FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 37,897
- 43,796
Natoa rai kwa wabunge kupendekeza adhabu ya kunyonga hadi kufa kwa waagizaji Wa madawa ya kulevya hasa 'sukari laini'. Mbinu hii imeonyesha kufanikiwa sana kwa nchi kama za China na Vietnam ambapo walimnyonga raia wa Australia kwa kuingia Vietnam na madawa ya kulevya. Kiukweli hakuna tofauti ya kumpiga mtu risasi ya kichwa na kumuuzia sembe, its the same thing, unamuua. Tofauti ni kwamba kumuua kwa madawa ni kifo cha kumtesa kwa muda mrefu, hivyo adhabu ya kunyonga ni quite appropriate. Najua wabunge wanaogopa kukutwa na kilichomkuta Amina Chifupa kwa kujitia 'kiherehere', lakini ni bora nyie wabunge wachache mfe kwa ajili ya wengi kuliko taifa lote liteketee kwa madawa ya kulevya. Najua kipindi kile cha uongozi wa kuchekeana chekeana na kupeana wiki moja muache kuuza madawa ilihali majina mtu anayo kimeshapita, na sasa hatuangalii mtu usoni, this is serious indeed! Lazima anyongwe mtu ndio tuonyeshe kwamba hii issue sasa ni serious. JPM kazi kwako.