Muswada wa marekebisho ya sheria ya manunuzi ya umma 2011 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muswada wa marekebisho ya sheria ya manunuzi ya umma 2011

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by lukindo, Mar 15, 2011.

 1. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,892
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  Nawasalimuni wana jamvi,

  Nimesoma kwenye gazeti linalochaipshwa Nairobi, The East African la juma hili juu ya nia ya serikari (mafisadi!!!?) kutaka kubadilisha sheria ya manunuzi ya umma ili kuweza kununua mitambo ya DOWANS, pia habari hii imekaririwa na baadhi ya magazeti ya hapa nyumbani jana na leo na hata ndani ya JF imejadiliwa.

  Nahisi tumeanza kuelekea kuzimu baada ya kuharibikiwa maana litakuwa moja ya makosa ya kihistoria endapo hilo litatekelezwa. Kwa maana hatujui nani watakuwa serikarini kesho na keshokutwa!

  Labda kwa kukumbushana, hii sheria imewekwa kwa nia ya kupata kitu kinaitwa "Value for Money". Na imesisitizwa mitambo au vitu vipya kwa sababu ya kuepuka rushwa zilizokithiri serikarini kama wote tunavyojua. Maana kwenye vitu vipya hakuna uongo mwingi!

  Jamani tujiulize,
  1. Ni akina nani hao wanaamua kuturudisha nyuma???
  2. Je, PPRA mtashuhudia hili likitendeka au mtafanya lolote!?
  3. Ni kweli mafisadi wamefikia kiasi hiki cha ujasiri??


  Ni kweli tukubaliane kama nchi sheria kubadilishwa ili kukidhi matakwa ya wachache?

  Nawakilisha
   
 2. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,014
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Hili badiliko la sheria haliepukiki. Tujiulize serikali ni nani. Tujiulize Dowans ni nani. Majibu ya maswali haya yakipatikana utaweza kujua kuwa badiliko ni inevitable.
  Sheria mpya is likely to be in place temporarily, baada ya manunuzi ya Dowans kufanyika then we go back to old sweet days. Mission achieved, a reason to toast with a glass of wine. Haya ndo maisha bora ktk vision ya mkwere.
   
 3. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #3
  Mar 15, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Bunge liliahirishwa kule Dodoma lakini kila siku vikao vya Bunge vinaendelea jijini Dar es Salaam. Vingi ya vikao hivyo ni vya kutetea DOWANS kwa gharama yeyote mfano Mkataba wa muda mfupi ufungwe kuwashwa mtambo wa BOWANS, sheria ya manunuzi ibadilishwe ili mitambo ya DOWANS inunuliwe n.k

  Kwa kuwa Raisi yuko juu ya sheria si aamuru tuu mitambo ya DOWANS inunuliwe na awe tayari kutetea uamuzi wake badala ya kubadili sheria?
   
 4. Khakha

  Khakha JF-Expert Member

  #4
  Mar 16, 2011
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 2,983
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  WADAU WA JF, HILI JAMBO LA KUREKEBISHA SHERIA KWA SABABU YA RA NA EL KUWABEBA BY KUNUNUA MITAMBO YAO YA DOWANS LIKOJE JAMANI? NCHI YETU YAELEKEA WAPI? NIJUAVYO DOLA LAZIMA INUNUE MALI AMBAZO NI BRAND NEW ILI ZI LAST LONG.:angry:
   
 5. M

  Mwamatandala Member

  #5
  Mar 28, 2011
  Joined: Jul 17, 2009
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Leo nimehudhuria ktk kikao kilichofanyika karimjee hall kupokea maoni ya wadau kuhusu marekebisho ya sheria ya manunuzi ya umma itakayoruhusu ununuzi wa bidhaa zilizotumika(chakavu) kwa ajili shughuli na mahitaji mbalimbali ya serikali.

  Hii imekuja baada ya mitambo chakavu ya DOWANS kushindwa kuruhusiwa kuendelea kuizalishia umeme tanesco kutokana na kutokizi masharti ya sheria hii.

  Kwa idadi kubwa ya wajumbe waliochangia,wamepinga vikali marekebisho hayo wakidai kwamba hayana tija na yatatoa mwanya wa ununuzi wa bidhaa zilizo chini ya kiwango na kupelekea matumizi mabaya ya fedha za umma. Kikao hicho kiliendeshwa na kamati ya bunge ya fedha na uchumi.
   
 6. eliakeem

  eliakeem JF-Expert Member

  #6
  Mar 28, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 2,937
  Likes Received: 1,034
  Trophy Points: 280
  Kumbe WIKIleaks iliongea ukweli.........ilisema kuna mafisadi papa ambayo yana ushawishi na uvutano mkubwa sana katika nchi hii hivi kwamba SHERIA ZINAWEZA KUBADILISHWA KWA MANUFAA YAO.

  Hii sheria ya manunuzi inabadilishwa kwa minajiri ya kununua mitambo chakavu ya ROSTAM AZIZ. KWA HIYO HAPO KARIMJEE MNAJADILI JINSI YA KUWEZA KUNUNUA MITAMBO YA ROSTAM.
   
 7. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #7
  Mar 28, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mbona taarifa tunazo kuwa CHADEMA ilituma rundo la watu kwenda kwenye huo mkutano na hao hao ndio walio kataa !
   
 8. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #8
  Mar 28, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,635
  Trophy Points: 280
  Mbona hata wewe ulikuwepo !!!!!!.
   
 9. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #9
  Mar 28, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Uliniona ?
   
 10. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #10
  Mar 28, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,892
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  Nimeona tangazo la hiyo meeting jana kwenye gazeti la Mwananchi nikasikitika sana! Ajabu ni kuwa sheria muhimu kama hiyo unaiorganize kana kwamba Karimjee ndio procurement experts and professionals wote wanapoishi.

  Tatizo Viongozi wetu kwa sasa wamelewa madaraka na wanadhani kuwa kila kitu ni kutengeneza ulaji na upinzani wowote ni kuwazuia wasile, wakumbuke kuwa vingine ni kwa maslai ya wote -sisi na wao!

  Endapo watabadilisha hii sheria na hii mijizi iliyojaa kwenye sekta ya umma, miaka 5 tu itatosha kuaccount wizi unaolingana na ujenzi wa miaka 45 iliyopita!
   
 11. S

  SUTU BUTUGURI Member

  #11
  Mar 28, 2011
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Taanzania, tanzania, ningekupenda kwa moyo wote ... kama ungekuwa na viongozi wanaokupenda. Lakini duuuuuuuu, viongozi wankuingilia kinyume na maumbile, mimi nitakupendaje? Inasikitisha, sheria kubadilishwa ili serikali iweze kununua vitu CHAKAVU. Ama kweli tumekwisha ...
   
 12. F

  Froida JF-Expert Member

  #12
  Mar 28, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,903
  Likes Received: 1,330
  Trophy Points: 280
  Duh mtume wangu naelewa lakini kwa nini unauchungu namna hii tukaze boot kuwahakikisha viongozi wanahakikisha wanatumia maumbile yanayopaswa kinyume cha hapo wakubali kupambana na NGUVU YA UMMA
   
 13. M

  Mwamatandala Member

  #13
  Mar 28, 2011
  Joined: Jul 17, 2009
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ni jambo la kusikitisha hususani ktk wakati huu ambapo taifa linakabiliwa na changamoto nyingi.
  Nilichojifunza ktk kikao kile ni kwamba wanakamilisha ratiba tu,lakini tayari nguvu ya mafisadi imewazidi wazalendo na hatimaye mabadiliko hayo haramu yatapitishwa bungeni na kuwa sheria.
  Lol!!
   
 14. JUST

  JUST JF-Expert Member

  #14
  Mar 28, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Time will tell

  huu ni msaada kwa wauza spare wa ilala, lancruiser vx, gx, v8,prado, hard top zikiharibika used zipo kibao pale ilala, na wewe ukiwa na meza iliyochoka nyumbani kwako unauzia halmashuri ya unapoishi,

  kwa mfano mdogo kama huo ni kwamba huu ndio ufisadi utakaovunja rekodi ya ufisadi wowote ule uliowahi kufanyika tz
   
 15. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #15
  Mar 28, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Inavyoelekea R.A anaendelea kutesa, hata mahakama ya kimataifa iliyompa fidia ya shs 94 bilioni ilitamka wazi kwamba bwana huyo anazo nguvu nyingi nchini kiasi kwamba sheria zinafanyiwa marekebisho kukidhi matakwa yake! Hii inaunga mkono husemi wa baba wa taifa unao rejerewa TBC mara kwa mara ya kuwa serikali corrupt zinatumikishwa na walionacho.
   
 16. k

  kimboka one JF-Expert Member

  #16
  Nov 10, 2011
  Joined: Jan 23, 2010
  Messages: 734
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  wabunge makini plz zuieni huo wizi,hakuna ufisadi mkubwa kama kuruhusu tanzania kununua vitu chakavu au used.km sasa sheria inazuia watu wanachakachua je wakiruhu hali itawaje!.jf tusaidie kupinga japo wametaja ni vitu maalumu lakini vifaa walivyotaja ni mhm sana si rahisi kukwepa wizi.
   
 17. m

  mhondo JF-Expert Member

  #17
  Nov 10, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Ni vifaa gani ambavyo wamevitaja ambavyo vinaweza kununuliwa ambavyo vimetumika?.
   
 18. kichwat

  kichwat JF-Expert Member

  #18
  Nov 10, 2011
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 1,824
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Michango inaendelea kutolewa katika mjadala unaoendelea Bungeni kuhusu kuruhusu Serikali kununua vifaa vilivyotumika (CHAKAVU)

  Baadhi ya Hoja:
  1. Ni pendekezo lenye mtazamo na mawazo ya Kimaskini.
  2. Mara nyingi vifaa used vinakuwa na teknolojia iliyopitwa na wakati, je spare zitatoka wapi? ...vicious circle
  3. Kama wakati huu ambao sheria hairuhusu Serikali kununua vitu used, na tayari Halmashauri na Wizara nyingi zimenunua vifaa used BILA AIBU, je tukiruhusu itakuwaje? ....mwanzo wa mwisho wa Tanzania.
  4. Labda lengo la Mswada ni kuwapa fursa wafanyabiashara wazawa ambao kwa sasa wanashindwa kupambana kimtaji na wale ambao wanauza vifaa vipya (think of Asians). ...kuna class fulani inataka KUTOKA.
   
 19. T

  Tetere Enjiwa JF-Expert Member

  #19
  Nov 10, 2011
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 217
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Katika muswaada wa manunuzi ya umma serikali imependekeza kununuliwa vitu vilivyo tumika, serikali imetaja maeneo ya kununua vitu chakavu kuwa ni meli, ndege, vichwa vya treni na mabehewa yake. Cha kujiuliza katika kipindi hiki serikali inapo jipanga kufufua shirika la ndege na reli kwa nini izungumzie kununua ndege au vichwa vya treni vilivyo tumika, je sio kuwa viongozi wetu ambao wengi ni mafisadi wanatengeneza mazingira ya kuibia serikali kitapeli kwa kupitia kupitisha mswaada huu wa manunuzi?

  Tukumbuke pia wakati wa kampeni rais alitoa ahadi za kununua meli sehemu mbalimbali sasa isije kuwa wajanja walio serikalini wanataka kutumia mwanya huu wakishirikiana na mafisadi wenzao wafanyabiashara kuibia serikali? Kubwa zaidi kutokana na mapendekezo ya mswada, ufisadi huu wa manunuzi utalihusisha baraza la mawaziri katika kutoa kibali cha manununuzi ya vyombo hivi vilivyo tumika. Wana jf hebu jaribuni kutoa maoni yenu katika hili.
   
 20. k

  kimboka one JF-Expert Member

  #20
  Nov 10, 2011
  Joined: Jan 23, 2010
  Messages: 734
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  ndege,meli na train na vingine inapolazimu
   
Loading...