SoC01 Mustakabali wa Elimu ya Tanzania na uhusiano wake kwenye masomo ya Ujasiriamali

Stories of Change - 2021 Competition

wakale kwanza

New Member
Jul 21, 2021
3
1
MUSTAKABALI WA ELIMU YA TANZANIA NA UHUSIANO WAKE KWENYE MASOMO YA UJASIRIAMALI.

ELIMU YA MSINGI

Tunapozungumzia Elimu ya msingi kwenye nchi kama Tanzania ni vizuri kujua umuhimu wa Kuhusisha Elimu hii na Elimu ya ujasiriamali.

Hususa ni Taasisi husika kukubali kuipokea Elimu hii ya ujasiriamali kama nguzo muhimu kwa kila mwanafunzi wa msingi, lakini ningependa Taasisi ya Elimu pia kufanyia kazi mpango mkakati huu kwa kuweka mchanganuo mahususi wa Elimu hii ya ujasiriamali kwa kugawa mtaala kulingana na ngazi za Elimu. mwaka 1964 uamuzi ulipitishwa wa kupunguza mafunzo ya elimu ya msingi kutoka darasa la nane na kuishia darasa la saba. Mfumo huu unatumika hadi leo. Lakini je katika badiliko hili kuna vitu vya ziada,vilivyoongezwa? Kwa upande wangu bado sijajua lakin kulingana na matokeo ya vijana hawa baada ya kumaliza Elimu ya msingi kushindwa kuweza kuwa na ufahamu japo thelusi au hata kufahamu tafsiri sahihi za ujasiriamali, ni dhahiri kabisa kujua kwamba tunapoanza kujenga nyumba ni lazima kujenga msingi,na kiufupi msingi ndo chimbuko la Nyumba. Tunapowatizama ndugu zetu wahindi ambao wanafanya Biashara hapa nchini ni dhahiri kwamba wanatupa changamoto kubwa kwa kutupa kuona ni jinsi gani watoto zao wanauwezo mkubwa katika kushughulika na maswala mazima ya ujasiriamali na kujitegemea katika umri mdogo. Tunapochungulia”SERA YA ELIMU NA MAFUNZO, SURA YA TATU, 3.0. HOJA NA MATAMKO YA SERA” ambao lengo lake lilikuwa ni Kuwa na mfumo nyumbufu wa elimu na mafunzo wenye tija na ufanisi na hivyo kuongeza idadi ya wananchi walioelimika na kuwa na maarifa kwenye fani mbalimbali. Kwahakika mfumo huu ulikosa

ELIMU YA SEKONDARI

Tunapogusa katika upande w a Elimu hii ya Sekondari.ni.ukweli usiopingika kwamba katika ngazii hii inahisika sana katika kumjenga au kumbomoa kabisa wakati tayari amekeishwa kutengenezewa msingi, wengi tutakua mashahidi juu ya takwimu nyingi tulizokwisha kuzisikia,kuhusu vijana wengi katika kipindi hiki wanaharibikiwa sana. Na kipindi.hiki ni kigumu kwa vijana kwakua ndo kipindi wanapokaribisha maisha mapya ya mabadiliko ya miili yaani kubalehe /kuvunja ungo, Elimu ya ujasiriamali ikiwa itapendekezwa kama mtaala mpya usiolenga kuwafundisha watoto kuacha shule na kujiajiri bali unaolenga kuwafungua vijana au wanafunzi katika uwezo wa kukabiliana na mapambano ya maisha au ujasiriamali pale tu atakapohitimu mafunzo/masomo yake ya Elimu ya juu.​

ELIMU YA CHUO KIKUU.

Unaporuka moja kwa moja na kutupa jicho katika upande huu wa Elimu ya chuo kikuu, ni vizur kufahamu ya kuwa hii ni Elimu ya ngazi ya juu, kwahiyo ni mahali pakuwekeza nguvu ndogo.ya kulainisha kijana ili Safari yake iendelee, ni.Muhimu kufahamu Tunazalisha vijana wengi kutoka Vyuoni wanaoshindwa kujiendesha wenyewe Maisha yao, je Elimu ya kupambana na mtaa wanayo? Jibu linaweza likawa sijui. Hii inaweza kupelekea kushiriki katika kazi hatarishi na wakati mwingine hata kupoteza maisha yao kwa kukosa msaada kwa kushindwa kujipambanua katika kuweza wa kuanza kujitegemea wenyewe kwenye kazi binafsi bila ya kuhusishwa na ajira.​

NINI KIFANYIKE?

Serikali na wizara husika ya Elimu inapaswa kuliangalia wazo hili kama ombi lenye kuonyesha tija kubwa kwa jamii na katika kuzalisha wimbi kubwa la Vijana wanaoweza kujiendesha na kujisimamia katika maisha yao kupitia Elimu hii.
 
MUSTAKABALI WA ELIMU YA TANZANIA NA UHUSIANO WAKE KWENYE MASOMO YA UJASIRIAMALI.

ELIMU YA MSINGI

Tunapozungumzia Elimu ya msingi kwenye nchi kama Tanzania ni vizur kujua umuhimu wa Kuhusisha Elimu hii na Elimu ya ujasiriamali.

Fact indeed. Safi sana
 
Back
Top Bottom