Muswada wa kukusanya maoni juu ya Marekebisho ya Katiba watinga Bungeni leo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muswada wa kukusanya maoni juu ya Marekebisho ya Katiba watinga Bungeni leo

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Pascal Mayalla, Apr 5, 2011.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Apr 5, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,621
  Trophy Points: 280
  Salaam wana bodi,

  Hatimaye ule Muswada Tata wa Marekebisho ya Katiba, umewasilishwa rasmi Bungeni leo kwa ajili ya kutangazwa kwa mara ya kwanza chini ya hati ya dharura.

  Baada ya hapo ndipo itafuatia hatua ya muswada huo kujadiliwa kwenye ngazi ya kamati kwa muda wa siku nne. Majadiliano hayo, yatafanyika mjini Dodoma kwa siku mbili na baadaye kuhamia jijini Dar es Salaam kwa siku mbili nyingine.

  Maoni ya wadau yatajumuishwa na kupelekwa bungeni kusomwa tena kwa mara ya pili na kujadiliwa na wabunge kwa muda wa siku mbili tarehe 18 na 19 mwezi April. Tarehe hiyo kipindi cha jioni, Bunge litakaa kama kamati kupitia kifungu kwa kifungu, na around 1:30 usiku, utasomwa kwa mara ya tatu na utapitishwa kwa kauli moja (ya wabunge wa CCM, hata wapinzani wote wakigomea!), na kuwa sheria rasmi. Bunge litaahirishwa mpaka Jummane Juni 7 ambalo ni la kikao cha bunge la bajeti na mchezo kuigiza wa katiba mpya, utaishia hapo, itabaki utekelezaji tuu.

  My Take:
  Kuawsilishwa huku, ni uthibitisho mwingine wa jinsi serikali yetu ilivyo ni serikali ya kibabe, jeuri na yenye msimamo mkali, ikiamua kitu, imeamua, hata wananchi wake wapige kelele vipi, haitasaidia kitu,
  Ni marekebisho ya katiba na sio katiba mpya!.

  Naomba kuwasilisha.

  Pasco.

  ==============
  MASAHIHISHO:

  Muswada uliowasilishwa ni wa namna ya kukusanya maoni ya wananchi juu ya mabadiliko ya Katiba; public hearing itafanyika Dar na Dodoma - Invisible

  Hata Zanzibar nao wameomba kupewa fursa ya Public hearing lakini Spika anadai kuwa Zanzibar wameshauriwa watumie kituo cha Dar es Salaam; Wabunge toka Zanzibar wanapinga hoja hii ya Spika - Invisible

  Wabunge wanapendekeza muswada huu ubadilishwe uende katika lugha ya Kiswahili ili wananchi waelewe nini kimo; serikali inadai inafahamu umuhimu wa kutumia kiswahili lakini hawakufanya tafsiri ya kiswahili na wanatambua kuwa huo ni upungufu, wanaamini wananchi watapata watu wa kupata tafsiri na wao hawadhani kama ni kikwazo sana - Invisible

  Zitto anasisitiza muswada wenyewe ndio kwanza wabunge wameupata na hawajaupeleka kwa wananchi kuujadili, anaona hakuna udharura kwani wabunge lazima kwanza washauriane na wananchi juu ya mabadiliko haya - Invisible

  Spika anadai mmoja wa watu walotaka uwe na uharaka ni Zitto hivyo anamshangaa kuwa inakuwaje atoe hoja hiyo - Invisible
   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #2
  Apr 5, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,610
  Likes Received: 3,911
  Trophy Points: 280
  Unataka uthibitishiwe mara ngapi?

  Soon after election we forcefully started to ask new const. ..on the way we surrendered... and even forgotten that we need new const.

  Serikali wamefanya NA wataendelea kufanya NA itakuwa hivyo NA hatuwezi kufanya lolote NA tutaishia kulalamika na kuandika articles nyingi NA tutanunua sana magazeti NA tutafika 2015 NA tutafanya uchaguzi kwa same katiba na same NEC NA yatajirudia haya haya NA tutaendelea na maisha NA atakuja rais mwingine na yake.

  Kindly, let me ask you a question and be honest, kwani tatizo mpaka sasa hivi liko wapi? (hints; wananchi, wapinzani, Chama tawala na serikali?)
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Apr 5, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Waberoya

  tatizo la kwanza ni wananchi
  la pili ni vyama vya upinzani
  serikali yenyewe kushindwa kuelewa kwamba yenyewe ndio mhimili na siasa/chama si mhimili

  chama tawala hakina tatizo kwani walishabadili lengo lao kutoka kumkomboa mnyonge hadi kushika dola!!
   
 4. Fred Katulanda

  Fred Katulanda Verified User

  #4
  Apr 5, 2011
  Joined: Apr 1, 2011
  Messages: 229
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nimejaribu kufuatilia Muswada ambao utawasilishwa Bungeni ni huu:
   
 5. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #5
  Apr 5, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ndugu Waberoya, tupe hebu tupe hapa basi habari kamili; ni kweli ni MUSWADA utakua umefika bungeni kwa kuzingatia maoni ya wananchi au wamepeleka huko yale yale maoni ya MAFISADI ili ikabarikiwe kwa jina la Watanzania??

  Haswa hili ndilo jambo zito kuliko yote kwa mwaka huu na tayari vijana kote nchini tupo tunasubiri tu tujue kwamba ni MUSWADA wa aina gani utakua umepelekwa bungeni na kwamba wabunge wenyewe (hasa spika) wataweka maslahi yetu mbele au ya CCM ili tujue kimoja.
   
 6. Zegreaty

  Zegreaty JF-Expert Member

  #6
  Apr 5, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 638
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Naomba wafanye fasta fasta ili Nguvu ya umma ichukue hatamu kwani tutakuwa tumeshapata sababu za kutosha.......tumeshaburuzwa sana,tumeshaonewa sana,sasa tunasema basi inatosha........:rip:CCM.
   
 7. s

  salisalum JF-Expert Member

  #7
  Apr 5, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 379
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Wasije wakarogwa wakapitisha muswada ule. Umeandikwa tu na Werema kutaka kumfurahisha rais, si wajua alivyo mnafiki na asivokuwa independent thinker!
   
 8. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #8
  Apr 5, 2011
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  I updated the 1st post
   
 9. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #9
  Apr 5, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,610
  Likes Received: 3,911
  Trophy Points: 280
  You are right! wananchi ndio wa kulaumiwa mno.. we are slumbering

  Habari gani kamili ya mimi kukupa wewe? kuwa muswada umebeba maoni ya watu ni lini yamechukuliwa? unanitega?

  Nikisoma tu post yako naona ni walewale...jambo zito kuliko yote?.. hilo zito kwako kaka!! watanzania wengi hawana hata mpango na hiyo katiba..Guys tunaposema kazi ipo na tuamshane na sio kupena moyo I know I have seen that we have big problem!!

  eti? unasema na unaamini kabisa Makinda ataenda kinyume na CCM na serikali yake?? you must be dreaming! kama unasubiri Anna abadilike na CCM ibadilike pole sana..pole we!! at a glance, nothing good comes out of CCM nothing!
   
 10. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #10
  Apr 5, 2011
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Another Tanzanian from another motherland.
   
 11. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #11
  Apr 5, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Hivi ni watanzania au hata humu ni members wangapi wanaijua au hata kuiona katiba ya nchi yenu.

  Mimi naamini zaidi ya 90% ya member humu hawajawahu kuiona Katiba ya tanzania zaidi ya kusikia kutoka kwa wanasiasa.

  sasa kuna kazi kubwa kuieleza na kuifundisha jamii nini katiba na umuhimu wake ndio mengine yaende.
   
 12. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #12
  Apr 5, 2011
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Waberoya,

  Nipo nawe aslimia 110, tatizo lako kwangu ni haya;
  • unahisi wewe unajua na u wish mawazo yako ndo sahihi, well, have you practise what you say? kama unahisi unayoamini why usichukue hatua? nilikuuliza ujuzi wako katika haya mambo hukujibu,
  • Huwa husemi as if unashauri ila unakuwa na jazba, sisi tunazo but we used to appreciate hatua zilizofanyika na wengine wewe unalaumu mpaka unawaombea SANDA.
  Fanya unaloweza kwa nafasi yako badala ya kulaumu tu as if ulishatumia resources zako na wengine wakamis-use. Wananchi hawa wataelewa watu kama nyie na sisi tutakapo kubali na kuongezea pale palipofikia sio kulauumu as if Slaa, Mbowe, Kitila, Baregu, Zitto, Julias na wengine hawataki. Wamefanya pao na bado wanazidi na sio kweli kuwa hawajui wapo wapi, wanafanya nini na wanaishia wapi.

  Sisi sote twende kwa wananchi, tutumie rasmimali zetu (time, money nk) kuwaelimisha, kupiga kelele, na vitisho.

  asante sana
   
 13. Elungata

  Elungata JF-Expert Member

  #13
  Apr 5, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 28,061
  Likes Received: 8,546
  Trophy Points: 280
  Lakini si invisble katoa sahihisho hapo na linaeleweka?naona kama people wanajump to the conclusion realy fast
   
 14. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #14
  Apr 5, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  NI MUSWADA KAMILI WA KUUNDWA KWA BARAZA LA TAIFA KURATIBU MCHAKATO WA KUPATIKANA KATIBA MPYA JINSI TUITAKAVYO WANANCHI KOTE NCHINI AU HAKUNA KABISA KITU MUSWADA KWA NJIA ZA ULAGHAI TENA!!!

  MUSWADA wa kuundwa kwa Baraza la Taifa la kuundwa kwa Katiba Mpya (ufafanuzi wa Dr Sengondo Mvungi) hakika ni A REAL TURNING POINT kwa uhai wa CCM kuendelea kwepo endapo watatii maoni ya wadau wote wa Mchakato wa kuandikw kwa Katiba Mpya bila ulaghai wowote au ndio lala salama na kwaheri ya kutawaliwa zaidi na hilo kundi dogo la MAFISADI wanaoichezea taifa jinsi wapendavyo wao.

  Tafadhali Wana-JF tawi la ofisi ya Waziri Mkuu, tawi la Wizara ya Sheria na Katiba, tawi la Makao Makuu CCM Dodoma, tawi la ofisi ya bunge au tawi letu la Ikulu Magogoni hebu fanyeni hima kutuwekea hapa jukwani nakala ya kilichopelekwa Dodoma kwa jina la MUSWADA ili vijana kote nchini tupate kujiridhisha kama kweli kuna mtu abatusikiliza au ndio tuseme tumendele kupuuzwa zaidi katika hili jambo la kufa na kupona kwa future yetu.

  Mnaweza hata kuweka PDF jinsi ndugu yetu Invisible anavyotufanyia mara kwa mara humu. Cha zaidi, wapiganaji wa ukweli kote nchini tukae mkao wa kufunga goli la kisigino hapa endapo uvumilivu wetu miezi hiyo yoooote itakua imechukuliwa mzaha kule bungeni Dodoma. Kwa zile njia zetu salamu zitafikishwa kwa kila kijana katika kila kijiji na kitongoji nchini bila shida.Wasomi wote katik vyuo vikuu vyetu ni sharti tuwe chachu ya mabadiliko tunayoyatamani ili kwa vitendo yatimie.

  Haki yetu kushiriki moja kwa moja katika kupanga, kuamua, kusimamia, kutoa hadidu za rejea, kutoa maoni, kuhakiki maoni, kupigia kura maoni kuwa katiba mpya kamwe hatupori mtu chini ya jua hili!!!!!!!!!!!!!

  Saa ya ukombozi iko karibu sana na historia ama kuandikwa ndani ya bunge au huku makwetu uswahili. Chaguo ni lao watawala katika hii ngwe ya lala salama.

  Wananchi kote nchini, Uwezo Tunao wa kupata aina ya mabadiliko kama ambavyo tunavyoyataka yawe; kote Bara na Visiwani. Vijana tukae mkao wa ushindi tangu sasa.
   
 15. M

  Mbuyi Member

  #15
  Apr 5, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 93
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 13
  Kwanza kama desturi naomba mnipokee kama mwan JF mpya. Leo ktk mjadala unaoendelea Bungeni, inaonekana Spika Makinda anamshangaa Zitto baada ya kutoa comments za kuomba mswaada (katiba mpya)usogezwe mbele ili wapate nafasi ya kujadilana na waliowatuma (wapiga kura wao). Je Mh. Zitto amesoma alama za nyakati au wakati umemkuta akiwa katikati?
   
 16. 2mbaku

  2mbaku JF-Expert Member

  #16
  Apr 5, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 317
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Iv kuna ugumu kiasi gani kutafsiri muswada huo kwa kiswahili? Iv itachukua muda gani kutafsiri muswada huo? Au hatuna wataalam wa kutafsiri? Mimi nisiyejua kiingereza ntajuaje kama nimepewa tafsiri halisi ya yaliyomo? Naomba muongozo!
   
 17. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #17
  Apr 5, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,870
  Likes Received: 6,610
  Trophy Points: 280
  Zitto ameshakuwa jepesi...
   
 18. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #18
  Apr 5, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Sio bure lazima na mental disorder
   
 19. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #19
  Apr 5, 2011
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Mswaada wame Udesa wewe, unafikiri wataweza kuupindua pindua.
   
 20. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #20
  Apr 5, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  Kwanini MUSWADA uandikwe kwenye kingereza wakati wananchi wanaongea kiswahili, lugha ya bunge ni kiswahili , lugha ya taifa ni kiswahili etc? ndio maana hawataki kuendeleza taifa ki elimu. Kama wameiandika kwa ajili ya wawekezaji kutoka nje sawa.
  LAKINI hii serikali isipo kua makini haya mambo yatawatokea puani!
   
Loading...