Musukuma: Mke wa Diallo alipewa Ukurugenzi na Hayati Magufuli. Asema alimsaidia Star Tv ilipofungiwa na TRA

Kinuju

JF-Expert Member
Mar 20, 2021
1,354
2,000
Mbunge wa Geita vijijini Mh Musukuma amemkaanga na kumuonya Diallo kuwa ni mnafiki na aache mara moja tabia ya kumsema vibaya Hayati Magufuli kwani atamuumbua zaidi.

Musukuma amesema Hayati Magufuli alimsaidia Diallo pale Star Tv ilipofungiwa na TRA na pia alimteua mke wake kuwa mkurugenzi wa wilaya.

Musukuma ameenda mbali zaidi kwa kusema Hayati Magufuli ameifanyia makubwa Kanda ya Ziwa ikiwemo daraja refu kuliko yote Afrika la Kagongo Busisi, ujenzi wa meli mpya, ujenzi wa viwanda vya dhahabu na SGR kutoka Mwanza hadi Isaka.

 

Dumas the terrible

JF-Expert Member
Jan 20, 2021
1,328
2,000
Msukuma aache kelele akae akijua maji ya moto hayaunguzi nyumba

Kwahiyo Kisa alimteua mkewe Diallo ndio akikosea asisemwe

CCM Kuna nyumbu hawajitambui

Kwahiyo ndio maana mlikua kimya Kwa maovu yake jiwe kisa tu aliwapa teuzi?

Yaani napata hofu watu dizaini ya Msukuma ataweza agongewe mkewe na akakaa kimya kisa tu kapata teuzi

Daaaaa kichekesho!
 

Kabulala

JF-Expert Member
Oct 13, 2019
697
1,000
ajiuzulu kwasababu amefichua kuwa mlikua na mwenyekiti wa ccm mwenye file milembe??
Ajiuzuru kwasababu hakusema mapema mpaka Mwenyekiti wao akashinda uchaguzi mkuu twice...Diallo inabidi atuombe watanzania msamaha Kwa kukaa na taarifa hizi muhimu wakati wote.

Alikosa Sana..hastahili kuendelea kuwa kiongozi nchi hii...yeye ni hatari Sana kuliko aliyemwita kichaa..coz yeye alikua na akili timamu but yet akakaa kimya...Kwa ufupi Diallo ni Traitor
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom