Musukuma: Kuna wanasiasa wameahidiwa 10% kuweka presha ndege kuzuiwa

Majs

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
229
485
Habari waungwana,

Mwenyekiti wa CCM mkoani Geita na mbunge wa Geita vijijini, Joseph Kasheku almaarufu kama msukuma ameamua kujibu kombora la mwanasheria mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu kuhusu sakata la ndege ya serikali kuzuiwa nchini Canada baada ya wadeni kusema wanaidai Tanzania.

Msukuma kasema deni hilo halijatokana na serikali ya awamu ya tano kwani kazi ilifanyika mwaka 1999 lakini kama Rais haiwezakani kukataa deni la serikali inalodaiwa, ameongeza kuwa suala hilo liko mahakamani na katika hatua za mwanzo sana.

Msukuma ameongeza kuwa kwa sasa ndege hiyo ipo kwa watengeneza ndege kwani hata mitandaoni inaonekana na sio kwamba imekamatwa ila wadai wameenda kufungua kesi kuizuia isiondoke na serikali itapeleka utetezi wake.

Anadai suala hilo limewekewa 10% ili watu waweke presha ili ikatanda kwenye nchi watu waende wakavute 10%. Ametaka serikali ya awamu ya tano isiendelee kusikiliza maneno ya kipuuzi na watanzania pamoja na kuwa na haki ya kuangalia mitandao kusikiliza hizo presha, wangejikita katika maendeleo na kuachana nazo kwani nchi ina madeni mengi.

Msukuma amedai hata ndege za kwanza zilipokuja na kumwagiwa maji, Lissu alidai zimechemsha na wananchi wa kijijini wakaamini ilhali ilikuwa mila na desturi ya ndege mpya kumwagiwa maji, baadae wakadai zinaharibikia njiani wakati bado wanapanda nao.

Msukuma amesema kuchelewa ndege kwa mwezi mmoja kusiibue mjadala na kuwatoa kwenye 'mood' kisha kuwataka wabunge wenzake warudi kwenye majimbo kwani watanzania waliowachagua wana matatizo mengi na wao wanahitaji kwenda kuwasikiliza.



Kideo kwa hisani ya Millard Ayo
 
. ”Nimemsikiliza Tundu Lissu lakini tumesikiliza pia majibu ya Serikali yaliyotolewa na Msemaji wa Serikali. Kikubwa ni kuwaomba Watanzania tuendelee kujenga uchumi wetu wa Serikali ya viwanda. Kutoka kwenye uchumi tuliokuwa nao mpaka hapa tulipo na tunakoelekea.”
Hilo ndilo jibu?
 
Hivi kwani nyie wa chama hamuwezi kukaa kimya tu, na kuepusha kuendelea kujidhalilisha na kujivua nguo hadharani..? Ukweli siku zote utabakia ukweli.. Mtazunguka lakini mwisho wa siku ukweli utabaki kama ukweli na kila mmoja atauona huo ukweli.. Tuko kwenye karne ya 21, dunia kama kijiji..
 
Ona mwingine huyu huu ujinga uwendawazimu mnautoa wapi? Kwa nini wagumu kufikiri? Eti huyu naye wa kuisemea serikali no wonder tutadaiwa mpaka kope za macho. Msukuma 1+1=2 it's never 3. Simple mathematics Lissu anawasaidia ninyi mnabaki na kunyooshea watu vidole. 10% mliichukua ninyi sasa ina wacost mnaona Lissu shetani. Hii nchi ina viongozi au viongozwa kha?
 
Back
Top Bottom