Muswada uliokwama kwa kukosa akidi kupitishwa leo bungeni ni kuhusu adhabu kwa mtu anaechakata taarifa za takwimu

eden kimario

JF-Expert Member
Jun 13, 2015
10,227
16,178
Dodoma. Muswada wa Sheria Mbalimbali namba 2 wa Mwaka 2018 ambao uliachwa Ijumaa wiki iliyopita kutokana na kukosekana kwa akidi inayohitajika kikanuni, leo utarudishwa kwa ajili ya kupigiwa kura ya uamuzi.

Kwa mujibu wa Kanuni ya 77(1), akidi kwa kila kikao cha Bunge cha kufanya uamuzi, itakuwa ni nusu ya wabunge wote kama ilivyofafanuliwa katika Ibara ya 94 ya Katiba.

Kushindikana kupitishwa kwa muswada huo kulitokana na Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee kuomba utaratibu kuhusu akidi ya wabunge kutotimia kufanya uamuzi. Mdee alimweleza Mwenyekiti wa Bunge Najma Giga kuwa kulikuwa na wabunge 67 tu kati ya 393 wakati shughuli hiyo ilipotakiwa kufanyika.

Akizungumza na Mwananchi jana, Giga alisema muswada huo utatolewa uamuzi leo.

“Kesho (leo) utatolewa uamuzi. Ni shughuli ya muda mfupi tu ya kutoa uamuzi,” alisema.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Bunge, leo wabunge watajadili muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali namba 3 wa mwaka 2018 ambao unajumuisha marekebisho ya Sheria ya Taifa ya Takwimu. Marekebisho hayo yanapendekeza adhabu kwa mtu anayechakata taarifa za takwimu na kuomba kibali katika Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kabla ya kusambaza takwimu adhabu ambayo inaonekana kuja kuwa mwiba kwa wadau.

Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT Wazalendo), Zitto Kabwe alisema marekebisho hayo yanazuia uchambuzi huru wa takwimu zilizotolewa na taasisi mbalimbali nchini.

“Unakumbuka 2007 nilikamatwa kwa sababu ya kufanya uchambuzi wa taarifa za BoT (Benki Kuu ya Tanzania) kuhusu uchumi? Sijapelekwa mahakamani kwa sababu ya Sheria ya Takwimu haikuwa na kosa hilo. Sasa sheria inafanyiwa marekebisho na nikifanya vile tena, ni jela miaka mitatu. Kifungu kipya cha 24A kinazuia uchambuzi huru wa takwimu zozote zilizotolewa,” alisema

Chanzo mwananchi
 
Kwani ile sheria ya awali ya takwimu Ilikuwa na mapungufu kiasi cha kuhitaji marekebisho ndani ya muda mfupi hivi?

Hii inaonyesha utungwaji wa sheria zetu una walakini sana na wabunge wanapaswa kuwa makini kwa kuisoma miswada vizuri na kuielewa na siyo kusema ndiyo tu.

Kama sheria zetu tunaweza kuachaacha loophole hivi vipi mikataba ya maliasili zetu si tutaishia kupigwa tu?
 
Walikuwa hawajaweka adhabu kwa mtu anaeongea sana kama zito
 
Hiv hii sheria ya takwimu itakuwaje kwa wanafunza wanofanya research? Hawataruhusiwa kitoa findings zao mpaka serikali ipitishe?
 
Kwani ile sheria ya awali ya takwimu Ilikuwa na mapungufu kiasi cha kuhitaji marekebisho ndani ya muda mfupi hivi?

Hii inaonyesha utungwaji wa sheria zetu una walakini sana na wabunge wanapaswa kuwa makini kwa kuisoma miswada vizuri na kuielewa na siyo kusema ndiyo tu.

Kama sheria zetu tunaweza kuachaacha loophole hivi vipi mikataba ya maliasili zetu si tutaishia kupigwa tu?
Hiyo sheria unatungwa kwa ajili ya Zitto peke yake, nyingine kwa ajili ya Twaweza, nyingine kwa ajili ya JF.... huko ndiyo tulikofikia.
 
Huu muswada ni mbaya sana, unazuia uwezekano wa watu kutumia taarifa na data "sahihi" kushauri, kukosoa, kuonya na kutoa muelekeo wa mambo ya nchi.
Kama wanadhani wanamkomoa Zitto, then basi waangalie 20 years from now tutakuwa na Taifa la namna gani baada ya wao kuondoka madarakani, Je wanataka tujenge Taifa la Hewala baba?, Tawile baba?
Kwa kweli inasikitisha sana yanayoendelea nchini sometimes!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom