Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya kodi ya Madini, Majengo na Pombe kali wapitishwa Bungeni

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,438
3,333
BUNGE limepitisha muswada wa sheria ambao pamoja na mambo mengine unaondoa kodi ya zuio la asilimia tano inayotozwa kwenye bei ya kuuzia madini kwa wachimbaji wadogo na kurekebisha Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa kutoa msamaha kwenye madini ya metali na vito yatakayouzwa katika masoko ya ndani ya nchi.

Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Namba 2 wa Mwaka 2019, umekuja siku 17 tangu Rais John Magufuli azungumze na wadau mbalimbali wa madini na kukubaliana kuondoa changamoto mbalimbali kwa wachimbaji wadogo wa madini nchini zilizowasilishwa kwake.

Muswada huo ulisomwa kwa mara ya pili na ya tatu bungeni chini ya hati ya dharura.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi amesema marekebisho hayo pia yanalenga kuondoa changamoto za wakulima wa zabibu na viwanda vilivyotumia zabibu katika uzalishaji na kuweka vitango vya mfuto vya kodi za majengo.

Alizitaja sheria zilizofanyiwa marekebisho ni Sheria ya Madini, ya Ushuru wa Bidhaa, Kodi ya Mapato, Mamlaka ya Serikali za Mitaa ya utozaji kodi ya majengo, na ya VAT.

Profesa Kirangi alisema lengo la marekebisho ya sheria ya madini ikiwa ni pamoja na kuondoa kodi ya zuio kwenye bei ya kuuzia madini ya aina zote kwa wachimbaji wadogo, lengo ni kuwahamasisha wachimbaji wadogo kuuza madini yao katika masoko ya madini yaliyoanzishwa na hivyo kuzuia utoroshaji wa madini nje ya nchi.

Marekebisho hayo pia yanakusudia kuanzisha vituo vya ununuzi wa madini katika maeneo ambako masoko ya madini hayakuwepo, na kuweka utaratibu wa uingizaji madini nchini.

Lakini pia kuweka mfumo thabiti utakaowezesha wachimbaji wadogo wa madini kununua na kuuza madini katika vituo vya ununuzi na masoko ya madini.

Kuhakikisha kodi zinazohusu leseni za madini zinalipwa kabla ya leseni kuhamishwa kwenda kwa umiliki mwingine na kuhakikisha mapato yanayotokana na biashara ya madini yanakusanywa ipasavyo.

Kuhusu marekebisho ya sheria ya bidhaa, yanalenga kupunguza ushuru wa bidhaa kwenye pombe kali inayotengenezwa nchini kwa kutumia zabibu zinazozalishwa nchini kutoka Sh 3,315 kwa lita hadi Sh 450 kwa lita.

“Marekebisho hayo yanalenga kuhamasisha viwanda vinavyozalisha vinywaji vikali hapa nchini kutumia mchuzi wa zabibu unaozalishwa na zabibu zilizolimwa ndani ya nchi ili kuhamasisha wawekezaji wengi kuwekeza katika uzalishaji wa vinywaji vinavyotumia mchuzi wa zabibu hiyo na hivyo kuongeza ajira, kuchochea kilimo cha zabibu na kuimarisha uchumi wakulima wa zabibu,” alisema Profesa Kilangi.

Lakini pia serikali inalenga kuondoa tatizo la wakulima wa zabibu nchini kukosa soko la kuuza zabibu kutokana na wazalishaji wa vinywaji vikali vinavyotumia zao hilo kutonunua kwa wingi kutokana na ushuru mkubwa wa bidhaa kwenye vinywaji vikali vinavyozalishwa kwa zao hilo.

Kuweka viwango mfuto vya kodi za majengo badala ya utaratibu wa hivi sasa ambapo kodi ya majengo kwa majengo yaliyofanyiwa uthamini inatofautiana kutokana na thamani ya kila jengo.

“Lengo la serikali ni kuondoa tatizo la ukwepaji kodi ya majengo na kuhamasisha wananchi kulipa kodi hiyo kwa hiari,” alisema Profesa Kirangi.

Katika marekebisho ya sheria ya serikali za mitaa ya utozaji wa kodi ya majengo, yanaweka viwango mfuto vya kodi ya majengo Sh 10,000 kwa nyumba ya kawaida, Sh 20,000 kwa nyumba ya ghorofa kwa maeneo ya makao makuu ya halmashauri za wilaya na mamlaka za miji midogo.

“Shilingi 10,000 kwa nyumba za kawaida na shilingi 50,000 kwa kila sakafu ya nyumba ya ghorofa iliyopo katika maeneo ya majiji, manispaa na halmashauri za miji,” alieleza.

Kutoza kodi ya majengo kwa kila kiwanja badala ya kila jengo lililopo ndani ya kiwanja husika kwa maeneo ya halmashauri za wilaya, mamlaka za mapato kuendelea kukusanya kodi ya majengo katika majiji, manispaa na halmashauri za miji na za wilaya kwa kushirikiana na serikali za mitaa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bajeti, George Simbachawene alisema inakubaliana na serikali kutoza adhabu kwa makosa yanayotokana na kufanya biashara ya madini kinyume cha sheria.

Adhabu hizo ni kutoza Sh milioni tano na isiyozidi Sh milioni 10 pamoja na kifungo kati ya mwaka mmoja hadi mitano na Sh milioni 20 na isiyozidi Sh milioni 50 kwa kampuni, hiyo alisema itasaidia wachimbaji wadogo na wafanyabiashara kufuata taratibu na sheria za biashara ya madini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bunge limepitisha Muswada wa Sheria wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba mbili ya Mwaka 2019 ambao umelenga kutatua changamoto za za kodi ikiwemokodi ya Majengo, madini na Kodi uya Ongezeko la Thamani (VAT).

Muswada huo uliopelekwa Bungeni kwa Hati ya Dharura ulijadiliwa na kupitishwa ambapo Wabunge mbalimbali walipata fursa ya kutoa maoni yao.

Akizungumza wakati wa kuwasilisha Muswada huo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Prof. Adelardus Kilangi, alisema kuwa marekebisho hayo yameondoa kodi ya zuio (withholding tax) kutoka 5% hadi asilimia sifuri kwenye bei ya kuuzia madini ya aina zote kwa wachimbaji wadogo ili kuwahamasisha wachimbaji hao kuuza madini katika masoko ya madini.

Alisema marekebisho hayo yanalenga kudhibiti upotevu wa mapato ya Serikali na kuhakikisha mapato yanayotokana na biashara ya madini yanakusanywa ipasavyo.

Aliongeza kuwa Muswada huo umependekeza kutoa msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa wachimbaji wadogo wa madini watakaouza madini yao katika masoko ya madini na vituo vya ununuzi wa madini.

Aidha, Prof. Kilangi alibainisha kuwa Muswada huo pia umependekeza kila kiwanja kitozwe Kodi ya Majengo badala ya kila jengo lililopo ndani ya kiwanja husika kwa maeneo ya Halmashauri za Wilaya.

Sheria zilizopitishwa ni pamoja nma Sheria ya Ushuru wa Bidhaa Sura ya 147, Sheria ya Kodi ya Mapato Sura ya 332, Sheria ya Mamlaka za Serikali za Mitaa ya Utozaji wa Kodi ya Majengo Sura ya 289, Sheria ya Madini Sura ya 123 na Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani Sura ya 148.

“Madhumuni ya marekebisho ya Sheria hizo pamoja na mambo mengine ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya kuondoa changamoto kwa wachimbaji wadogo wa madini, wakulima wa zabibu ndani ya nchi na viwanda vinavyotumia zabibu hiyo katika uzalishaji pamoja na kuweka viwango mfuto (fixed rate) vya kodi ya majengo.” Alisema Prof. Kilangi.

Alisema kuwa Serikali imeona upo umuhimu wa kuwasilisha Muswada huu kwa haraka kupitia Hati ya Dharura ili kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo kupunguza utoroshwaji wa madini nje ya nchi unaofanywa na wachimbaji wadogo ambao wanakwepa kodi.
 
Ni jambo zuri tunasubiri utekelezaji tu.

Maana kwa mfano kama withholding tax,sheria zinaeleza vzr tu lkn utekelezaji wake huku mtaani sio kabisaa.
 
Du! JF bwana thread positive kama hii hakuna anayejitokeza kuchangia. Wana JF wanapenda sana ligi za snitchers na spinners zaidi kuliko positive development. Pengine hii ndio sababu spinners wa upinani hapa nchini huwa hawachaguliwi kuongoza nafasi za uongozi wa dola kwa kuwa wapiga kura ni positive na wahahitaji positive development communication.
 
Kwa kupunguza kiwango cha kodi kwenye vileo vinavyotengenezwa kupitia juisi ya zabibu kutasababisha viwanda vya pombe kali kuongezeka bei ya pombe kali itashuka vijana wataweza kuimili bei kwahyo mbali na mapato ya serikali kuongezeka ila na kundi la vijana walevi litaongezeka kwa kiwango cha lami.
 
Du! JF bwana thread positive kama hii hakuna anayejitokeza kuchangia. Wana JF wanapenda sana ligi za snitchers na spinners zaidi kuliko positive development. Pengine hii ndio sababu spinners wa upinani hapa nchini huwa hawachaguliwi kuongoza nafasi za uongozi wa dola kwa kuwa wapiga kura ni positive na wahahitaji positive development communication.
Kwa taarifa yako katika sheria ya madini the core problems have neither solved nor explained.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
What is that core problem?
Black market. Yaani mchimbaji anachimba anauza kwa broker na broker anauza kwa dealers kwa bei ya soko LA dunia. Dealers anatengemea kupata faida kwa price fluctuations. Mfano 300kg iliyokamatwa imekamatwa kwa wanunuzi. Mnunuzi ananunua Tsh500 to 1000 less than London metal exchange kwa kila gram inayouzwa kwa sasa around tsh90000, unaweza jiuliza MTU anatafuta faida ya 1000 kwa kila 90000. Hivyo ukimwambia atoe 7% royalty razima apate hasara. Kwa maana hii Serikali inapaswa kuwatoza wachimbaji kabla hawajauza kwa broker ili biashara iwezekane. Bahati mbaya wachimbaji hawaeleweki hivyo serikali inashindwa kuwa control na hapo black market inaingia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kupunguza kiwango cha kodi kwenye vileo vinavyotengenezwa kupitia juisi ya zabibu kutasababisha viwanda vya pombe kali kuongezeka bei ya pombe kali itashuka vijana wataweza kuimili bei kwahyo mbali na mapato ya serikali kuongezeka ila na kundi la vijana walevi litaongezeka kwa kiwango cha lami.
Pombe kali za bei cheap zipo hata sasa hivi, mimi ninaona tunapiga hatua

Pia raisi na baraza lake la mawaziri wamefanyia kazi maoni ya wadau wa madini, one step at a time tutafika tuu

Leo, nimeona TARURA, ndio wanakusanya ushuru wa kupaki magari hapa dar es salaam sijajua mikoa mingine, ni moja ya step, tunakuwa na uhakika bara bara za mitaa kuboreshwa kwa kiwango kizuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haupo fair. Ni Kodi ya kodi ya kichwa inarudishwa Kiana aina

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana mkuu, ukiangali hapo kodi zimeondolewa kabisa na sehemu nyingine zimepunguzwa kwa kiasi kikubwa

Mfano kwenye madini, 5% ya withholding tax haipo tena, mwanzoni ilikuwepo

VAT, imeondolewa kwenye masoko ya ndani, mwanzoni ilikuwepo...hiyo ni 18%

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapana mkuu, ukiangali hapo kodi zimeondolewa kabisa na sehemu nyingine zimepunguzwa kwa kiasi kikubwa

Mfano kwenye madini, 5% ya withholding tax haipo tena, mwanzoni ilikuwepo

VAT, imeondolewa kwenye masoko ya ndani, mwanzoni ilikuwepo...hiyo ni 18%

Sent using Jamii Forums mobile app
Kodi ya majengo is not fair kabisa. Mwenye ghorofa wakati nae ni kiwanja kimoja eti alipie 50000 kila sakafu. Hii ni akili au matope maana yake watu waache kujenga magorofa na inaweza ikawa ghorofa ya kuishi tuu sio biashara. Nikijenga ghorofa na flat moja juu nalipia 50000. Is not fair

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kodi ya majengo is not fair kabisa. Mwenye ghorofa wakati nae ni kiwanja kimoja eti alipie 50000 kila sakafu. Hii ni akili au matope maana yake watu waache kujenga magorofa na inaweza ikawa ghorofa ya kuishi tuu sio biashara. Nikijenga ghorofa na flat moja juu nalipia 50000. Is not fair

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa mkuu unataka mwnye ghorofa alipe kiasi gani?kama jengo lina sakafu(floor) 30, ni fair alipe hivyo mbona masikini hatuna maghorofa tumewekewa 10k, wanaonyonywa ni hao matajiri kwa expense za masikini, fair

Sent using Jamii Forums mobile app
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom