Muswada wa katiba mpya: CHADEMA wasitafute mchawi. Kosa lilikuwa ni kususia kuujadili bungeni. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muswada wa katiba mpya: CHADEMA wasitafute mchawi. Kosa lilikuwa ni kususia kuujadili bungeni.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jumakidogo, Dec 4, 2011.

 1. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #1
  Dec 4, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Binafsi nilikuwa nikiamini sana katika hoja nzito zilizokuwa zinatolewa na wabunge wa chadema mara kwa mara pale bungeni. Lakini kususia kujadili mjadala wa muswada tata wa katiba, kulikofanywa na wabunge hao kulitokana na jazba ya ghafla bila ya kufikiria madhara yatakayotokea mbele. Walikuwa na hoja nzito na sababu za msingi kuupinga mswaada huo ambapo watanzanzania kwa mamilioni wangepata somo kupitia kwao kwa hiyo hata kama ungepita kutokana na wingi wa wabunge wa CCM. Wangepata faida kubwa kwani mamilioni ya watanzania wangeona na kusikia pumba na mchele katika muswada huo. Naamini kwa uwezo wao mkubwa wa kujenga hoja. Kile walichokuwa wanakitetea kingekuwa na nguvu kuliko hali ya kutapa tapa iliyopo sasa. Mara nyingi hasira hasara, mpaka sasa sijafahamu sababu hasa ya kususia vikao vile. Kwa kususa kwao sasa kunawaghalimu watanzania walio wengi. Kwa hili hawawezi kukwepa lawama.
   
 2. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #2
  Dec 4, 2011
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,319
  Trophy Points: 280
  We subiri tu.... mwalimu Seif lazima tumpeleke jela kwa ufisadi anaofanya CUF. Unajaribu kupindisha hoja ili tumwache... Hatumwachi ngoooo lazima tumpeleke jela akanyee debe
   
 3. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #3
  Dec 4, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Jumakidogo,
  Naona jana ulilala unaiota CHADEMA!
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Dec 4, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  @Jumakidogo, kama CHADEMA hawakutoka bungeni nina hakika sote tusingekuwa tunajadili huu muswada wa katiba hapa. Na sio kwenye hili jukwaa peke yake hata huko mitaani watu wa kawaida kabisa wanaongea kuhusu muswada wa katiba, na wengi wanaonekana kukubaliana na CHADEMA kuwa ni mbovu. Kuna miswada mingine imepitishwa bungeni pamoja na kwamba ni mibovu lakini imepita na hakuna mtu anaongea chochote huku uraini! Inabidi upime matokeo ya CHADEMA kutoka nje kwa upana zaidi.
   
 5. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #5
  Dec 4, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Mangapi Mazuri wamejadili Bungeni yakakataliwa? Hili la Katiba ndo Mungu agewashushia Neema Wabunge wa CCM kupiga kura Kuupinga Mswaada kutokana na Chadema Kuujadili? Unakumbuka pendekezo la Sheria ya Mahakama la Lissu? Kwa mfumo wa Bunge hata Chadema wakikaa, kwenye issue nyeti hakuna anayewasikiliza..
  Pili uliona walivyotukanwa wakati Maelezo ya Lissu yanajadiliwa, so ulitaka watu wazima wake pale kutukanwa? Kutoka ilikuwa ni Busara ya Hali ya juu
   
 6. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #6
  Dec 4, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Siamini kama tukio lile lilikuwa limepangwa. Kulikuwa na makosa makubwa kwa spika yule mwanamke kukataa ule mwongozo. Lakini CDM hawakutulia. Mjadala unaendelea, lakini ni kwa sehemu finyu sana hasa kwa sisi tuishio mijini. Ningependa sana kama ngoma ile wangeanzia kuicheza palepale ndani ndipo mengine yafuate baadae.
   
 7. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #7
  Dec 4, 2011
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  umetumwa nini? mbona CUF walijadili na kupitisha lakini wameenda ikulu kurudia kitu kilekile au hilo hujaliona?
   
 8. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #8
  Dec 4, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Magamba yakishaamua yameamua tu! Kwani PM Pinda alipolidanganya Bunge alifanywa nini? Kwa kweli yule mama ameharibu sana hadhi ya Bunge!
   
 9. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #9
  Dec 4, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hebu twende taratibu, tuwe wakweli kwa nafsi zetu na tuache kupotoshana. Unasema 'watanzania kwa mamilioni wangepata somo...!!' Mamilioni ambao hawakusikia, hawakuona, hawakusoma wala hawakuitafuta hotuba ya Lissu! Unataka kutuaminisha kuwa wangepata somo kama tu Chadema wasingetoka bungeni!! Ikiwa pamoja na Chadema kueleza mara kadhaa sababu za wao kutoka nje bado umekuwa mzito kuelewa, unataka usaidiweje?! Mtanzania yeyote mwenye nia njema anayetaka kujua sababu atatafuta hotuba ya Lissu au atatafuta msimamo wa wanasheria na wadau mbalimbali juu ya muswada huo ulivyo hovyo na jinsi sheria na kanuni zilivyopindishwa.
   
 10. T

  Topical JF-Expert Member

  #10
  Dec 4, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nini kazi ya mbunge??
   
 11. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #11
  Dec 4, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Kugonga meza na kuchambua maisha binafsi ya mh. Tundu Lisu!
   
 12. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #12
  Dec 4, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo ulitaka lazima kile kilichoandikwa na Lissu ndo kikubaliwe. Nadhani unakumbuka nguvu ya hoja ya mbunge Manchali aliyebaki na kuchangia hoja ile. Wabunge wote wa CCM walikaa kimya. Chukulia kama wangechangia wengine zaidi ingekuwaje! Vyovyote vile kutoka haikuwa sahihi. Tusiwe watetezi wa kila kitu.
   
 13. T

  Topical JF-Expert Member

  #13
  Dec 4, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nafikiri ulikuwa una maanisha "Kukimbia na kutoka nje bunge kwa kuogopa kutetea hoja mfu au siyo"

  Ili wananchi wasijue kwamba hawana hoja wanakimbia..halafu wanakwenda kubembeleza kuonana na rais?? oops
   
 14. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #14
  Dec 4, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kwa swali lako hilo hapo juu unataka kumaanisha kuwa hotuba aliyosoma Lissu siyo msimamo wa Chadema! kwa hiyo ungekubali michango ya wabunge wengine wa Chadema lakini siyo Lissu!!!
   
 15. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #15
  Dec 4, 2011
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  @By Jumakidogo

  Jumakidogo Ujuwe Maalim Seif sio Mzaramu wala Mnyamwezi kwa hio Muungano ukivunjika utampata vipi kumuhukumu wakati Tanganyika itakuwa nchi mbali na Zanzibar?
   
Loading...