Musukuma: Profesa Sospeter Muhongo usomi wake hauna faida kwa Tanzania

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Musukuma amemshukia mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo kwamba usomi wake hauna faida kwa Tanzania. Musukuma amesema ni wakati kwa Serikali kuwaamini wasomi aliowaita wa darasa la saba akidai kuwa wanakulia kwenye kazi.

Mbunge huyo ametoa kauli hiyo bungeni mjini Dodoma leo jioni Jumanne Aprili 13, 2021 katika mjadala wa mapendekezo ya makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi ya waziri mkuu mwaka 2021/22.

Amebainisha kuwa ni wakati wa Serikali kuwaamini watu wenye elimu ya darasa la saba badala ya kung'ang'ania maprofesa wasiokuwa na maana ambao wakati wote wanasubiri wengine waanzishe halafu wao wabebee ajenda juu kwa juu.

Amemtaja Profesa Muhongo kwamba wakati akiwa waziri wa nishati na madini alishindwa kufanya mambo mazuri lakini anashangaa kuona ameanza kuwa mkosoaji mkubwa.

"Mwaka 2016 nilimuita Profesa Muhongo nikamwambia kwenye haya makinikia tunaibiwa lakini alichukua kipaza sauti akatangaza hadharani kwamba Geita wamechagua mtu wa darasa la saba wamekosea sana," amesema Msukuma.

Amesema baada ya hapo walichukua mchanga wakaenda nao mbele ya rais wa awamu ya tano, Hayati John Magufuli na ilibainika kuwa mchanga huo ulikuwa na madini ya thamani kubwa.

Aprili 9, 2021 bungeni mjini Dodoma, Profesa Muhongo alisema uchumi wa gesi pekee ndiyo utakaoifikisha Tanzania kwenye uchumi thabiti na kukosoa mawazo ya kutegemea uzalishaji wa umeme mkubwa kwa kutumia maji.

Amesema Tanzania inatakiwa ijikite katika matumizi ya umeme mchanganyiko badala ya kutegemea mabwawa ya maji ambayo wakati wowote yanaweza kukauka.


Mwananchi
 
Tukubaliane kimsingi mbunge aliyeishia darasa la saba hawezi akajilinganisha na hata mtu aliyeishia form 4 katika uwanja mpana wa kupambanua mambo. Geita wamekula hasara
kama ilivyokuwa mbeya mjini na sugu
 
Niliwahi kumtembelea ndugu yangu pale Udom kwenye mabweni yao nikabahatika kuingia chooni,nilistaajabu kukuta kuta za choo zimepigwa Machata kwa kutumia kinyesi nilijiuliza sana juu ya hawa wasomi wetu kwa akiongeacho msukuma nakubaliana nae huenda hata Huyo Prof. Ni jamii ya hawa wachora kuta na kinyesi vyooni, kifupi si kila asomae sana basi jamii au familia yake itanufaika nae.
 
Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Musukuma amemshukia mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo kwamba usomi wake hauna faida kwa Tanzania. Musukuma amesema ni wakati kwa Serikali kuwaamini wasomi aliowaita wa darasa la saba akidai kuwa wanakulia kwenye kazi...
Ndugu wa-Tanzania, ifike wakati tuvitumie viungo vyetu tulivyopewa naMwenyezi Mungu kwa kazi iliyokusudiwa, mathalan tutumie bongo zetu kufikiri na midomo kutamamka yale yaliyo kwishafanyiwa kazi na bongo zetu.

Prof. Sospita nimemsikiliza kwa makini sana, ametoa ushauri mzuri tu. Sasa anatokeza mtu ametokea alikotokea anatumia mdomo kufikiri badala ubongo wake. Musukuma na Lusinde, msidhani wa-Tanzania ni wapumbavu sana wa kusikiliza porojo zenu.

Ni vyema mara nyingi kukaa kimya endapo huna uwezo wa kuchangia hoja kubwa za kisayansi
 
Tukubaliane kimsingi mbunge aliyeishia darasa la saba hawezi akajilinganisha na hata mtu aliyeishia form 4 katika uwanja mpana wa kupambanua mambo. Geita wamekula hasara
Eti hawezi kulinganisha na mtu wa form 4!! Ni ujinga mtupu!

Musukuma ni darasa la saba lakini ni milionea na ana kampuni la mabasi na biashara nyinginezo na amevipata kabla hata ya kuwa Mbunge sasa kimtazamo tu hiyo ni akili na uwezo wa kupambanua mambo katk kujikwamua.

Haya wewe tuambie nadhani pia wewe ni msomi ongeza na wasomi wenzio uliosoma nao vipi unamfikia hata nusu ya utajiri alionao Musukuma?
 
Niliwahi kumtembelea ndugu yangu pale Udom kwenye mabweni yao nikabahatika kuingia chooni,nilistaajabu kukuta kuta za choo zimepigwa Machata kwa kutumia kinyesi nilijiuliza sana juu ya hawa wasomi wetu kwa akiongeacho msukuma nakubaliana nae huenda hata Huyo Prof. ni jamii ya hawa wachora kuta na kinyesi vyooni,kifupi si kila asomae sana basi jamii au familia yake itanufaika nae.
Hahahah
Unaweza ukawa msomi lakini
Usiwe mstaraabu
Na unaweza usiwe msomi ukawa
Mstaarabu

Ova
 
Back
Top Bottom