Muswada wa mafao kwa viongozi wakwama tena Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muswada wa mafao kwa viongozi wakwama tena Zanzibar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kiche, Jan 24, 2012.

 1. k

  kiche JF-Expert Member

  #1
  Jan 24, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), imesitisha mjadala wa muswada wa sheria mpya ya masilahi na mafao ya viongozi wa kisiasa baada ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuukataa muswada huo, kwa madai ya kutozingatia masilahi ya Taifa.

  Muswada huo, ulianza kupata misukosuko ya kukataliwa na Wajumbe kutokana na sheria hiyo, kupendekeza watoto wa Marais wastaafu, kulipwa pensheni ya mshahara wa kima cha chini Sh. 125,000 kwa kiwango cha sasa kwa kila mwezi, ambapo wanawake ukomo wao utakuwa ni baada ya kuolewa na wanaume baada ya kufikisha umri wa miaka 20.

  Aidha Sheria hiyo, imependekeza wajane wa Marais Wastaafu, kuanza kulipwa pensheni ya kila mwezi sawa na mshahara anaolipwa Rais aliyopo madarakani pamoja na kupewa huduma ya nyumba na matibabu.

  Muswada huo uliowasilishwa Januari 18 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini, baada ya wajumbe kukamilisha kazi ya kuujadili na Waziri kuitwa kufunga mjadala wa muswada huo.

  Waziri Makame, alisema baada ya Serikali kuzingatia maoni na mapendekezo ya Wajumbe, ameamua kuahirisha kufanya majumuisho ya muswada huo, hadi kikao kijacho cha Baraza hilo, ili kutoa nafasi ya kuzingatia mapendekezo ya wajumbe kuhusiana na Muswada huo.

  "Mheshimiwa Spika, naomba kusisitiza muswada hauondoshwi, kinachofanywa ni kuahirisha kutoa majumuisho hii leo, ili kupata fursa ya kuwasilisha mabadiliko ya muswada kwenye kamati iliyopitia muswada huu, kwa lengo ambalo kwa pamoja Serikali na Waheshimiwa Wawakilishi wapate kuelewana zaidi na kukubaliana katika mapendekezo yao kwa faida ya Nchi," alisema.

  Alisema kwa mujibu wa kanuni ya 85(1) ya baraza la wa wawakilishi, ameamua kuahirisha kufanya majumuisho ya muswada huo, hadi kikao kijacho cha Baraza hilo, kitakachofanyika baada ya miezi mitatu.

  Muswada huo ulichangiwa na Wajumbe 37, wakiwemo Mawaziri 11 ambao walisimama kuutetea kwa hoja mbalimbali, lakini Wajumbe 26 waliochangia muswada huo, waliupinga kwa maelezo haujazingatia msilahi ya nchi, na utawabebesha mzigo wananchi ambao ndio walipa kodi.

  Wawakilishi hao, walisema kabla ya Serikali kufikiria kuongeza masilahi ya viongozi wa kisiasa, ilipaswa kutatua kero za kiuchumi na huduma za jamii zinazowakabili wananchi wa Zanzibar.

  Muswada huo umekwama kwa mara ya pili baada ya awali kukataliwa katika kikao cha Baraza hilo kilichofanyika Oktoba mwaka jana.

  CHANZO: NIPASHE

  Mtazamo wangu.

  Hivi kweli mswada kama huu unaolazimishwa unatofauti na ufisadi?inaingia akilini kupitisha malipo ya aina hii!!??kama malipo ya aina hii yanaweza kulazimishwa hivi ni mangapi yaliyojificha yanayotendwa na viongozi wetu??ingekuwa ni kwenye bunge la jamuhuri tayari yangeshapita kwani wabunge wetu wengi akili ya kufikiri ni ndogo sana ni kama hakuna,kwa mtu mwenye fikra sahihi ni lazima wamkere.
   
 2. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #2
  Jan 24, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Safi sana! na bado uendelee kukwama hivyohivyo.
   
 3. N

  Njele JF-Expert Member

  #3
  Jan 24, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sijapata kuona mafao ya upendeleo kiasi hicho, ni dalili ya viongozi waliopo madarakani wanajitengenezea mazingira watakapostaafu.
   
 4. EPA TZ

  EPA TZ Member

  #4
  Jan 24, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yan viongozi wetu wa serikali ambao wamewasilisha huo muswada ndio wanaofikiria kimasaburi masaburi aka 'MAKALIO'
   
 5. k

  kiche JF-Expert Member

  #5
  Jan 24, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hii nchi inakera sana,akitokea mtu anatafuta watu wa kuingia msituni naamini itabidi wengine wakataliwe kwa jinsi watakavyokuwa wengi!!!
   
 6. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #6
  Jan 24, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Yaani mtu akilala akiamka ajiulizi atawafanyia nini watanzani? ye anajiuliza atawaibia vipi watanzania.
  Kweli kuna haja ya kuingia msituni.
   
 7. magessa78

  magessa78 JF-Expert Member

  #7
  Jan 24, 2012
  Joined: Sep 28, 2009
  Messages: 271
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yaani mjane wa karume alipwe mshahara sawa na rais shain?maajabu ya dunia haya!
   
 8. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #8
  Jan 24, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Nadhani tunatakiwa kuhoji akili za waziri aliyepeleka muswaada huu barazani! Halafu hivi Rais wa "NCHI HII" kweli yuko makini nahoja zinazokwenda barazani? Masaburi wee wacha tu!
   
 9. MANI

  MANI Platinum Member

  #9
  Jan 24, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,410
  Likes Received: 1,863
  Trophy Points: 280
  Mkuu umesahau na watoto pia walipwe !
   
Loading...