Mussa na Firauni walivyotufikisha hapa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mussa na Firauni walivyotufikisha hapa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, May 1, 2011.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  May 1, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu Zangu,


  TUMEKUWA tukitamka; Ukistaajabia ya Mussa , utayaona ya Filauni! Si wengi wenye kuyajua ya Mussa ni yepi na ya Filauni pia.

  Kuna simulizi niliyopata kuipokea. Kuwa alipata kutokea bwana mmoja. Yeye na mkewe walisubiri kwa miaka mingi kupata mtoto. Ikafika siku mkewe akatunga mimba. Na katikati ya kuilea mimba hiyo, bwana yule akapata safari. Naam. Akasafiri kwenda mbali. Nyumbani kamwacha mkewe mjamzito.

  Huku nyuma, mke akapata maumivu. Mganga akamwambia; ili mimba isalimike, basi, ni sharti ale maini ya mbuzi, na afanye hivyo kila anapopata mimba.

  Nyumbani hakukuwa na mbuzi wa kuchinja. Mama yule akaenda kwa ndugu wa mumewe mwenye zizi la mbuzi. Akamweleza shida yake.

  Bwana yule mfuga mbuzi akakataa katakata. Kuwa hawezi kuchinja mbuzi wake kwa ajili ya kupata maini ya tiba tu. Mama mjamzito akarudi nyumbani akiwa mnyonge. Na mimba ile ikaharibika.

  Mume aliporudi akasimuliwa na mkewe. Hakuamini masikio yake. Iweje nduguye amfanyie hivyo? Alijiuliza. Akafunga safari mpaka kwa Mussa kuomba ushauri.

  Alipofika kwa Mussa akasimulia kisa chake. Mussa alimsikiliza kwa makini. Na kwa vile aliombwa kutoa ushauri, basi, Mussa akamwambia; " Hayo yameshatokea, msamehe nduguyo!"

  Bwana yule akaushangaa sana ushauri wa Mussa. Kwamba amsamehe tu mtu aliyesababisha mimba ya mkewe iharibike! Basi, akafunga safari hadi kwa Filauni kupata ushauri wake. Filauni naye akasikiliza kwa makini kisa chote.

  Na kwa vile aliombwa kutoa ushauri, basi, akatamka; " E bwana ee, mimi naona umsamehe tu nduguyo!"

  Bwana yule akaupinga ushauri ule. Akamtaka Filauni aje na ushauri ulio na busara zaidi. Basi, kwa vile Filauni aliombwa aje na ushauri tofauti na wa mwanzo, naye akatamka;

  " Basi, mimi naona ni vema ukamkabidhi mkeo kwa nduguyo aliyekataa kumchinja mbuzi ili maini ya tiba yapatikane. Na akae na mkeo hadi atakapompa mimba. Na kwa vile mimba itakuwa ya kwake, basi, nduguyo atalazimika kumchinja mbuzi ili ipatikane tiba. Na mtoto akizaliwa, we nenda kamchukue mkeo na mtoto!"

  Naam, ndio hayo ya kustaajabia ya Mussa na kuyaona ya Filauni! Na siye tuliokulia pwani mtu akikwambia; " Acha Ufilauni!" Basi, ujue amekasirika.

  Ndio, na hata katika jamii yetu, na hususan kwenye fikra zetu, kuna mahali ambapo akina Mussa Na Filauni wamechangia katika kutufikisha tulipo sasa. Na hili nitalijadili zaidi huko twendako.

  Maana, mara nyingi, kama wanadamu, makosa tuyafanyao hutokana na makosa ya wengine. Tunachofanya ni kuyarudia makosa.

  Je, unafanyaje pale kipofu anapokuvamia na kukusababishia maumivu makali? Jibu; Utakasirika kwa sababu ya maumivu uliyoyapata. Hiyo ni hali ya kibinadamu.

  Lakini, ukiamua kulipiza kisasi, kwa wewe kujitoboa macho na kumvamia kipofu, basi, hapo utakuwa umetenda lisilo na busara. Na hilo ni Neno la Leo.Tafakari!

  Maggid
  Iringa,
  Jumapili, Mei Mosi, 2011
  http://mjengwa.blogspot.com
  0788 111 765
   
 2. PongLenis

  PongLenis JF-Expert Member

  #2
  May 1, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 423
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  nimeipenda artcle yako.. lakini naona kama umekosea .. ni FIRAUNI na SI FILAUNI
   
 3. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #3
  May 1, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,141
  Trophy Points: 280
  Afadhali sasa umeachana na zile siasa zako za maji taka kaka yangu Maggid.
   
 4. m

  maggid Verified User

  #4
  May 1, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Pong Lenis, asante sana. Isomeke Firauni na si kitu kingine!
   
 5. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #5
  May 1, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Nimekusoma.
   
Loading...