Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mafao Kutua Bungeni - Mapendekezo Kunufaisha Wachache | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mafao Kutua Bungeni - Mapendekezo Kunufaisha Wachache

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by wikolo, Oct 25, 2012.

 1. w

  wikolo JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 801
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  [h=2]Muswada wa mafao wawaliza wafanyakazi[/h]  25th October 2012
  [​IMG] *Utawanufaisha wanachama wa mfuko mmoja  Muswada wa marekebisho ya sheria ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ambao unatarajiwa kuwasilishwa katika mkutano wa Kumi wa Bunge, umewaacha solemba wanachama wa mifuko mingine baada ya marekebisho hayo kurejesha fao hilo kwa mfuko mmoja pekee.

  Sheria ya mafao ilipitishwa katika mkutano wa Bunge wa Aprili mwaka huu na kuwazuia wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii kuruhusiwa kuchukua mafao yao hadi wafikishe umri kati ya miaka 55 na 60.

  Baada ya wanachama wa mifuko hiyo na wadau wengine wakiwamo wabunge kuipinga sheria hiyo, serikali iliahidi kuwa itaifanyia marekebisho na kuwasilisha muswada kwa hati ya dharura.

  Tayari Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, amekwishawasilisha muswada huo katika Ofisi Ndogo za Bunge, jijini Dar es Salaam, ikiwa na maana kuwa utajadiliwa kwenye Mkutano wa Bunge unaotarajiwa kuanza wiki ijayo.

  Muswada huo unakusudia kufanya marekebisho ya sheria mbalimbali.

  Kwa mujibu wa muswada huo, ambao NIPASHE imeuona, sehemu ya sita inapendekeza marekebisho kwenye Sheria ya Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF), sura ya 372 kwa kuongeza kifungu kipya cha 44 ili kutoa fursa kwa mfuko huo kutoa fao la kujitoa kwa mwanachama wake.

  Kwa maana nyingine ni kwamba wanachama wa mifuko mingine kama NSSF itaendelea kutumia sheria ambayo imelalamikiwa na wafanyakazi.


  HOJA YA JAFO YAZIKWA

  Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mbunge wa Kisarawe (CCM), Seleman Jafo, ambaye wakati wa mkutano wa Bunge wa Bajeti, alitaka kuwasilisha muswada binafsi, alisema amepata barua kutoka kwa Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashillilah, ikimtaarifu kwamba, serikali itawasilisha muswada wa marekebisho hayo, hivyo hana sababu ya kuandika muswada mpya.

  Jafo alisema kwa kuwa alikwishawasilisha hoja ya kutaka marekebisho kwenye sheria ya hifadhi ya jamii, Bunge lilimweleza kwamba ni fursa kwa serikali au Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii; hivyo serikali imeazimia kuiwasilisha kwenye mkutano ujao.

  “Lakini kwa hali hii ni kwamba serikali haitatatua matatizo ya msingi ya hoja yangu, muswada unatakiwa uguse mifuko yote kwa sababu malalamiko ni ya wafanyakazi wote,” alisema.

  SUGU AIONYA SERIKALI

  Kwa upande wake, Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu, aliionya serikali kutochezea wafanyakazi kwa kuwa kufanya hivyo ni kuhamasisha fujo.

  Alisema ni vyema marekebisho yatakayowasilishwa bungeni yakarejesha fao la kujitoa kwa mifuko yote kwa kuwa wafanyakazi wengi hawana usalama kazini.

  “Tunajua faida ya pensheni uzeeni kwa sababu ni msaada mtu anapostaafu, lakini kwa mfumo wa nchi yetu ambayo wafanyakazi hawana usalama wa kazi haiwezi kufanyakazi ipasavyo,” alisema.

  Sugu alisema wafanyakazi kama wa migodini au hostelini wanafanyakazi katika mazingira magumu na wanaweza kuachishwa kazi wakati wowote hivyo fao la kujitoa litawasaidia.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau, alisema fao la kujitoa katika mifuko ya hifadhi ya jamii halimo katika sheria za kimataifa.

  Dk. Dau, alisema hayo alipokuwa akijibu hoja za wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) katika kikao kati ya kamati hiyo na bodi na menejimenti ya shirika hilo, katika Ofisi Ndogo za Bunge, jijini Dar es Salaam jana.

  Alisema pia ni Tanzania Bara pekee ndiko ambako kuna fao la kujitoa katika mifuko hiyo, lakini katika nchi za Kenya, Uganda, duniani kote, hata Zanzibar, suala hilo halipo.

  Hata hivyo, alisema mwanachama wa NSSF anapoamua kujitoa, anaupunguzia Mfuko mzigo wa kumtunzia pensheni yake ya uzeeni, badala yake na kujiumiza mwenyewe.

  Shinikizo la kutaka serikali kuirekebisha sheria hiyo ili wanachama wa mifuko walipwa mafao wakati wanapoacha kazi, liliilazimisha serikali kukubali yaishe na kuahidi kuwasilisha muswada wa marekebisho ya sheria ya mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2012.

  Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka, aliliambia Bunge la bajati kwamba kabla ya kuwasilishwa, muswada huo utapelekwa kwa wadau ili watoe maoni na pia Mamlaka ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) itatoa elimu kuhusu fao la kujitoa.

  Hata hivyo, alisema wapo baadhi ya watu waliotafsiri kuwa kusitishwa kwa fao la kujitoa kwamba mifuko ya hifadhi ya jamii imefilisika kwa kuwa imewekeza kwenye miradi mibaya, jambo alilosema sio la kweli.

  Kabaka alisema kuwa mifuko hiyo haina hali mbaya kifedha wala haijafilisika na kwamba kuzuia fao la kujitoa ni utekelezaji wa sheria.

  Waziri Kabaka alisema mchakato wa kuwasilisha muswada huo utaanza mara moja kwa kuwashirikisha wadau wote wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii.

  Kabla ya kauli ya Kabaka, Bunge lilipitisha Azimio lililowasilishwa na Jafo, la kuletwa bungeni muswada wa dharura wa marekebisho ya Sheria Na. 5 ya mwaka 2012 inayozungumzia marekebisho ya Sheria ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ambayo ndani yake inaelezea kuzuiwa kwa fao la kujitoa kwa wafanyakazi.

  Kutokana na mapendekezo ya muswada huo kutowatuhusu wanachama wa mifumo kingine kuchukua mafao kabla ya miaka 55 au 60, wanachama hao huenda wakashinikiza kwa njia za maadamano na migomo.

  Aidha, upo uwezekano wa kuzuka mjadala mkali bungeni kwa kuwa na wabunge nao ni wanachama wa m
  ifuko hiyo.


  Source: Nipashe
   
 2. K

  Kintiku JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 611
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 45
  Kama wanadhani maandamano ni CHADEMA tu basi ngoja waone safari hii wafanyakazi wanavyoweza kuamdamana
   
 3. w

  wikolo JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 801
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mkuu unadhani ni nani atawaongoza wafanyakazi hawa kudai haki yao? Manake kwa viongozi wa TUCTA wanavyolichukulia hili, ni kama haliwahusu vile!
   
 4. moto2012

  moto2012 JF-Expert Member

  #4
  Oct 25, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 2,171
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  TUCTA waamke sasa wajenge heshima kwa wanachama wao! Mimi nasubiri kusikia tamko la TUCTA wakikaa kimya juu ya hili najua watakuwa wamenunuliwa
   
 5. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #5
  Oct 25, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Haijalishi, mifuko imefilisika au haijafilisika, mimi nataka fedha zangu. Mwakani nakwenda chuo, wameninyima mkopo sasa wanataka kuninyima fedha zangu za NSSF. Wafie mbali na siasa zao. Wanaharibu nchi tu hawa. Viongozi gani wasio na mipango. Kama wanataka fedha wachukue kwenye madi si fedha yetu.
   
 6. Scofied

  Scofied JF-Expert Member

  #6
  Oct 25, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,026
  Likes Received: 203
  Trophy Points: 160
  tunawapa wiki mbili tu tujue mbivu na mbichi ndo watajua nguvu ya wafanyakazi....tutajua nani mkombozi wa kweli wa wananchi.....chadema tunawategemea kwa hili msituangushe tafadhalini....hata kama kwa kuvunja hizo thamani huko bungeni...
   
 7. O

  Orche Senior Member

  #7
  Oct 25, 2012
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 146
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hivi ni kwa nini viongozi wetu wana dharau hivi? Inanisikitisha sana maana kwa serikali inayothamini watu wake na kujua kuwa ni watu wazima haiwezi kufanya kitu kama hiki. Kwanza walisema hoja haijakamilika mpaka mwakani, lakini waliposikia Mh. Mnyika analeta hoja binafsi ndo wanakuja na hoja ya danganya toto kama hili. Tuombe Mungu atusaidie watanzania maana hili ni janga.
  Ni wakati muafaka kwa wafanyakazi kushikamana kudai haki yao bila uoga wala itikadi yoyote. Tusiogope vitisho vyovyote vya serikali hii ya CCM
   
 8. m

  mdunya JF-Expert Member

  #8
  Oct 25, 2012
  Joined: Oct 7, 2012
  Messages: 765
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  pole mkuu! Imetoka hiyo unless . . . . !
   
 9. m

  mdunya JF-Expert Member

  #9
  Oct 25, 2012
  Joined: Oct 7, 2012
  Messages: 765
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  samani
   
 10. C

  CDM Member

  #10
  Oct 25, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 73
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Mimi huku niliko mbali. nimezimia kabisa nikiamka nataka pesa zangu
   
 11. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #11
  Oct 25, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 25,677
  Likes Received: 16,614
  Trophy Points: 280
  Ndugu zangu mlitegemea nini wakati PESA zote zimeelekezwa kwa DARAJA la KIGAMBONI na CHUO KIKUU CHA DODOMA?
   
 12. manuu

  manuu JF-Expert Member

  #12
  Oct 25, 2012
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 4,063
  Likes Received: 9,674
  Trophy Points: 280
  NSSF si ndiyo mfuko unaongoza kwa kutumia pesa zetu wanachama katika miradi hasara ya serikali.?
   
 13. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #13
  Oct 25, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,320
  Likes Received: 5,611
  Trophy Points: 280
  Vasco Da Gama ameleta uswahiba amechezea pesa za walalahoi kwa manufaa yake kisiasa bila idhini ya wachangiaji na ameshindwa na hataweza kuzilipa labda auze migodo yake,sasa anatapatapa kurudisha uwezo wa NSSF ya swahiba Dau!CDM sijui wako wapi wachukue nchi na kumaliza uswahiba huu nchi isonge mbele.Kama EL akileta hoja hiyo kurudisha imani ya wafanyakazi,atapata kura zote hata za wapinzani,maana rais lazima atoke kaskazini ama la patachimbika na CCM itameguka!!
   
 14. K

  Kifulambute JF-Expert Member

  #14
  Oct 25, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,518
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  kwanza tokea waseme mimi sipeleki yangu tena NSSF ni ujinga mtupu
   
 15. K

  Kifarutz JF-Expert Member

  #15
  Oct 25, 2012
  Joined: Aug 7, 2012
  Messages: 1,695
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Nauona live usaliti wa TUCTA na serikali zingine ni za kiku-ma kabisa
   
 16. m

  mdunya JF-Expert Member

  #16
  Oct 25, 2012
  Joined: Oct 7, 2012
  Messages: 765
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  hivi huyu mama waziri wa vijana na ajira Gaudensia Kabaka kapatwa na ugonjwa gani? Mpaka . . . . . . !
   
 17. Bwaksi

  Bwaksi Senior Member

  #17
  Oct 25, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 125
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kuna watu tutajitoa mhanga kwa niaba ya wafanyakazi wenzetu waliolala usingizi. Hizi pesa ni haki yetu. Lazima kieleweke
   
 18. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #18
  Oct 25, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 271
  Trophy Points: 180
  nadhani mwisho wa huyu DAU ndo unafika sasa
   
 19. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #19
  Oct 25, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280

  Wafanayakazi kuandamana? Sahau.
   
 20. Mtingaji

  Mtingaji JF-Expert Member

  #20
  Oct 25, 2012
  Joined: Sep 28, 2012
  Messages: 1,217
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Ramadhani Dau inaonekana hajui hata wenye pesa anazozisimamia ni akina nani? katika sheria za kimataifa zinazo faa ni hiyo tu ya kuzuia fao la kujitoa ndiyo anazungumzia? Afanye kwanza kama alivyokuwa anafanya Gaddafi, atoe nyumba bure-asikopeshe, atoe umeme bure, atoe huduma ya maji bure, atoe matibabu ya uhakika bure na atoe elimu bure!

  Kwanza kwa fomular ya PAYE ya kodi, wafanyakazi wengi tunalipa kodi hiyo kwa zaidi ya 33% ya kipato cha mfanyakazi, tukifika mitaani tunakutana na VAT kwenye bidhaa 18%. Ukijumlisha PAYE + VAT= 51%.

  Nchi ambazo zina kodi ya zaidi ya 50% kama nchi za nordic, huduma za jamii ziko juu sana na mtu akizeeka, anapelekwa kwenye nyumba za wazee kutunzwa huko. huyu Dau hayo hazungumzii analopoka kama amenawa uso asubuhi kwa kutumia kopo la chooni!

  Ukichukulia Kenya, mfanyakazi anatozwa 5% na mwajiri analipa 15%, pesa hiyo inakuwa inazaa kila mwaka. Mtu akifikisha umri wa kustaafu, analipwa mkupuo mara dufu ya ile aliyochangia, kisha anaanza kulipwa pension. Tanzania ukistaafu, mifuko ya NSSF/PPF ukibahatika kulipwa-maana ni bahati pesa yako ikiwa imezaa si zaidi ya 1% jumlisha na usumbufu wa kuwa unafuatilia kila mara makao makuu!

  Kama mtu akichukua pesa yake anakupunguzia mzigo, kwa nini ung'ang'anie huo mzigo, Dau anauchungu sana na wazee wa kesho wakati hawa wa leo wanapigwa mabomu barabarani, matibabu ya bure inekuwa ngumu nk.

  Dau kajipange upya, kauli zako zitalighalimu taifa siku si nyingi, kwa vile una roho ngumu kwa msimamo wa unakoswalia, anza kuandaa sentesi zingine mapema kwani yaliyotokea Marekana yatakwenda kutokea kwenye nchi ya Hayati Mwl. Nyerere.
   
Loading...