• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Musoma: Wahukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kukutwa na hatia ya kumuua mtu kwa kumchinja

beth

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Messages
1,674
Points
2,000
beth

beth

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2012
1,674 2,000
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Musoma, imewahukumu kunyongwa hadi kufa watu watatu kwa kosa la kumuua Tabu Makanya (58) kwa kumchinja na kutenganisha kichwa na kiwiliwili.

Waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa ni Musiba Maregeba, Abeid Casimil na Ndaro Sumuni wote wakazi Kijiji cha Kwibara Kata ya Mugango Wilaya ya Musoma vijijini mkoani Mara, huku Wandwi Mugulu diwani wa Kata ya Mugango, akiachiwa huru.

Hukumu hiyo imetolewa na Jaji Girson Mdeme wa hiyo baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani na upande wa Jamuhuri.

Jaji Mdeme, alisema ametoa adhabu hiyo ya kunyongwa hadi kufa kwa washtakiwa baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na mashahidi saba pamoja na vielelezo vilivyotolewa mahakamani na upande wa mashtaka.

Awali washtakiwa hao walihukumiwa kunyongwa hadi kufa na Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza katika kesi namba 189/2013 ambayo hukumu yake ilitolewa Julai 14,2015.

Jaji Mdeme alisema, wakati washtakiwa wakisubiri kunyongwa baada ya hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, walikata rufaa ambayo ilisikilizwa na na Mahakama Kuu Kanda ya Musoma Agosti 16.

Washtakiwa hao walikuwa wakituhumiwa kumuua Tabu Makanya (58) mkazi wa Kijiji cha Kwibara Kata Mugango, ambapo Februali 21 mwaka 2013 majira ya saa 5.00 usiku walivamia nyumba ya mwanamke huyo kwa kubomoa mlango kwa jiwe kubwa marufu fatuma.

Ilidaiwa wakiwa na mapanga na tochi, baada ya kuingia ndani walitoa onyo kwa watoto wa Tabu na kuwata kukaa kimya bila kupiga kelele.

Baada ya kuwatisha watoto, walimvamia mwanamke huyo kisha kumchinja na kutenganisha kichwa na kiwiliwili na kukiweka ndani ya mfuko wa sandarusi na kuondoka nacho.

Ilidaiwa wakati watuhumiwa hao wakiwa katika harakati za kutoka eneo la tukio, wananchi walifanikiwa kumkamata mtuhuniwa mmoja akiwa na kichwa hicho.

Kuhusu diwani aliyekuwa amejumuishwa kwenye kesi hiyo, inadaiwa alikamata baada ya uchunguzi wa awali kuonesha kwamba yeye ndiye aliwatuma watu hao kumtafutia kichwa cha binadamu kwa makubaliano ya kuwapatia fedha.

Ilidaiwa kuwa, diwani huyo alitaka kichwa hicho ili kukitumia kishirikina kwenye masuala ya uvuvi wa samaki lakini baada ya jalada lake kupelekwa kwa Mwanasheria wa Serikali, aliondolewa kwenye kesi hiyo.
 
Perfectz

Perfectz

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2017
Messages
6,065
Points
2,000
Perfectz

Perfectz

JF-Expert Member
Joined May 17, 2017
6,065 2,000
AUAE KWA UPANGA ATAKUFA KWA UPANGA, SIO MIMI NI MAANDIKO YANASEMA
 
Raoluoroliech

Raoluoroliech

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2019
Messages
584
Points
1,000
Raoluoroliech

Raoluoroliech

JF-Expert Member
Joined Apr 15, 2019
584 1,000
Daaaah mkoa wa mara kila tukio ni la kugofya tu
 
interlacustrineregion

interlacustrineregion

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2018
Messages
7,215
Points
2,000
interlacustrineregion

interlacustrineregion

JF-Expert Member
Joined Oct 28, 2018
7,215 2,000
Amani ni bora kuliko mali na fahari
 
Kunde Ekeke

Kunde Ekeke

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2018
Messages
6,656
Points
2,000
Kunde Ekeke

Kunde Ekeke

JF-Expert Member
Joined Feb 5, 2018
6,656 2,000
Diwani kaponaje? Sheria zinakanganya
 
Kazitunayo

Kazitunayo

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2013
Messages
3,511
Points
2,000
Kazitunayo

Kazitunayo

JF-Expert Member
Joined Mar 30, 2013
3,511 2,000
Diwani chama gani hadi jina lake likatolewa
 
R

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Messages
21,314
Points
2,000
R

Retired

JF-Expert Member
Joined Jul 22, 2016
21,314 2,000
Mara nyingi court of appeal huwa wanaachiwa kwa sababu ya mess up ya ushahidi huko chini!
 
cocochanel

cocochanel

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2007
Messages
24,409
Points
2,000
cocochanel

cocochanel

JF-Expert Member
Joined Oct 6, 2007
24,409 2,000
Inasikitisha sana, hao watoto wa marehemu kuona unyama huo.
 
EvilSpirit

EvilSpirit

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2017
Messages
3,257
Points
2,000
EvilSpirit

EvilSpirit

JF-Expert Member
Joined Jun 15, 2017
3,257 2,000
Sijui kwanini alichagua kichwa cha huyo mama
 
Sir_Martine

Sir_Martine

New Member
Joined
Sep 9, 2019
Messages
1
Points
20
Sir_Martine

Sir_Martine

New Member
Joined Sep 9, 2019
1 20
Diwani anapona vipi hapo?...Huyo kiumbe achunguzwe tena maana kuna jambo hapo
 
GODZILLA

GODZILLA

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2014
Messages
4,047
Points
2,000
GODZILLA

GODZILLA

JF-Expert Member
Joined Dec 26, 2014
4,047 2,000
Ujinga umetamalaki miongoni mwa watanganyika!

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Farolito

Farolito

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2018
Messages
3,616
Points
2,000
Farolito

Farolito

JF-Expert Member
Joined Sep 10, 2018
3,616 2,000
Walihukumiwa na mahakama kuu kanda ya Mwanza wakakata rufaa mahakama kuu kanda ya Musoma.

Nilifikiri wangeenda mahakama ya rufani?
 
P

pye Chang shen

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2016
Messages
5,195
Points
2,000
P

pye Chang shen

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2016
5,195 2,000
Pole Sana kwao
 

Forum statistics

Threads 1,405,608
Members 532,052
Posts 34,490,473
Top