Muswada wa Marekebisho Sheria-2020: Unajua watu hawataweza kudai haki kwa niaba ya Wanyonge? Viongozi wa juu Serikalini hawatashtakiwa moja kwa moja!

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,797
11,959
Asasi za Kiraia 220 zimefanya uchambuzi wa muswada huo wa sheria na kuwasilisha mapendekezo ya mabadiliko ya muswada huo kwa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria. Taasisi hizo zimeeleza kuwa japo kuwa zinafahamu muswada huo una lengo wa kusasisha Sheria iliyopo sana huku ikibaki kuendana na Katiba, ni mambo machache sana yanaenda na Katiba ya Tanzania ya Mwaka 1977

Asasi hizo zimesema wakati mambo machache yaliyopendekwa kwenye muswada huo yanaendana na Katiba au yanaifafanua Katiba vema, mambo mengi kwenye muswada huo yanakengeuka na kwenda kinyume na Katiba

Baadhi ya mambo yanayoenda Kinyume na Katiba ni;


1. Kifungu cha 7(b)(2) na 7(b)(3) of Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No.3) 2020
Mapendekezo ya mabadiliko ya sheria yanaruhusu wale tu walioathiriwa moja kwa moja na uvunjifu fulani wa haki kufungua mashitaka ya kudai haki zao. Mabadiliko haya yakipitishwa yatazuia raia wengine kufungua mashtaka kwa maslahi ya umma wanapohisi kuna uvunjifu wa Katiba.
Kwa maana nyingine, hutaruhisiwa kumtetea raia mwenzako hata kama hana uwezo wa kujitetea, hutaruhisiwa kutetea nchi yako kupitia Mahakama isipokuwa pale tu unapokuwa umenyanyaswa moja kwa moja, na hutaweza kutoa mchango wako kuilinda Katiba yetu. Hii inaondoa uzalendo.
>>> Mapendekezo hayo yakiwa hivyo, Ibara 26 ya Katiba inampa kila raia jukumu na uhuru wa kuilinda Katiba yetu kupitia Mahakama ya nchi.
Athari kwenye maisha ya kila siku: Kwenye maisha ya kila siku tulio wengi tunakutana na changamoto za hapa na pale. Kuna mifumo tofauti kutusaidia kukabiliana na hizi changamoto ikiwemo, kwa matatizo makubwa na magumu, mifumo ya Mahakama.
Kutoruhusu mtu au taasisi kufungua mashtaka bila kuathirika moja kwa moja inakulazimisha kujitegemea na kujitetea unapokutwa na unyimwaji wa haki zako unaohitaji Mahakama kuingilia.
Kuna watu wengi ambao wamesaidiwa kudai haki zao na mashirika tofauti ambao wanawasaidia kwa utalaamu, rasilimali na mikakati na kusimamia kwa ujumla mashtaka yao. Mabadiliko haya yatawaathiri sana wasiokuwa na uwezo na ujasiri wa kujisimamia wenyewe kisheria kama vile walemavu, watoto, wajane na makundi mengine mengi ya kijamii ambayo yamekuwa yakisaidiwa na watetezi wa haki za binadamu kwa maslahi ya Umma.


2. Kifungu cha 7(b)(4) na 18A na 65A of Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No.3) 2020
Mabadiliko ya sheria yanaondoa maana ya kuwa Jamhuri na badala yake tunaanza kulekea kwenye utawala usiokuwa wa kisheria kama vile utawala wa kifalme. Kwenye Jamhuri watu wote, wananchi na viongozi, wanaangaliwa sawa kwa jicho la sheria. Ndio tunaoita utawala wa sheria – kila mtu awe mdogo au mkubwa, anawajibika kwa kile alichofanya mwenyewe.
Kwa kuwatoa watu fulani kutoka mfumo wa kawaida wa haki, mfumo wa Mahakama, na kufanya hawawezi kuwajibishwa moja kwa moja, hata kama wamekiuka Katiba, inatupeleka kuwa na ngazi mbili za raia, wanaofuata sheria na wasiofuata sheria.
Pamoja na haya, misingi ya demokrasia na Jamhuri yetu ni mihimili mitatu ya Serikali, Bunge na Mahakama. Kila mhimili una majukumu yake na haitakiwi kabisa kuingiliana.
Mhimili mmoja unawajibisha mwingine kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo na haki. Hii haijalishi nani anashika cheo cha Rais, ni msingi wa Katiba yetu, nchi yetu na sheria zote za nchi.
>>> Ibara ya 13 ya Katiba inaeleza usawa mbele ya sheria kwa kila mwananchi na Ibara ya 4 inazungumzia mihimili mitatu ya Serikali na jinsi zinavyotakiwa kushirikiana, kila taasisi kwa uhuru wake.
Athari kwenye maisha ya kila siku: Kuna watu wanaopenda kusema demokrasia siyo chakula. Ukweli ni kwamba haki za mfumo wetu wa utawala, zinajulikana kama haki za siasa, hazionekani wazi kwenye maisha ya kila siku kama ilivyo kwa haki nyingine kama za kuishi na kupata chakula.
Tunaporuhusu baadhi ya watu kuwa nje ya sheria ambazo sisi wote tunazifuata, tunatengeneza mazingira tatanishi ya kutegemea utashi mtu moja au watu wachache. Wao ndio wataamua utamu na ugumu wa maisha yetu bila sisi kuwa na mchango wowote.
Mamlaka ya viongozi wetu wote yanatoka kwa wananchi na kila hatua inayotupeleka mbali na hilo, inazidi kupunguza uwezo wetu wa kuamua mwelekeo ya maisha zetu.


3. Kifungu cha 7(b)(2) na 7(b)(3) na 18A na 65A of Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No.3) 2020
Haya mabadiliko ya sheria yanawapa kundi la watu Mamlaka juu ya sheria na yanapunguza uwezo wa baadhi ya watu kudai haki nchini. Kwa sababu Mahakama ni sehemu ya mwisho kupeleka kilio chako ukinyimwa haki, hii ni sawa na kutomruhusu mtoto kulia unapompiga.
Tunahitaji kutoa dukuduku letu na kuamini kwamba tunapokanyagwa na mtu yoyote, tutafidiwa. Utawala wa sheria unategemea imani yetu katika mifumo ya sheria. Mifumo yetu ya sheria ikianza kuleta ubaguzi kuanzia kwenye sheria zenyewe ndio tunaelekea kuuua mfumo yenyewe.
>>> Ibara 26 ya Katiba inampa kila raia jukumu na uhuru wa kuilinda Katiba yetu kupitia Mahakama ya nchi
Athari kwenye maisha ya kila siku: Tunapofunga milango ya mfumo wa haki nchini ndio walalahoi wanakosa njia muhimu ya kufidiwa. Watu maarufu na wenye mahusiano na vigogo na wanasiasa wanaweza kuwa na njia tofauti lakini wananchi wa kawaida wanategemea mfumo wa Mahakama wanapodai haki zao. Wapi tupeleke kilio chetu haki zetu zikikiukwa?

Je, una maoni gani kuhusu muswada huu unaotarajiwa kupitishwa Bungeni hivi karibuni?

Pia, unaweza kusoma: Muswada wa Rais, Spika, Waziri Mkuu kutoshitakiwa unapangiwa siku mbili Juni 5&6 tena kwa hati ya dharura

Kusoma zaidi uchambuzi wa Vifungu vinavyokiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tafadhali tembelea PDF hii
 

Attachments

  • Misc_Amendments_No_3_of_2020_Preamble_&_Analysis_FINAL_220_CSOs.pdf
    985.6 KB · Views: 23
Sooo Sad. Kuna mambo mengine yanayoendelea nchi yetu unaweza ukafikiri unaota labda lakini ndo hivyo yanatokea. Ikitokea sheria ikapita Viongozi wa juu watakuwa wanafanya mambo ya ajabu na hakuna ambaye atakuwa anaweza kumshtaki.

Very sad.
 
Sooo Sad. Kuna mambo mengine yanayoendelea nchi yetu unaweza ukafikiri unaota labda lakini ndo hivyo yanatokea. Ikitokea sheria ikapita Viongozi wa juu watakuwa wanafanya mambo ya ajabu na hakuna ambaye atakuwa anaweza kumshtaki.

Very sad.

Kimsingi mpaka sasa viongozi wanafanya haya mambo, ila kwakuwa wamefanikiwa kunyamazisha umma kwa mbinu chafu, kwa kisingizio cha uzalendo, sasa wameona wajiwekee kinga ya maovu wayafanyayo.

Kinachofuata kwakuwa watakuwa na kinga, watamuongezea rais muda wa kukaa madarakani kwa nguvu,na hakutakuwa na uwezo wowote wa kuwashitaki. Njia pekee ya kumalizana na hili, ni nguvu ya umma kuchukua nafasi yake.
 
Kimsingi mpaka sasa viongozi wanafanya haya mambo, ila kwakuwa wamefanikiwa kunyamazisha umma kwa mbinu chafu,kwa kisingizio cha uzalendo, sasa wameona wajiwekee kinga ya maovu wayafanyayo. Kinachofuata kwakuwa watakuwa na kinga, watamuongezea rais muda wa kukaa madarakani kwa nguvu,na hakutakuwa na uwezo wowote wa kuwashitaki. Njia pekee ya kumalizana na hili, ni nguvu ya umma kuchukua nafasi yake.
Hizo sheria acha waweke kwa hila zao, ila ipo siku atapatikana mwingine asiyezingatia sheria na kuwawajibisha ipasavyo.

Kama wao wanaweza sasa vipi ije ishindikane baadae kwa mwingine.
 
Viongozi hawa wakuu wa nchi wanapoingia madarakani wanaapa kulinda katiba ya nchi. Sasa endapo watakiuka na kuvunja katiba kwa namna yo yote ile wanapaswa kuwajibika au kuwajibishwa.

Kitendo cho chote cha kuwalinda kwa uvunjifu wa katiba ni uhaini. Muswada huu wa kuwalinda viongozi hawa kwa kuvunja katiba ya nchi ni kuhalalisha uhaini, jambo ambalo hakikubaliki. Haiwezekani kabisa Rais aape kulinda katiba halafu aivunje kwa sababu yo yote ile aachwe bila kuchukuliwa hatua za kisheria.

Tanzania tutakuwa nchi ya ajabu duniani inayoamini katika demokrasia kuwa na sheria ya namna hii. Kwa namna nyingine tutakuwa tunaiambia dunia kuwa Rais wetu ndiyo katiba yetu na kwamba Rais anaweza kuichezea katiba yetu kwa kadri anavyotaka.

Wito kwa wote wapenda haki nchini kupinga muswada huu kwa nguvu zote.
 
DHANA YA MIHIMILI MITATU NDIO BASI TENA?

Marekebisho yanayopendekezwa kwa kifungu namba 4 cha Sheria ya Mapitio ya Sheria na Sheria ya Usimamizi wa Bunge (kifungu namba 115) yanawapa Rais na Mwanasheria Mkuu wa Serikali nguvu juu ya masuala ya Kibunge

Msingi mkuu wa Taifa lolote la Ki #Demokrasia ni mihimili mitatu ya Dola; yaani Bunge, Mahakama na Serikali kufanya kazi kwa uhuru na kuwajibishana

Kuingiliwa kwa majukumu ya mhimili mmoja ni kinyume na Katiba na misingi ya Kidemokrasia

SERIKALI INADHAMIRIA KUZUIA ULINZI WA KATIBA?

Ni haki ya kila mtu kuchukua hatua kisheria kuhakikisha ulinzi wa Katiba na Sheria - Katiba ya JMT 26(2)

Mabadiliko ktk Sheria ya Utekelezaji Haki za Msingi & Wajibu yanalenga kuzuia ufunguaji kesi kwa maslahi ya umma

Mabadiliko haya yanataka mtu kusimamia haki yake mwenyewe inapovunjwa na si ya watu wengine bila kuzingatia uwezo, utayari na hata umri wa wale wanaonyimwa haki

Je, kuna tatizo gani mtu mwenye uwezo na nafasi anapodai haki ya mwingine au ya umma kwa ujumla?




#Muswada2020 #Amendments2020

#Muswada2020 #JFLeo
 
Kuna mambo ukiyafikiria sana kwa taifa hili..... nikujinajisi waziwazi bila aibu.
 
Anayechezea katiba yetu ni rais, hao wengine anawachomeka tu ili isionekane lengo ni yeye. Na maadamu kufanikiwa kuua uhuru wa kujieleza na uhuru wa vyombo vya habari, huku akitumia madaraka yake vibsya kuchezea chaguzi za nchi hii, sasa hivi anajiwekea kinga binafsi na genge lake ili atawale kama wansvyotawala kina Museveni.

Ndani ya chama chake cha ccm hakuna anayeweza kumkanya maana karibia wote ni wachafu, na isitoshe ccm haiwezi tena kushindana kihalali na kupata ushindi bila kutegemea madaraka ya urais yanayotumika vibaya. Kwa hapa tulipofikia bila kuingia mtaani tutawaliwa kwa shuruti bila ridhaa yetu.
 
Back
Top Bottom