Musonye ashangaa mashabiki kupenda bure

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,069
253
KATIBU mkuu wa Baraza la Vyama vya soka Afrika Mashariki na Kati, CECAFA, Nichaolaus musonye amepongeza mahudhyuria makubwa ya mashabuiki wa soka, lakini akashangaa kuona Watanzania wanapenda bure.

akizungumza kwenye Uwnaja wa Taifa juzi, Musonye alipongeza wingi wa mashabiki hao na kusema lengo limetimia kwani hata wadhamini wanapenda kuona uwanja unajaa waweze kukidhi haja zao.

"Unajua watu wanashindwa kuelewa, uwanja upo mzuri, kwanini wanashindwa kuja kuona mechi, tena ni mara moja kwa mwaka, tumeweka kiingilia hakuna watu, lakini tumetangaza bure, watu wanajaa.

"Kweli sijapata kuona, watu wanapenda sana bure, lakini wacha wafurahi, hii ni CECAFA inapenda watu wake," alisema Musonye akizungumza na Mwananchi Jumapili.

Rais wa CECAFA alitangaza siku tatu za bure zilizokuwa zimalizike Ijumaa, lakini zimeongezwa siku mbili zaidi hadi leo na baada ya mechi hizo, hatua inayofuata mashabiki watalazimika kulipa.

"Tumetoa nafasi kwa mashabiki kuona bure mechi naamini wamepata burudani, sasa kuanzia hatua ya juu, itabidi walipe," alisema Tenga alipozungumza na waandishi wa habari katikati ya wiki iliyopita.

Hii si mara ya kwanza kwa mashabiki wa soka katika ukanda wa CECAFA kuingia bure, Rwanda imekuwa ikifanya hivyo mara kadhaa wakati mashindano hayo kwa ngazi ya klabu na timu ya taifa yanapofanyika nchini humo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom