Muswada: Kuanzisha "Mawakili" wa viti maalumu?

Lord Diplock MR

JF-Expert Member
Mar 16, 2015
1,393
3,234
MAWAKILI WA VITI MAALUMU

MAAJABU KIDOGO:
1. Unafuta BAR EXAM kwa Wanasheria kupitia kuelekea kupokelewa katika orodha ya MAWAKILI wa Tanzania.

2. Unaanzisha LAW SCHOOL OF TANZANIA kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Bar Exam, ili Wanasheria wote wenye LL.B waende kusoma ili wawe MAWAKILI.

3. Then ghafla Unaanzisha MAWAKILI WA VITI MAALUMU ambao ni Wanasheria wa Serikali au Watumishi wa Mahakama, eti wanapewa EXEMPTION wasiende kusoma kwenye Law School tena, bali wapewe tu "kama zawadi" kwa utumishi Serikalini au Mahakamani.

Yaani Tunaanzisha MAWAKILI WA VITI MAALUMU ambao vigezo vyao vitakinzana na vile vilivyowekwa na Sheria kuu.

Yaani leo ni sawa na Kuwatunuku DAKTARI wa binadamu kuwa DAKTARI BINGWA eti tu kwa sababu amefanya kazi ya kutibu kwa miaka kadhaa kwenye Hospitali za UMMA.

"Mawakili wa Viti maalumu"

A.k.a "Mawakili wa UPE"

A.k.a "Mawakili wa Mwendokasi."

IMG_20200610_175401_159.jpeg
 
Kuna watumishi wengine wametumikia nchi kwa kutukuka, sasa hadi Shule ya Sheria inaanzishwa aidha walikua ni waadhiri au kada yoyote chini ya serikali...sasa unakuja kumwambia mtu kama Kabudi, Majamba au Judge Ruhangisa arudi Law school asome ili awe Wakili, ilhali hao walimu wenyewe wa hapo Law School walikua wanafunzi wake!! kichekesho hiki.
 
Mkuu mbona ngumu kidogo kukuelewa? kuna bwana mmoja alifundishwa na mwalimu pale UDSM lakini baada ya miaka kadhaa yule mwalimu akaenda London School of Economics na alimkuta mwanafunzi wake akiwa mhadhiri pale na mambo yaliendelea bila mawaa kama unavyotaka kutuaminisha
 
Alipaswa kupita bar exams. Hii sio kosa letu, wakiwa vichekesho tutawacheka tu. Kwani wao walivyotukazia si tulikuwa vichekesho kwao??
 
Mkuu mbona ngumu kidogo kukuelewa? kuna bwana mmoja alifundishwa na mwalimu pale UDSM lakini baada ya miaka kadhaa yule mwalimu akaenda London School of Economics na alimkuta mwanafunzi wake akiwa mhadhiri pale na mambo yaliendelea bila mawaa kama unavyotaka kutuaminisha
Hiyo ni mara chache sana, kama kunguru kumnyea mtu. Sio kwamba ana shabaha.
 
Back
Top Bottom