Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,498
- 9,279
Kuhusu Sheria ya Mawakili, alisema inalenga kuanzisha Kamati za Maadili za Mawakili kwa ngazi ya mkoa ili kurahisisha upatikanaji wa haki.
“Pia, kumwezesha mwananchi anayemlalamikia wakili kwa ukiukaji wa maadili kushughulikia tatizo lake katika ngazi ya mkoa bila ya uhitaji wa kusafiri kuifuata kamati ya maadili katika ngazi ya taifa," alisema.
Kwenye Sheria ya Usajili wa Vizazi na Vifo, muswada huo unapendekeza ubadilishanaji wa taarifa za usajili wa matukio muhimu baina ya taasisi moja na nyingine.
Kuhusu Sheria ya Majina ya Biashara, muswada unapendekeza majina ya biashara yanayosajiliwa yawe ni ya wale tu wanaokidhi vigezo vya kusajiliwa kwa madhumuni mahsusi.
Pia inapendekezwa kuongeza adhabu ya faini ili kuhakikisha adhabu inayotolewa na sheria inaendana na wakati na hivyo kuzuia utendaji wa makosa.
Katika Sheria ya Kampuni, muswada unapendekeza kuhakikisha watu wenye sifa ya kusajili kampuni ni wale tu wenye sifa na watapaswa kuwasilisha taarifa zao binafsi.
Pia, unapendekeza kuweka katazo au zuio la kusajili kampuni kwa watu waliowahi kutiwa hatiani au ambao taarifa zao zimetolewa na mamlaka husika kuwa mwombaji wamekuwa wakijihusisha na makosa yanayohusiana na utakatishaji fedha, ufadhili wa ugaidi, biashara ya binadamu, biashara ya dawa za kulevya au makosa mengine yanayohusiana nayo.
Inapendekezwa katika muswada huo kuruhusu watu wenye umri wa zaidi ya miaka 70 kuteuliwa kuwa wakurugenzi wa kampuni.
Kwenye Sheria ya Mahakama za Migogoro ya Ardhi, inapendekezwa kubadilisha muhula wa kushikilia nafasi kwa wenyeviti wa mabaraza ya ardhi na nyumba ya wilaya.
Muswada huo unapendekeza kufanya marekebisho katika Sheria ya Mahakama za Mahakimu ili kuwaondoa wazee washauri wa mahakama katika mahakama za mwanzo kwa kuwa mahakama hizo sasa zinasimamiwa na mahakimu wakazi wenye weledi wa sheria na hivyo kuongeza kasi ya utoaji haki kwa wakati.