jouneGwalu
JF-Expert Member
- Apr 11, 2011
- 2,687
- 1,780
Je unazungumziaje tabia za watumishi wengi katika manunuzi kutokuwa waadilifu. Tatizo ni nini? Bila 10% kazi hazifanyiki!
kwa Tanzania procurement ni taaluma mpya sana, hvyo wataalamu lilikuwa tatizo hapo nyuma kidogo!
Hivyo watendaji hawa wengi walikuwa wanasimamia wasichokijua kwa nafasi kubwa, hivyo tatizo kubwa lilikuwa ni upungufu wa ujuzi katika taaluma na miiko yake!
Suala la 10% nakuhakikishia halikwepeki mkuu wangu, sababu kuna wakati linakuja katika sura ya zawadi. Hebu we piga picha kama mfano wewe ni Supplier umeshiriki bid ambapo mpo suppliers zaidi 20 hvi, na hyo kazi ni kama ya Tshs milions of hundred, afu ukashinda katika haki (na inatokea kwa asilimia kubwa tu kushinda kwa haki) je utashindwa kuwapa chochote wale members wa bodi ya tenda??
Hayo ndio mazingira ya utendaji, pia kuna suala la mahusiano na supplier kitaaluma kabisa hili na linafaida zake, na haitazuilika kupata mkono toka kwa supplier sababu naye anambinu zaidi za kutaka kukushika katika kipindi cha mkataba!
Muhimu zaidi ni kuwa na watumishi ambao wenye uwezo kitaaluma. Toka mwaka juzi serikali ilianza kwa kasi kidogo kuajiri wataalamu wa idara hii japo mwaka jana naona zoezi limeingia nyongo kidogo, hvyo bado halmashauri nyingi sana hazina wataalamu kwenye eneo hili, achilia mbali kwenye mawizara na idara nyingine za umma!