Musukuma aisifia DP world ya Dubai sakata la bandari. Adai Taifa linacheleweshwa na wajinga wanaotaka kushirikishwa kila kitu

juma30

Senior Member
Jun 25, 2022
149
421
SAKATA la kuuza Bandari kwa Mwarabu limezidi kuwagawa watanzania hapo Mbunge Joseph Msukuma amewashambulia watanzania wanaopiga kuuzwa kwa bandari kwa mwarabu.


==============

Mimi ni mmmoja wa Wabunge niliyeenda Dubai, kuona uwekezaji uliopo Dubai. Wala sijifichi. Nilienda kwenye ziara ya Kamati ya Mh. Mbarawa. Na mimi kidogo sijui unaweza kununua akili yangu kwa gharama gani maana mimi ni La Saba mwaminifu. NduguMwenyekiti, Tanzania tunachelewa kwenda kwenye maendeleo kwasababu ya Digrii – Risk Assessment, Mchakato; haya mambo yatatuchelewesha! Upembuzi yakinifu, jamani!

Hivi, unajengaje reli ya kisasa, ya matrilioni, kwenda Congo, kwenda Mwanza, halafu una Bandari inayotoa mabehewa 120 kila siku. Tunachelewa sana Mwenyekiti. Tunachelewa kwasababu ya watru wachache, wajinga ambao kila kitu unataka ushirikishwe. Sawa, tunataka tuletewe mkataba, humu kila mtu atachangia dakika 10.

Tumefika wakati sasa na wataalamu wetu wooote ni wajinga. Mpaka CAG anayetugombanisha humu naye ni mjinga, maana yake sisi tuna jicho lakini hatuamini.


Mimi nilienda Dubai na wabunge wenzangu kama 30 hivi, kule bandarini sikuona watu, ni mashine tu zinapishana.
Habari zaidi, soma:
  1. Sakata la DP WORLD: Rais Samia asema Serikali itatafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar, sasa kuchangia robo tatu ya bajeti ya nchi
 
Hivi kwa nini Wabunge hawataki kukubali kuwa huko tulikotoka mbunge kujua tu kusoma na kuandika ilikuwa sawa, lakini kwa sasa Elimu ya kuanzia iwe form 6. Yani hiki kitu akina Msukuma et al wanakipinga kweli. Haya sasa skia anavyoongea bila kufikiria.
 
Back
Top Bottom