Musukuma: CHADEMA hawana ubavu wa kumhoji na kumfukuza Lowassa. Mwenye mbwa hawezi ng'atwa na mbwa wake mwenyewe

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,075
4,111

Mwenyekiti wa CCM Geita na mbunge wa Geita Vijijini, Mh. Joseph Kasheku almaarufu kama King Musukuma tajiri wa Geita, amekishukia CHADEMA pamoja na Edward Lowassa.

Musukuma anasema KIDAMPA kama Lema hawezi kumshambulia Lowassa, kama wana uwezo wamfukuze kwenye chama.

Mimi nakuomba mzee Lowassa, hatua ulioinza ni nzuri, huku ndio kwenu. Hilo genge la wahuni hutoliweza. Rudi ukaombe radhi kwenye chama chako ambacho kitakuzika kwa heshima.

Lowassa kwenda kwenye lile genge la wahuni ilikuwa ni hasira tu, lakini halisi watu wenye maana tuko huku, ni busara tu arudi.

Rais wetu ana busara na hekima, sio kila mtu wa kumkaribisha. Wewe huwezi kumkaribisha mtu kama MBOWE, mnaenda kuzungumzia nini? Ataenda kuzungumzia nyanya zake zimeng'olewa na DC. Sio suala la kitaifa, ni binafsi.

Musukuma amesema upinzani wa kweli ni kukubaliana na yanayotendwa na mwengine na kama chama kilichoko madarakani kimefanya nzuri, uungwana ni kwenda kupongeza ila hofu kwa wahusika ni kuwa Lowassa anakimbia.

Ameendelea kusema mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe asiishie kufurahisha watu kwenye redio na mitandao ya kijamii, atoe kauli naye aone kama mwenye mbwa anaweza kung'atwa na mbwa wake mwenyewe kwani Lowassa ndio mwenye chama.
 
Attachments

  • DTKnTwLXUAAry8B.jpg
    DTKnTwLXUAAry8B.jpg
    19.4 KB · Views: 78
akili ndogo wataelewa Kwanini Lipumba baada ya kula Mgao wale kwa Ngoyai akili ikamrudi fasta akajua CCM Ina Wagombea wawili 2015

Chadema ni Bafu la Watuhumiwa wa Ufisadi wakishaoga wanajifuta wanarudi zao CCM

Tuhuma za Kupiga pesa kwenye vitambulisho vya Taifa Mh. Lawrence Masha alienda kuoga Chadema kwa Miaka miwili baada ya kutakata karudi zake home vizuri kabisa
 
CCM ni pango la wanyang'anyi
 
Back
Top Bottom