na kuheshimu kazi zinazofanywa na madaktari wasaidizi ambao kwa kiasi kikubwa wapo vijijini.”Ummy alisema hawatasajiliwa kama madaktari kwasababu daktari kwa mujibu wa sheria ni mtu mwenye shahada na kwamba, madaktari wasaidizi wana elimu ya stashahada ya juu.


Chanzo : Mwananchi Online
 
Serikali ya kukurupuka, ona sasa kila kitu kinaenda mwendokasi kama gari lisilo na dereva makini
 
Waziri wa afya nimemdharau sana,kwa kauli juu ya Madaktari wasaidizi, eti hawapo rasmi na hats mtaala wa kada yao hakuna....Ni aibu kubwa.

Hao madaktari wasaidizi ndo waliojaa kwenye karibu hospitali zote za mikoa,wilaya hadi kwe vituo vya afya nchini.Ndio wanafanya kazi zote huko za tiba mpaka upasuaji.
Wanaposimama majukwaani kujisifia kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi hao anaowadharau na kujifanya eti hawatambui ndio wanaofanikisha hayo.

Waziri mzima ameshindwa kujishughulisha japo kidogo kusoma makabrasha ofisini kwake yanayohusu kada hiyo,ameshindwa hats kuipitia sharia iliyoanzisha kada hiyo??
Anasahau wizara take ndo inaendesha mafunzo ya madaktari wasaidizi,inaandaa mitihani,inawapa Vyeti.Anashindwa kujua kuwa wizara yake inawasajili na kuwapa leseni za kufanyia kazi hiyo....MTU wa namna hii ndo tumemkabidhi wizara nyeti ya afya.
 
Wizara hii imepatwa. nilidhani wangejipanga kutumia muda kama huo kupeleka miswada ya kuboresha sekta upande wa huduma na wala sio miswada ya kutambuana kwa majina. Nawashauri warejee maoni ya wananchi kuhusu kulegalega kwa huduma za afya hapa nchini. kama anawaogopa wabunge watampa za uso kwa kushindwa kutimiza malengo ya kupunguza vifo basi ni vema akajitoa kuhudumu kwenye wizara hiyo
 
Kama wanataka kuitwa Dr si waende wakasome medicine si miaka 5 tu.

Hata hao madaktari wasaidizi wamesoma medicine(clinical medicine) tena kwa hiyo hiyo miaka mi5;mitatu ya awali STASHAHADA,na baadae miwili STASHAHADA ya juu(tena ni baada ya kufanya kazi kwa muda usiopungua miaka mi3)

Kozi/mafunzo yao ni ya vitendo zaidi(rejea mtaala wao)...hivyo hiyo imewafanya wawe fit zaidi.
Kumbuka kuwa wamepitia mkondo ule ule wanaopitia hao wa shahada,na wanafundishwa na madaktari bingwa,na vyuo vyao vipo kwenye hospitali za rufaa.

Na tutambue kuwa hawa madaktari wasaidizi, ndo waliopo huko peripheral wakiwahudumia Watanzania wenzetu miaka nenda rudi,bila shaka wengi wetu tumepita mikononi mwao kuanzia mimba hadi hapa tulipofikia.

Tuache kumpotosha waziri,tutaharibu sekta ya afya nchini.
 
Back
Top Bottom