Musoma wanakufa njaa, Chakula chao cha njaa kilipelekwa Igunga kuokoa jahazi wakati wa uchaguzi

theophilius

Senior Member
Nov 19, 2010
150
54
Kulingana na joji marato wa ITV, akimnukuu mkuu wa wilaya ya Musoma, chakula cha njaa kilichopangwa kupelekwa Musoma kilipelekwa Igunga wakati wa uchaguzi mdogo, na kwamba ndiyo sababu ya kuchelewa kuwapelekea wananchi waliokumbwa na uhaba mkubwa wa njaa wilayani humo, kiasi cha kushindia mboga za majani, mgagani. Haya, ama kweli walisema, kama ni wananchi kula nyasi na wale ili mradi, mradi wa serikali ya CCM ufanikiwe..
 
by: Eistein

Nikweli uliyosema nduguyangu, nami nimeyasikia na yamenisikitisha sana. Hao ndio viongozi wetu waliopaswa watuongoze kutoka katika matatizo, wao wanafanya maamuzi kwa maslahi yao binafsi, bila kujari kuwa kunawatu wanapoteza maisha kwa sababu ya maamuzi yao mabovu. Any intelligent fool can make things bigger and more complex... It takes a touch of genius - and a lot of courage to move in the opposite direction.Albert Einstein
 
Chadema kazi kwenu, ushahidi kwamba CCM walitumia njaa, kuwahonga chakula wanaIgunga, ili wapewe kura huo unaendelea kujidhihilisha, maana chakula hakikugaiwa kutokana na utaratibu, bali kililenga uchaguzi ndiyo maana kikachukuliwa chakula cha sehemu zingine hili wapewe hao wa Igunga...

Hivi kesi ya kupinga matokeo iliishafunguliwa?
 
Umenishangaza mkuu na statement yako as if wewe ni Mkenya huwezi kukemea rushwa Tanzania
 
mi mwenyewe nilishangaa.eti anasema "wale walikuwa na uchaguzi wasingepiga kula wakati wananjaa.yaani alikuwa anaongea kama katibu mwenezi wa ccm kumbe mkuu wa wilaya. ni hatari. mia
 
Umenishangaza mkuu na statement yako as if wewe ni Mkenya huwezi kukemea rushwa Tanzania

ukifuatilia kwa uakini (read btn the lines) utabaini kwamba lengo zima ni kuamsha hisia za kukataa vitendo vya ruswa za kitaasisi/watawala
 
Ni jambo la kusikitisha sana kuona watanzania wennzetu wanakosa chakula hadi kula mgagani. Lakini pamoja na kuilaumu serikali yetu, hebu tujaribu kuangalia, je juhudi za mwananchi mmoja mmoja katika kujikwamua na tatizo hili zinachukuliwa?

Kweli nawaambieni, wananchi wa mkoa huo baadhi yao hawajishughulishi na shughuli za kilimo pamoja na kwamba wanapata mvua za kutosha. Pamoja na kwamba ndiyo, serikali ina mdudu uzembe na imejaza mafisadi tujue kwamba kwa kuilaumu serikali kamwe hatutajikwamua na tatio hili.

Wananchi wa mikoa yote ambayo tunapata mvua walau mara moja kwa mwaka, basi tujitahidi katika kilimo ili kile tutakachovuna kitusaidie kwa muda wakati tukiendelea kutafuta namna nyinine ya utatuzi wa janga hili la njaa.
 
itv hawakutoa vizuri kama chanel ten, mi niliangalia zote itv na chanel ten yule mkuu wa wilaya alisema kipindi cha kampeni serikali ilipeleka chakula cha msaada igunga (ambacho ni cha watu wa shinyanga na musoma) ili washibe waweze kupiga kura, tena akasisitiza huo ndio ukweli hata kama unauma, kuwa wasingeweza kupiga kura wakiwa na njaa.

angalizo;
kuna hatari wenye njaa wakaua mbunge wao ili chakula cha msaada kije kwa wingi kwenye kampeni
 
Back
Top Bottom