Uchaguzi 2020 Musoma: Wananchi walalamika majina yao kuhamishiwa vituo vingine bila kupewa taarifa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Musoma. Baadhi ya wakazi wa kata ya Bweri manispaa ya Musoma wamelalamika majina yao kupelekwa katika vituo ambavyo hawakujiandikisha kupiga kura na kusababisha watembee umbali mrefu kwenda vituo vingine.

Wakizungumza na Mwananchi Digital leo Jumatano Oktoba 28, 2020 kwenye kituo cha Bweri FDC baada ya kutoona majina yao, baadhi walidai kuelezwa na wenzao kuwa waliyaona majina yao katika kituo kingine kilichopo takribani kilomita moja kutoka eneo hilo.

Alipoulizwa kuhusu hali hiyo msimamizi wa uchaguzi jimbo la Musoma mjini, Fidelica Myovela amesema majina yamehamishiwa katika vituo vingine ili kurahisisha upigaji wa kura, kusisitiza kuwa kila kituo kinapaswa kuwa na wapigakura 450.

"Mimi nilijiandikishia hapa (FDC) na uchaguzi uliopita nilipigia kura kituo namba moja, sijabadilisha kitu chochote sasa hapa jina halipo nimemuomba mtu aniangalizie kule Bweri Shule ya Msingi anasema jina lipo inakuwaje wanabadilisha vituo bila taarifa?" amehoji Eva Masenti.

Mkazi mwingine wa jimbo hilo ambaye hakutaka jina lake kutajwa amesema alijiandikishia kituo cha Nyamitwebiri Sekondari lakini alipofika katika kituo hicho jina lake halikuwepo na akalazimika kwenda kituo cha FDC namba moja na kulikuta.
 
Watumie simu kuangalia vituo *152*00# kisha wabonnyeze # kisha 9 kisha wabonyeze 1,halafu namba ya kitambulisho cha mpiga kura ila wasianze na T. Watajua kituo kipo wapi. Kama wameamua kupiga wapige tu ni kukomaaa.
 
Huyu mwananchi hata kuhakiki jina lake hakufanya na Bado analaumu serikali. Hii nchi bana tunajua laumu kuliko fanya kazi.
 
Mwananchi ukijaribu kumuhadaa ndio anazidi kutafuta HAKI yake CCM hawalijui hilo.

Ndugu zangu wa Musoma tembeeni hata umbali mrefu ili tuichague HAKI dhidi ya Udikteta.
 
Back
Top Bottom