Muswada wa katiba mpya: Huyu professor lazima anahusika nao

Paranoia...number one symptom of a mob. Muacheni...he has a right to an opinion. Msitake kila mtu akubaliane na CDM au Shivji. Lazima mkubali kuwa kuna watu wanamtazamo tofauti.
 
Kwani ni lazima kusapoti?....hebu nipe composition ya mkutano wa kitaifa,halafu nieleze nani atawachagua hao wajumbe.
 
Muswada si lazima kila mtu au akubali au aukatae kama ulivyo, kila mtu ana haki ya maoni yake. Na hiyo ndio demokrasia.

Ukiachana na mswada wa katiba, leo hii kuna watu wanamini mungu Binadam, mungu N'gombe, mungu jua, mungu anaeonekana, mungu asiyeonekana na wapo wasioamini kabisa kuhusu mungu. Huyo ndio binaadam. Ingekuwa wote tunakubaliana kwa kila kitu tungekuwa ni ma-"robot".

Nikimaanisha kuwa sioni sababu kwa nini huyo professor akubaliane na yote wanayosema Shivji, Ulimwengu na mwingine yoyote, kumbuka Shivji na Ulimwengu pia ni wana CCM lakini na wao wana maoni yao binafsi.
 
Mkuu tupe jina la huyo prof. tufuatilie trend yake ili tumjue vizuri kwani ni ngumu sana kuchangia juu ya mtu usiyemjua... Na pili kukubaliana au kupingana kuhusu huo mswada ni jambo la kawaida kwani inategemea na faida anazopata huyo mtu kwa kukaa huo upande aliopo!!!
 
Back
Top Bottom